Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Saturday, December 9, 2017

Njia 31 ambazo zitamfanya msichana akupende zaidi na kufurahi



1. Mwambie yeye ni mzuri na sio uko sexy au hot

2. Mshike mkono wake kwa kuwa unampenda na sio unazingua

3. Mtumie sms nzuri ya kumwamsha asubuhi

4. Cheza nae michezo mingi na mfanye ashinde yeye

5. Mkumbatie mara kwa mara mgongoni kwa kumshtukiza

6. Usijirushe na x wako wakati yeye hayupo hayo sio mapenzi

7. Kama unaongea na binti mwingine mkiwa pamoja ukimaliza maongezi rudi na kumkisi mpenzi

8. Mtumie sms au kumpigia simu na kumwambia unampenda

9. Mtambulishe kwa marafiki na kuwaambia kuwa ni mpenzi wako

10. Penda kuzichezea nywele zake na kuzisifia

11. Jaribu kutoka nae hata kama atakataa

12. Onyesha kuumia ukigundua watu wanammezea mate

13. Mchekeshe kila mara kumfanya atabasamu

14. Mfanye alale mikononi/mapajani mwako akijisikia kulala

15. Kama amekuudhi wewe mkiss na kutomjibu vibaya

16. Onyesha hisia zako kwake

17. Kila mwanamke anahitaji zawadi tatu kutoka kwa mwanamme:(pafyumu,viwalo na mekapu seti)

18. Mjali kama unavyowajali marafiki zako

19. Mwangalie machoni mwake na onyesha kuvutiwa nae

20. Tumia muda mwingi weekend kuwa nae kwakuwa unampenda

21. Mkiss mvua ikiwa inanyesha bila kuwa na mwamvuli

22. Mkiss kuonyesha wampenda

23. Kama unasikiliza mziki mpe headphone ya pili nae asikilize

24. Ikumbuke birthday yake na kumpa zawadi hii inamaana kubwa kwake

25. Kila mara akikukosea jaribu kuonyesha haujaumia na unazidi kumpenda

26. Kila mara mpigie simu na kumwambia huta uumiza moyo wake na unamjali na unapenda kuisikia sauti yake

27. Mpe kila hitaji muhimu alitakalo

28. Onyesha kujali vitu vidogo afanyavyo kwani itampa imani zaidi

29. Usiwakumbatie mabinti wengine ukiwa nae

30. Ukiwa na muda jaribu kuwa nae jirani atakujali kwa hilo

31. Kama unamjali usimwambie ila onyesha kwa vitendo

Aina 12 za wanaume ambao binti hata awe mjanja vipi atakutana nao katika maisha yake


MR. THUG LIFE
Faida zake
Hukufurahisha na ya kukusisimua
Hufanya ucheke
Anakua pembeni yako kwa kila jambo na atakupigania na kukulinda
Hasara
Mara nyingi wanatabia za kunywa pombe na kuvuta sana sigara
Kila mra hakosi drama za kukushangaza
Atakuwa katika hali hiyo ya ukorofi milele
Kushikwa na kuwekwa jela ni kawaida yao kutokana na drama zao
MR. KWA SASA SINA MSICHANA
Faida zake
Atakuchukua na kukutoa out kila mara
Atakutambulisha kwa marafiki zake wote
Atakuwa ni mtu wa kukupa pongezi wakati wote
Hasara
Anamchumba ambaye wako naye kwa muda mrefu
Hawezi kukuambia kuwa ana mchumba
Baada ya kuteka moyo wako nawe umedata ndio atakuambia kuwa ana mpenzi
MR. MAARUFU
Faida zake
Atakupa fedha nyingi na hakuna kukulizwa maswali
Ana style nyingi za jinsi anavyoendesha maisha yake
Atakuonyesha baadhi ya mambo mazuri katika maisha yako
Hasara
Kamwe usije jaribu kuishika simu yake
Anamaamuzi ya kutokukushirikisha, anaweza kuja nyumbani kwako wakati wowote bila kutoa taarifa
Anapenda kuwa karibu na marafiki zake zaidi kuliko wewe.
MR. MISHEMISHE A.K.A JEMBE
Faida zake
Anaweza kukupa mialiko wewe na marafikio zako katika minuso mbalimbali na kumbi nyingi za
Unaweza kuwa na heshima na kila uongeacho na kuchochea mazungumzo pia
Anavaaa nguo za gharama
Hasara
Huwezi kujua kama yeye ni shoga au lah kwani hana kazi, muda wote yupo kwake na huoni dalili za kuhangaika lakini ana maisha mema na pombe kila siku
Hujifanya anakuwa mkali ukijaribu kumwelezea juu ya mpango wa mahusiano yenu kwenda mbele
Ukiwa bado kwenye mstari wa kupata tiketi uingie kwenye pati, au mnuso unaweza kushuhudia drama pale mlangoni na kisha mkaruhusiwa kuingia
Ana rundo la picha za yeye na celebrities kibao lakini hawajuani na mmpoja kati ya hao mastaa
MR. MSOMI
Faida zake
Muda wote yupo smart
Anakujali na kuhakikisha unajisikia vyema
c.Ana kazi nzuri sana
hasara
Mambo yake yanaboa sana kwani muda mwingi anahangaika na mambo ya kazi
Hata kwa bed ni mvivu sana kwana anakuwas kachoka na majukumu
Hayuko smart sana na mambo ya mtaani kama kukutoa out kwani anakuwa busy
Daima ni mtu wa kukuliza lini tutaonana tena
MR. GETO
Faida zake
Hukufanya ucheke
Anavutia kuwa naye karibu
Ana hasira za haraka, lakini kwa ujumla ni mtu poa
Atasema yeye anataka uhusiano wa kweli
Hasara
Ana watoto 3 au zaidi kwa mama tofauti
Anataka kukutumia apate chakula, fedha za matumizi na sio upendo
Na kila ukimwambia ukweli juu ya mambo yake anakataa au kuwa mkali
Kama ukikaa naer anaweza rudi hata saa tisa usiku na kujitetea alikuwa na marafiki
MR. RASTA
Faida zake
Atakufundisha mambo mengi ya upendo na amani
Yeye ni mwanaharakati au mwanamapinduzi
Atakupa maneno na falsafa zenye kukupa msukumo wa amani na ni maneno ya kihalisa yenye hisia
Anataka mke na familia
Hasara
Atakupiga chini akipata binti wa kizungu
Ana hela za kufanyia starehe ila hana kazi maalumu
Haimiliki suti nzuri, siku zote amevaa kombati au jinsi na kutokwa na jasho
Mwishoni utagundua kuwa alikuwa anakuigizia
MR. FUTURE
Faida zake
Atakutambulisha kwa mama yake
Ana kazi na atakuwa mtu wa kujirusha na wewe
Atakupa fedha za mahitaji yako kama unahitaji
Wakati mwingine huenda kanisani Jumapili
Hasara
Wakati mwingine naye anataka kuwa mtu wa kuishi free
Ni mtu wa kuvaa mikufu na saa fake
Kuna wakati yeye yuko busy na kufuatilia michezo aipendayo na kukusahau wewe kama upo
Baada ya kuachana ndio utagundua alikuwa ana mabinti kibao.
MR. KICHECHE
Faida zake
Atakuambia ukweli – kwamba wewe sio mmoja tu kwake
Yeye atakwambia kwamba umembadilisha na yuko tayari kutulia na wewe
Anakaa kwake ana usafiri na atakuomba uhamie pale make wote
Hasara
Hawezi kukutambulisha kuwa wewe ni mpenzi wake mkiwa sehemu hasa akiona kuna wanawake
Kwa ujumla yeye ni mzushi wa kila afanyacho
Anatarajia wewe kuamini uongo wake wote kwa sababu tu alikuambia ukweli kuhusu wanawake wengine alipkuwa nao
Baada ya kumdaka uongo wake atajitetea alishakuambia kuwa alikuwa kicheche
MR.NINA KAZI NZURI
Faida zake
Bila shaka ana kazi
Hana tabia nyingi mbaya sana
c.Atachukua wajibu wa kukuhudumia wewe wakati wewe ni mgonjwa
Atakwambia kwamba yeye ana upendo wa dhati na wewe
Hasara
Utadumu naye katika uhusiano wa miaka 2 au zaidi na kisha unakuja kugundua ni mvivu, mpuuzi na bedui ambaye anataka wewe kufanya kazi zote za mke lakini si kukupa pete.
Atamaliza kwa kukuambia anakupenda ila wewe sio chaguo lake
Baada ya kukuacha miezi mitatu baadae anafunga ndoa
MR. RAFIKI WA UHAKIKA
Faida zake
Yeye ni rafiki yako bora, uamweleza kila kitu kinachokusibu na mnakwenda pamoja vizuri sana
Anatoa ushauri kwa wakati unapopatwa na matatizo
Ni mwanaume wa kweli
mwelewa na anakujali na ni mcheshi wa kupindukia
Hasara
Manishia kujirusha na mwishowe unakuja kugundua hana lolote yeye anataka sex basi.
Hapo unahitaji kupata mpenzi mpya kwani yeye hana mpango wa maisha na wewe
MR. MWANAUME SAHIHI
Faida zake
Yeye anampenda Mungu na anachukua uhusiano wake na Mungu kwa umakini
Yeye ni mwelewa, ana kipaji na uwezo wa kukuchukua wewe kiakili na kihisia
Naye atakupenda hata wakati wewe haupendeki
Yeye ana ujuzi wa kufanya kazi kwa ustadi na anapendwa !
Anakubali makosa yake na inajitahidi kuwa mtu bora
Anaelewa uhusiano unajengwa kwa 200% . Yeye100% na wewe 100%
Yeye hana kundi la watoto wa mama, yeye ni nadhifu zaidi na anakitambua.
Yeye ni rafiki wa bora wa kweli na kila kitu unachotaka kwa mwanaume yeye anacho
Alikuwa mzuri ulivyokutana naye ila baada ya kukaa naye unagundua anazidi kuwa nadhifi zaidi
Anaweza kupangilia mavazi – anajua tofauti kati ya mavazi rasmi , ya kawaida, ya kitaaluma, ya biashara
Yeye anampenda mama yake na kuheshimu wanawake
Hasara
Hujawahi kutana naye na kama yupo basi ana mke au mchumba .
Yeye hataki uhusiano wowote kwa sasa
Umeshamsikia sana mtu wa aina hii lakini kamwe hujakutana naye na lazaidi umeshakutana na aina hizo hapo juu za wanaume na wakakuchezea vilivyo

MUHIMU KWA VIJANA WENZANGU.!



Wengi itakuwa bado miaka miwili, mitatu au minne kabla ya kutimiza miaka 30. Natambua kuwa kuna waliokwisha fikisha na kuna uwezekano kuna walio nyuma kidogo.
Kama katika umri tulionao sasa kuna mtu anakuambia wewe bado ni mdogo/mtoto, basi huyo mtu hakupendi na anakulemaza kiakili. Kua! Acha utoto! Mambo yafuatayo kwa vigezo vya kibinadamu mwenye akili timamu, mtu mwerevu lazima uwe ushayatimiza.


1) Kuweka misingi ya kifamilia:
Katika umri huo unatakiwa uwe umeoa, umechumbia au uko katika uhusiano wenye kueleweka unaelekea kwenye kujenga familia. Kama katika umri huu bado unabadilisha wanawake na kudandia vicheche, basi sahau kuwa na familia imara. Mambo yafuatayo yatakuwa yanakunyemelea;
– Kuoa/kuolewa msichana/mvulana mdogo sana ambaye atakuona unamzeesha
– Kuoa /kuolewa chapchap bila kuwaza
-Kuokoteza magonjwa ya hatari
– Kunogewa na usela na kusahau kuoa/kuolewa
2)Kujitegemea kiuchumi:
Hapa simaanishi kufanya kazi na kupata mshahara pekee, la hasha! Hapa nalenga wale watoto wa mama ambao pamoja na kuwa wana kazi na mishahara, bado wanalalama mishahara haitoshi na kukimbilia kuomba hela nyumbani wanapoishiwa mara kwa mara. Wale ambao bado wanakaa nyumbani hii inawahusu pia. Pia wale wanaotumia 100% ya mishahara kununua vitu vinavyoisha (consumption) wakingoja wapate hela nyingi au wazazi, ndugu na jamaa wawasaidie kwenye uwekezaji. Africa tunachelewa sana kwenye hii sector.
3) Kuwa na kitega uchumi:
Kama unadhani mshahara wako wa milioni kadhaa ni mwingi sana, ngoja augue mtu wa karibu au wewe mwenyewe halafu daktari akuambie mgonjwa wako/wewe ana/unatakiwa ape/upelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi wakati huna bima ya afya inayolipia hilo ndo utajijua kama mshahara wako heshima yake inaishia samaki samaki au inavuka border. Kitega uchumi si lazima uwe na mkampuni mkubwa, la hasha! Ila uwe na kitu cha kueleweka na chenye malengo ya kukua kuwa kitu cha maana. Kwa wale wagumu kuelewa, UNATAKIWA UWE NA PATO LA PEMBENI NJE YA MSHAHARA.
4) Makazi:
Uwe hata na kiwanja hapo Bunju Arif! Huezi kunywa bia kila weekend halafu wenzio wakiongelea issues za nyumba/viwanja/mashamba yao unakimbilia kubadilisha mada (Eti Huyu LVG wamuondoe kabisa anaharibu timu). Kumbe unazuga kupotezea story za viwanja/nyumba.
5)Uwe na professional qualification
: ACCA,CPA,CFA,CSIA,CPB, LAW SCHOOL ETC wale wa procurement wana ya kwao n.k. Ikifika huu umri kama CPA imekataa, tafuta hata mitihani za marketing upige, CPA sio issue zako. Lazima uwe na defined career (Kama hukubahatika kwenda kidato kingi, uwe na namna ya halali na ya kudumu ya kukupatia kipato). Umri huu kama huna utaalam katika fani yako, jiandae kuwa frustrated ofisini. Madogo wanasoma jamaa angu! Halafu wako tayari kupewa salary ndogo wapige kazi kuliko wewe.. So take care!
6) Uwe ushaamua ka hicho kitambi unakiondoa au unakilea:
Hapa sichekeshi! Kitambi kina madhara mengi. Suruali haikai vizuri, UTAPIGIWA, Kisukari, pressure n.k. Ukikinyamazia muda huu jua kitakuwa kishakomaa na majukumu yatakuwa mlima. Ukikiachia kijiamulie, kitakuganda kama “roba ya mbao” till death does you apart! Kama unakipenda endelea nacho, kama hukipendi uwe ushaweka program ya kukiondoa.
7)Uwezo wa kusaidia wanaokutegemea:
Kama we ni wa kishua, hapa hapakuhusu. Wewe ambaye si wa kishua, wazazi walikuwa na mategemeo flani walipokuwa wanakusomesha. Kama umefika miaka 30 hujaanza kuyatimiza mategemeo yao bila sababu ya msingi, jua watakuwa washakata tamaa na wewe.
8) Uwe na busara.
Kuwa mtu wa kufikiri kabla ya kutenda. Tengeneza haiba nzuri na ya kuheshimika kwa wanaokuzunguka. Kama huna busara hadi umri huu basi we sahau suala la busara ukiwa hai.. Labda utakutana nayo akhera.!
9) Savings:
Hapa nimeweka kizungu kuonyesha msisitizo. Kila mtu ana kipato chake. Ila formula ni kwamba angalau uwe ushahifadhi fedha sawa na mishahara yako ya mwaka na nusu gross of Tax kwa kipindi hicho. Kwa wale wagumu kuelewa namaanisha Ukiacha kazi au kusimamishwa kazi, uwe na uwezo wa kukaa mwaka na nusu bila kuingiza kitu chochote lakini uendelee kuishi maisha yale yale.
10) Umjue Mungu:
Nimeliweka hili mwisho si kwamba ni la mwisho kwa umuhimu, La hasha! Ni ili ulikumbuke zaidi. Mjue Mungu, mpende na umuogope. Nenda ibadani, soma neno lake na umuombe. Uwe na desturi ya kusali nyumbani kwako angalau kila unapoamka na wakati wa kulala. Kama humuogopi Mungu katika umri huu, basi wewe kwenda Mbinguni ni ngumu kuliko ngamia kupenya tundu la sindani (hata kama ni masikini).

NIKWANINI WANAUME HUCHEAT/KUWA NA MWANAMKE MWINGINE LAKINI HAWAKAMATWI

Wao hawatumii simu kuwasiliana

Msingi mkubwa wa wanaume wa aina hii wanatunza siri kuhusu wao wenyewe na familia zao, kazi zao hata majina yao wakati mwingine
HAWATUMII SABABU YA KUWA KAZINI
Mara nyingi mtu anaye cheat hutumia style moja ya kuwa kazi zinamfanya kuwa busy kumbe anatumia muda na hawala yake, hivyo basi wadanganyifu wa kiwango cha juu hawatumii sababu ya kuwa kazini kwani wanajua akianza kushtukiwa jambo la kwanza ni kuangalia muda anaotumia kazini.
HUHAKIKISHA MKE ANA FURAHA MARA ZOTE
Kwa kuwa atafanya kila njia kuhakikisha mwanamke anakuwa na furaha, hii ina maana kwamba mwanamke mwenyewe atajisahau na kujiona kuna amani kumbe ndani yake kuna udanganyifu mkubwa. Anaweza kukupa zawadi kila mara hasa akisafiri, anafanya kila kitu kuonesha anakujali kumbe anakuzunguka na inakuwa ngumu sana mwanamke kujua kwa sababu kila kitu anachohitaji anapata.
HAWATUMII SIMU
Wanaume wa aina hii si kawaida yao kuwapa mawahala namba za simu za mkononi, nyumbani au kazini. Wanajua kupitia simu za mkononi text message tu inaweza kuharibu mambo, acha kupigiwa simu kabisa. Pia wanajua wanawake ni rahisi sana likitokea jambo lolote ambalo hajaridhika au kukorofishana mara nyingi hupiga simu kwa wake wa hawa wanaume ili kuvuruga zaidi. Ndiyo maana hawatumii simu.
WANALIPA CASH BILA RISITI
Kawaida hawatumii credit card kulipia huduma zao kwani kuna bank huonesha matumizi ya pesa yako kwenye bank statement (hasa nchi zilizoendelea). Wanaogopa kwani kwenye account kunaweza kuonesha hotel na sehemu alienda na jinsi alivyotumia pesa.
Pia hawataki risiti kwani anaweza kujisahau akiwa nyumbani risiti ikakutwa kwenye mfuko wa suruali au wallet.
WANABANA MATUMIZI
Kawaida cheater mzuri hakopi pesa kwa ajili ya kustarehe na huyo mwanamke na pia anahakikisha matumizi yana balance na kuwa kama kawaida, hawana mambo ya ku-impress mwanamke kwa kutumia fedha nyingi hadi kukopa kwani wanajua matatizo ya kifedha yakitokea lazima atiliwe mashaka na kushikwa so mambo ya pesa wapo makini sana.
HAWADANGANYI OVYO
Hawana tabia ya kudanganya sana na mara kwa mara, kwani wanajua ipo siku data zitagoma bali wao huelezea uwongo unaofanana sana na ukweli ambao anayeambiwa anadhani ni ukweli kumbe ndani kuna uwongo.
Pia hawezi kueleza kitu hadi aulizwe pia anakuwa na majibu mafupi yasiyo na maelezo mengi ili kuficha data zaidi.
HAWATUMII MARAFIKI
Kawaida hawatumii marafiki au marafiki kuwasaidia kuficha siri zao. Wanajua marafiki kwa kuchemka au kwa makusudi wanaweza kufikisha habari kwa familia. Hujitunzia siri wao wenyewe na yeye tu ndo anajua kila kitu. Hata mwanamke ataambiwa asimwambie mtu na akimwambia mtu urafiki unakufa kwani anajua jinsi watu wengi wanavyojua issue basi uwezekano wa habari kuzunguka ni mkubwa.
WANAENDA MBALI
Kawaida cheaters wa aina hii si kawaida yao kutembea na majirani, marafiki, wasichana wa kazi au wafanyakazi wenzao au mtu yeyote ambaye yupo connected na mke wake, wao huenda mbali kabisa ambako hakuna mtu anawajua. Wanatumia ile principle kwamba ukiona mwizi anaimba jirani ndo kukamatwa kumekaribia, hivyo hawathubutu kuwa na wanawake wa karibu ambao jamii anaishi wanamfahamu.
KUMBUKA
Kuwa mwaminifu katika ndoa yako ndiyo jambo la misingi na muhimu si maisha yako tu bali hata familia, ukoo wako na jamii nzima.
Kumbuka kila mwizi ana siku yake ya arobaini hivyo basi hata kama hujagundulika ni vizuri kuacha hiyo tabia mapema ili uanze kujenga familia bora na yenye mafanikio pasipo wewe mwenyewe kuishi ndani ya guilt

Hii ndiyo tofauti ya mvulana na msichana kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Kila kunakokucha watu wanalalama kuwa siku hizi mapenzi hayan maana but ni kwa sababu wameshau kuwa kati ya mwanaume (mvulana) na mwanamke (msichana) wanatofauti kubwa kati yao, tofauti hizo ni kama zifuatavyo.
1. Mvulana anapomwona msichana kwa mara ya kwanza anamtamani na kumtathmini kama kweli anaweza kumfaa kwa matamanio yake mfano je ni mrembo, akitoka naye out atauza, je anamajivuno ama yupo kawaida, WAKATI msichana anapomuona mvulana kwa mara ya kwanza anamjaji kwa muonekano wake, mfano je huyu ana pesa, ana usafiri ama anafanya kazi ya maana au ndo hivyo tena SASA mara nyingi wengi hukosea hapo na kuwawekea aidha positive ama negative attitude kisa alivyo vaa.
2. Mvulana akiona msichana amemtamani kwa kiwango cha juu basi kinachofuata atamweleza kile anachohitaji wakati Msichana yeye atasikiliza kile mvulana atakachozungumza kwa kuzingatia vigezo alivyoviona aidha handsome ama tajiri anazitaka hela zake.
3. Kwa kuwa wavulana huona kwa macho na kupeleka akilini ( ANA ANGALIA, ANAMTAMANI, THEN ANAFIKIRIA ITAMCOST KIASI GANI KUMPATA YULE MREMBO) maana yake hilo jambo haliendi moja kwa moja moyoni bali ni kichwani WAKATI msichana yeye atasikia kile anachoambiwa then maneno kama ni matamu basi yataenda moja kwa moja moyoni bila kufikiria kwa umakini kwanini huyu mtu kaniambia ananipenda, ndo hapo atakapoanza kufikiria atakuwa too late.
4. Mvulana inamchukua muda mrefu kumpenda msichana ki ukweli ukweli wakati msichana inamchukua muda mfupi kumwamini mvulana kulinana na mwonekano wake.
5. Mvulana anapoumizwa huwa ni baada ya kukaa muda mrefu na msichana na kumwamini lakini anapoinvest love for Real anajikuta yupo kwenye dimbwi la tapeli wa mapenzi ila Msichana humchukua muda mfupi kuumizwa kwa sababu hakumchunguza sana mpenzi wake na alimwamini kwa kusikia kile anachosema mdomoni bila kujua kilichomo moyoni mwake, na anapogundua ndipo matatizo yanpoaanzia hapo.
ALL IN ALL TUNAPASWA KUHESHIMU MAHUSIANO YETU!

MAMBO MUHIMU YANAYOZIDISHA UPENDO KWA WAPENZI NI HAYA HAPA

Katika Mapenzi kuna vitu vingi unaweza kumfanyia Mpenzi wako ukamfurahisha na kumfanya azidishe Mapenzi ila katika safu hii nitazungumzia Mambo machache muhimu yatakayokusaidia kuboresha na kudumisha penzi lako kwa umpendaehttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEicg6B0pzLjVtC1e-Q-zRupC6AR0G87wahFow9oH2eT18qdcVsL-GjQVeUurAMrBwIHwHR1gqUMyOGhZRFP8uCwFjGo7_oLlYfz_fqW4dVYeoPa0t8V_5oniALH0T2M4Q8qvdIa577CKtM/s640/all-black-woman-husband-and-wife.jpg
YAFUATAYO NI MAMBO MUHIMU YANAYOZIDISHA UPENDO:
1.KUMNUNULIA ZAWADI MPENZI WAKO:
»
Zawadi ni moja ya sehemu husika katika Mapenzi inayoweza kufanya penzi likawa bora na lenye kupendeza siku zote, faham kwamba hakuna mtu asiependa kupewa zawadi na kila anaepewa zawadi siku zote hujihisi kama ni mtu anaependwa na anaejaliwa na kuthaminiwa hususani katika ulimwengu wa Mapenzi unapompa mpenzi wako zawadi basi faham ya kwamba utamfanya mpenzi wako ajione kama ni wapekee kwako na anathamani kubwa kwako hivyo hatosita kudhihirisha mapenzi yake kwako,
kikubwa zingatia pindi unaponunua zawadi kwa ajili ya kumpa mpenzi wako jitahidi kuwa mbunifu na uwe ni mwenye kubadilika sio kila siku zawadi zile zile zinajirudia kwa kufanya hivi utamboa mpenzi wako kuwa mbunifu na jaribu kumpa mpenzi wako zawadi zenye kutunzika mfano kama Card, maua, nguo n.k. Utamfanya azidi kukupenda zaidi na zaidi.
2. MSIFIE MPENZI WAKO:
»
Sifa zinaleta changamoto katika mapenzi. Unapaswa kutambua kuwa usiwe mchoyo wa sifa kwa mpenzi wako usisubiri watu wapembeni wamsifie mpenzi wako pindi anapofanya jambo zuri na lenye kupendeza chukua nafasi hii wewe kama kioo chake unadhani usipo msifia mwenza wako unataka nani amsifie?! Jitahidi kudhihirisha sifa kwa mpenzi wako kwa mfano umemuona mpenzi wako kapendeza basi usisite kumwambia "Sweetie nimependa vazi lako la leo ama hakika umetoka sex nakutamani zaidi ya siku zote navyokutamani ingawa siku zote unaziteka hisia zangu ila leo ni zaidi" unaweza kumpa maneno kama haya na mengine mazuri ya kuvutia, sifa zipo nyingi mbali na kumsifu mavazi yake hata tabia n.k. Kwa kufanya hivi utamfanya mpenzi wako azidishe mapenzi kwako kwani atahisi kampata mtu anaejali ubora na uhalisia wake kimaumbile na kimatendo. ZINGATIA:- Usitoe sifa ilimradi sifa zisizo na ukweli.
3. EPUKA KUMUUDHI MPENZI WAKO:
»
Sote tunafahamu kuwa hakuna binadamu aliekamilika na hakuna alietolewa nyongo kila mtu anakasirika na anakosea ila solution kubwa ni kudhibiti hasira na kurekebisha makosa na kusuluhisha hususani kwenye mapenzi, katika mapenzi hakuna jambo baya linalopunguza upendo kama ugomvi na kumuudhi mpenzi wako mara kwa mara. Ili kuboresha mapenzi na kulifanya penzi lako liwe imara na lenye kuvutia basi jitahidi kuepuka kumuudhi mpenzi wako na pindi ikitokea umekorofishana na mpenzi wako jaribu kutafuta suluhu mwite kaa nae muombe samahani iwapo kama unakosa na hata ikitokea kosa si lako pengine kakuudhi na bado unamuhitaji usikae na kinyongo wala usiumize nafsi yako kaeni muyamalize muendeleze mahusiano yenu na msiwe watu wa kuzungumzia tofauti zenu kwa watu wa pembeni. Kwa kufanya hivi daima mtakuwa ni mfano mzuri wa kuigwa na mapenzi yenu hayatofika kikomo zaidi yataendelea kushamiri.
4. MFANYIE YATAKAYO MFURAHISHA:
»
Kuna mambo mengi mazuri na yakuvutia katika mapenzi unaweza kuyafanya kwa mpenzi wako yakamfurahisha kwa mfano unaweza kusoma tabia ya mpenzi wako na ukajua ni nini anapenda na kipi hapendi kufanyiwa ukajitahidi kujilinda kumtendea asiyoyapenda na ukaufungua moyo wako kwa kumridhisha kumfanyia kile anachokipenda. Katika mapenzi watu wengi hupenda kutolewa Out, kupewa ofa ya lanch, kupewa zawadi zenye mvuto na zenye hamasa nzuri kwenye mapenzi. Unaweza kufanya vitu vizuri vyenye kuvutia kwa mpenzi wako vikamvutia ikawa ni nafasi nzuri kwako kumfanya azidishe mapenzi.
5. KUWA MTU WA UTANI KWAKE:
»
mpenzi msomaji ninapozingumzia mapenzi na maanisha mazoea yaliyoambatana na upendo, siku zote mapenzi hujijenga moyoni kwa mtu kutokana na ukaribu na mazoea yaliyopo baina ya watu wawili, katika pointi hii ya mwisho nataka nizungumzie utani katika mapenzi unafaida gani. Mpenzi msomaji fahamu yakuwa utani ni moja ya sehemu katika mapenzi na utani unasaidia kuboresha mapenzi ila utani ninaotaka kuuzungumzia hapa ni utani wa kawaida na sio ule wa kuvuka mipaka. Elewa wazi kabisa unapokuwa na mpenzi wako na ukawa ni mtu wa utani inakusaidia wewe kumfanya mpenzi wako akuzoee na awe anajisikia kuwa karibu nawewe muda wote kwani utakuwa unamfurahisha kutokana na utani wako. ZINGATIA:- Usivuke mipaka ya utani, usimtanie kupitiliza, mtanie kutokana na mazingira, usiwe utani unaofanana nakweli, mtanie kwa faida.

Naumia Sana Moyo Kwa Nayosikia Kuhusu Mchezo wa Kuruka Ukuta mpenzi Wangu Anaofanya

Tags
Kupenda kunaumiza kama hujawahi kupenda na usitamani kupenda kwa kweli ..na mpenzi wangu kwa kweli mtoto mashalaaa kaumbika na kajaliwa kiukweli yeye ananipenda sana kuna siku alinitamkia chochote nachotaka atanipa ili mradi nisimpoteze ..

Sana naumia maana nilipata habari na mtu wa karibu kua mpenzi wangu anaruka ukuta nilipuuzia nikaona hayo ya uongo sasa nimekuja kusikia tena juzi kwa baadhi ya watu kua huyu ni tabia yake kurishwa ukuta toka yupo chuo sasa nikipima na maneno yake kua chochote nachotaka atanipa picha inanijia maana kila tuwapo faragha ananiwekea mitego ya ajabu ajabu tuu ..

Sasa uyu nilikua na malengo nae aje awe mke sasa naingiwa na hofu unaeza oa mke anaefanya huo uchafu? sasa heshima si itashuka jamani? nifanyeje?

Mapenzi Sio Kujifungia Chumbani tu na Kufanya Ngon0

Tags
Mapenzi ni ubunifu, unaweza ukaona kitu kidogo lakini kitu hiko ukikifanya kwa mlango wa mapenzi kinakuwa kikubwa na hakiwezi kusahaulika kirahisi kwa mwenza wako. ukizungumzia mapenzi watu weusi wengi tunajua mapenzi ni kujifungia chumbani na kutiana tu, hapa ndo wazungu wanapotupiga bonge la gepu pale wakiwakamata dada zetu.

Basi ili kufanya mapenzi yako yaonekane mapya kila siku si lazima kila siku mjifungie chumbani kufanya staili mpya au sio lazima kila siku mtoke kwenda kula dina sehemu nzuri.

Unaweza ukamchukua mpenzi wako ukaenda nae sehemu ilio tulivu kisha mkaanza kusoma vitabu(hii inategemea na nyie wawili mnapendelea vitabu vya aina gani ila sio vya kemia au physics

Inapendeza sana mkiwa mmekaa pamoja mkisoma vitabu, mkabadilishana mawazo kwa kile kilichoandikwa kwenye kitabu. inaweza mkaenda beach(tulivu) au sehem ambayo unahisi mtakaa mtatulia bila usumbufu, mkasoma vitabu vyenu taratiiibu.

Unaamini Kuna Uchawi Katika Mapenzi? Soma Hii Inakuhusu

Tags
BILA shaka msomaji wangu uko poa, kwa wewe ambaye unasumbuliwa na shida mbalimbali za kidunia, nakuombea kwa Mungu upate ahueni. Wiki iliyopita tulianza kujadiliana kuhusu mada hii kama inavyojieleza. Je, wewe unaamini kwamba kwenye mapenzi kuna uchawi? Unaamini kwamba kuna kitu kinaitwa limbwata? Je, ni kweli mtu anaweza kwenda kwa mganga na akafanikiwa kumpumbaza mwenzi wake akili? Nakushukuru wewe uliyetumia muda wako kunipa majibu ya jinsi unavyoyaelewa mambo haya.

 Majibu niliyoyapata yalikuwa katika makundi mawili; wapo waliosema wanaamini ni kweli kuna uchawi katika mapenzi, wakaenda mbali na kutoa mifano iliyowatokea au waliyoishuhudia na kuwafanya waamini kwamba kweli kuna uchawi katika mapenzi. Msomaji wangu mmoja kutoka Unguja, Zanzibar, alisema anao ushahidi wa jinsi mume wa rafiki yake alivyoendewa kwa mganga na kimada wake hadi akafikia hatua ya kutelekeza familia ya mke na watoto watatu, akahamia kwa kimada. Unaambiwa mpaka leo hasikii haambiwi, ameikana familia yake kisa kimada.

Kundi jingine lilisema haliamini katika uchawi! Kwamba mume kumsaidia mkewe kuosha vyombo, kufua, kupika, kumpa kila anachokitaka au kutii kila anachoambiwa, siyo lazima awe amerogwa bali akioneshwa mapenzi ya dhati, yupo tayari kufanya chochote ilimradi mwenzi wake afurahi! Kwa wale walionitumia ushuhuda kuhusu limbwata, wengine wakilalamika kwamba wenzi wao wamebadilishwa mawazo na wanawake au wanaume wa nje mpaka kufikia hatua ya kuwakana wapenzi wao wa awali kwa sababu ya ndumba, nataka waelewe kitu kimoja muhimu sana.

 Mapenzi ya dhati yana nguvu kuliko hata mauti, vitabu mbalimbali vya dini vinathibitisha hili. Kwamba, ukimpenda na kumuonesha mapenzi ya dhati mwenzi wako, naye akakupenda, mkashibana, hakuna nguvu inayoweza kuingia katikati yenu, iwe uchawi, ndumba au majini na kuwatenganisha.

Hata kama kuna mtu anautazama uhusiano wenu kwa husuda, hata akikesha kwa waganga kwa lengo la kuwatenganisha ili yeye apate nafasi, ni sawa na kazi bure! Penzi la dhati lina nguvu asikwambie mtu! Hata hivyo, mapenzi ya dhati yanapokosekana ndani ya uhusiano, uwe ni uchumba, ndoa au mahusiano ya kawaida, ni dhahiri kwamba hata vitu vidogovidogo tu, vinaweza kuwatenganisha mkaishia kusingizia uchawi!

 Kama hampendani, mtu anaweza kuingiza maneno ya kuwafitinisha tu, mkaachana. Kama hampendani kwa dhati, ugomvi mdogo tu, unaweza kuwatenganisha, kama ni ndoa ikavunjika, kama ni uchumba ukaishia njiani na mambo ya namna hiyo! Kwa hiyo jambo la msingi, siyo kukimbilia kwa waganga mambo yanapoharibika ukiamini mwenzi wako amerogwa na mpenzi wa nje. Unachotakiwa kufanya kuanzia sasa, kabla mambo hayajaharibika, ni kuhakikisha kila siku iendayo kwa Mungu, unaishi vizuri na mwenzi wako.

Mpende kwa dhati, kuwa mwaminifu, mjali, msamehe anapokosea, mtimizie mahitaji yake ya msingi na usichoke kumrekebisha kwa njia nzuri ili mwisho aje kuwa bora!

Mkiishi hivi, hata atokee mchawi kutoka kuzimu, wala hawezi kuvunja ndoa yenu wala wewe hutahitaji kwenda kwa mganga ili kumroga au kumpumbaza akili asikuache, mapenzi yako ndiyo yatakayokuwa uchawi tosha. Lakini ikitokea mkaishi kwa mazoea tu, hakuna mapenzi ya dhati ndani ya nyumba, kila mmoja anajiona yeye ni bora, kiburi, dharau, usaliti, maudhi, uongo na kero za namna hiyo zimetawala, uhusiano wenu hauwezi kwenda popote na ninyi ndiyo mtakuwa wachawi wa penzi lenu.

Hata ukihangaika kwa mitishamba na hirizi, kama humuoneshi mapenzi ya dhati mwenzi wako, ni kazi bure! Siku akimpata anayemjali na kumuonesha mapenzi ya dhati, itakula kwako. Ni hayo tu kwa leo, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine murua.

SOMA HAPA UJUE NAMNA YA KUBUSU



Ili mfurahie busu mnatakiwa kupeana (umbusu-akubusu) hivyo ni jambo muhimu la kuzingatia ni kuto achama au kukusanya midomo yako kama unataka kubusu kwa sauti (kama zile busu za sauti za vijana mtaani) na badala yake busu kimahaba…..


Sogeza midomo yako kama ilivyo (umeifumba lakini iko-relaxed) kwenye midomo ya unaetaka kumbusu…..kisha itulize midomo hiyo juu yake na sasa toa “busu kavu” juu ya midomo yake kisha jitoe alafu rudi tena x3…..1)-inua uso wake kwa kutumia kidole (hii ni kwa wanaume) na mbusu moja kwa moja kwa kugusanisha pua kiaina…2)-Busu kwa kupindisha shingo/kichwa ili kutogusanisha pua zenu…3)-ukiwa umepindisha kichwa/shingo…mshike mkono au mkumbatie kiasi na busu tena.

Ukiona/hisi anajisogeza au anakupa ishara kuwa uendelee kwa kufungua mdomo kiaina, kukushika mkono/kifua/kitambi/kiuno au kuweka mkono kwenye bega basi endelea na “busu nyevu” kwa kubusu ktk mtindo wa kulamba-kunyonya mdomo(lips) wa chini na tulia hapo kwa sekunde chache kisha pokea ulimi wake kwa ulimi wako alafu ukwepe na kisha rudi kwenye midomo ya busu lip ya juu…..

Ongeza ujuzi wako sasa…na kumbuka kupumua kwa kutumia pua sio unampumulia mwenzio mdomoni….(atashiba hewa) au unabana pumzi (Mauti inakukumba). Unaweza kufumba macho aku kukodoa....inategema na wakati wenyewe.

Kuna aina tofauti za kubusu ili kutuma ujumbe kwa mpenzi wako lakini busu zote zinahusianisha ulimi na mate. Unaweza ukapewa busu wewe ukadhani ni kawaida (kama hujui) lakini mwenzio anakwambia amechoka, anakupenda, anashukuru, amefurahi kukuona, hataki kusex siku/wakati huo, hana raha/hujamfurahisha, anataka kuwa peke yake, anamachungu, yuko busy n.k.

Busu hizi zina jinsi yake ambayo utaijua kwa vitendo…..nadhani wabongo wengi hawajui unless wamewahi kufanya mahusiano ya kimapenzi na watu wenye utamaduni wa kubusu kwa mate/ulimi (Wazungu wazuri ktk hilo).

Baadhi ya watu hujiuliza kwanini wazungu wanapigana denda kila wakati lakini hawasisimki kimapenzi? Sio kila denda ni “nataka kusex” kuna denda nyingine za machungu au hasira, nakumbuka kama unampenda mwenzio lazima utahisi machungu yake sasa ku sisimka kutatoka wapi hapo ei?

Ongezea ujuzi na utundu ulionao ili na wengine wajifunze...karibu!

*HomeWork….muombe mpenzi wako akupe ma busu tofauti kuwakilisha hisia zake….kila la kheri!

USIJARIBU KUFUATILIA NYENENDO ZA MPENZI WAKO KAMA HAUWEZI KUVUMILIA MATOKEO.... JIFUNZE HAPA!!!


Siku za leo kilio cha wengi walio kwenye uhusiano ni kusalitiwa na wapenzi wao waliotokea kuwaamini sana. Wapo ambao si tu kwamba wanahisi bali wanawafumania kila kukicha waume/wake zao licha ya imani waliyokuwa nayo kuwa hawawezi kusalitiwa. 

Imefika wakati baadhi yetu hatutaki hata kufuatilia nyendo za wenza wetu tukijua kwamba kufanya hivyo ni kujitafutia presha za bure. Labda mimi naweza kuwa na uelewa tofauti katika hili la kufuatilia nyendo za wapenzi wetu. Ninachojua mimi ni kwamba, ili uwe na amani moyoni mwako juu ya mwenza wako lazima uthibitishe kama kweli anakupenda na ametulia. 

Utafanya hivyo kwa kufuatilia nyendo zake bila yeye kujua na katika kufuatilia kwako ndipo utajua kama kweli umempata mwenza sahihi ama laa. Wapo ambao husimamia kwenye ule msemo kwamba, ukimchunguza sana bata humli! Jamani ule ni msemo tu, tunajua kila mmoja ana mapungufu yake ila ni vyema ukayajua ya wako ili ujue namna sahihi ya kuishi naye.

Nalazimika kusema haya kwa kuwa, kasi ya wapenzi kusalitiana imekuwa ikishika kasi kila siku kiasi cha baadhi kuhisi bila kusaliti hawasikii raha. Yaani wanapatilizwa kila kitu na wenza wao lakini bado wanatoka nje. 

Unakuta mwanaume ana mke mzuri anayejua mapenzi na kila kitu lakini bado mwanaume huyo haridhiki. Pia wapo wanawake ambao wamebahatika kuwapata wanaume ‘handsome’, wanaojua mapenzi na kujali pia lakini bado tamaa za usaliti wanakuwa nazo. Ukiuliza kipi kigeni wanachofuata huko nje, jibu hakuna. 

Watu wa sampuli hii ni vyema kuwabaini kuliko kubaki na ile imani kwamba, anakupenda na hawezi kukusaliti. Una ushahidi gani kama kweli anakupenda na hakusaliti huko anakopita?

Hivi leo ukiambiwa utaje sababu inayokufanya uamini kuwa mwenza wako hachepuki utatoa sababu gani? Hakika huwezi kuwa nayo, sanasana utaishia kusema unamuamini kwa kuwa hujawahi kumfumania wala kuona dalili za kuzungukwa. 

Kizuri ni kwamba, ukifuatilia sana utagundua wengi wetu hutuna imani ya asilimia 100 ya kutosalitiwa. Wengi wetu licha ya wenza wetu kuonyesha wametulia, bado hatuwaamini kupitiliza. Hii yote ni kwa sababu akiamua kukusaliti anaweza kufanya hivyo na wewe usijue lolote.

Nilishawahi kufanya uchunguzi huko nyuma kwa kuzungumza na baadhi ya watu kuhusu hili suala la kusalitiwa. Wengi walikiri kujua kwamba wanasalitiwa lakini wenyewe wanadai ni mambo ambayo wakiyafuatilia hawawezi kudumu kwenye ndoa zao. 

Ni kweli niliobahatika kuongea nao kwenye hili ni wachache sana lakini maelezo yao yamenifanya niwe na uhakika wa hiki ninachokiandika leo. 

Kipi kifanyike?
Kutokana na maelezo yangu hapo juu utakubaliana na mimi kwamba hakuna anayeweza kusimama mbele za watu na kuthibitisha kuwa hasalitiwi. Kikubwa ni wewe na mimi kuwaamini wapenzi wetu.

Lakini pia hakuna ubaya kama utafuatilia na kujua kama kweli uliye naye ametulia na hachepuki. Usibaki kuamini kibubusa kwamba husalitiwi, wakati mwingine fuatilia nyendo zake bila yeye kujua. 

Najua kweli ukifanya hivyo unaweza kugundua madudu mengi kwa huyo uliyenaye na ukajikuta unachanganyikiwa lakini ni bora utakuwa umejua yaliyojificha ili uchague mwenyewe kusuka au kunyoa.

Heri ujue kisha kama huwezi kumuacha, uzungumze naye, abadilike kuliko umuache aendelee kufanya ufuska wake gizani kisha wewe ubaki na imani kwamba ametulia na hawezi kukusaliti. 

Lakini kama moyo wako unagoma kumfuatilia mpenzi wako na moyo wenyewe unakuhakikishia kwamba mwenza wako katulia, basi baki na imani yako hiyo.Lakini kwa ulimwengu wa sasa kama utakuwa umejihakikishia kwa asilimia 100 kwamba una mpenzi ambaye hajawahi kukusaliti na wala hafikirii, jiweke kwenye kundi la watu waliobahatika na Mungu awabariki sana.

UNA HAKI YA KUMPENDA, UNA HAKI YA KUMTOSA!

Hakuna ubishi mapenzi yanachukua nafasi kubwa katika maisha yetu. Mimi na wewe tunahitaji kuwa na wapenzi tena wenye mapenzi ya dhati ili maisha yetu yaweze kukamilika. Bila kuwa na mtu ambaye kuna wakati unammis, ukiwa naye unajiona ni mwenye bahati kwa faraja anayokupa, ni lazima utahisi umepungukiwa kitu muhimu.
Lakini wakati ukweli ukiwa hivyo, wapo wanaochukulia mapenzi kama kitu rahisi. Kitu ambacho anaweza kuingiza usanii na mambo yakaenda. Hapa namaanisha hivi, mtaani kuna watu wa aina mbili. Kuna ambao wanajua kweli kupenda. Akisema anampenda fulani, anamaanisha na kuna wale ambao wanaweza kusema wamependa kumbe wametamani au wana nia zao wanazozijua wenyewe.
Unamkuta mwanaume anadanganya kuwa ametokea kumpenda msichana fulani na ana dhamira ya kufunga naye ndoa lakini kumbe hana lolote, nia yake amuonje kisha aingie mitini.Achilia mbali hao, kuna wanaume ambao wanatumia pesa na utaalam wao wa kuongea kuwarubuni wasichana ili watembee nao kwa kipindi fulani kisha wakisharidhika, wanawaacha. Wavulana hao wapo na wamekuwa ni tatizo kubwa huko mtaani.
Lakini pia wapo wasichana ambao wenyewe wanajiita wa mjini. Yaani wao hawajui kupenda, wanachoangalia ni mwanaume ‘mwenye nazo’. Wakishampata, watajifanyisha kuwa na mapenzi ya dhati kupita maelezo kumbe hamna kitu, usanii mtupu!
Katika mazingira hayo sasa utaona ni kwa jinsi gani mapenzi yamekuwa janga. Ndiyo maana leo hii wapo wanaotamani kutojihusisha na mambo ya mapenzi kwa sababu hizihizi za usanii na ujanjaujanja mwingi.
Wakati mambo yakiwa hivyo, kuna baadhi ya watu ambao wamekithiri kwa tabia ya kuwatesa wapenzi wao kisa wameoneshwa kuwa wanapendwa sana.
Wapo watu ambao wakipenda wamependa kweli na hawawezi kujizuia kuonesha hisia zao kwamba ‘wamekufa’. Hatua hiyo sasa hivi badala ya kuwa changamoto kwa aliyependwa ili naye aongeze mapenzi, inakuwa tatizo.
Uchunguzi unaonesha kuwa, sasa hivi mwanaume akioneshwa kupendwa sana na mwanamke, atavimba kichwa na kumfanyia mwenzake kila aina ya visa eti kwa kuwa amebaini amependwa na hawezi kuachwa.
Hili halipo kwa wanaume tu. Wapo wanawake ambao nao kwa kujua kuwa waume zao wamekufa kwao, dharau inaongezeka, heshima inapungua na kufanya hata yale ambayo wanajua yanawakera wenzao.
Hivi kwa nini tufikie hatua ya kuwatesa watu ambao wameshindwa kujizuia kuonesha mapenzi yao kwetu? Kupendwa sana imekuwa nongwa jamani? Hujui kwamba Mungu anaweza kukupa adhabu kwa kutenda dhambi hiyo ya kumuumiza mwenzako bila sababu hasa katika ulimwengu wa sasa ambao kupendwa ni bahati?
Mbaya zaidi mtu anakutamkia kwamba anakupenda sana na yuko tayari kufanya lolote ili kukufanya ufurahi na wewe unajibu kuwa unampenda, kumbe hamna lolote. Matokeo yake sasa kadiri siku zinavyokwenda, unaanza kuonesha uhalisia kwamba humpendi kwa matendo. Hii siyo sawa na ni dhambi kubwa. Mimi nadhani kama humpendi mtu ni vyema ukamwambia mapema ili asikupe nafasi kwenye moyo wake.
Unapokubali kuwa na wewe unampenda kisha baadaye unaanza kumtesa kwa kumfanyia mambo ambayo hakuyatarajia, unafanya makosa na ni dhambi hata kwa Mungu.Kama kweli unapenda, mdhihirishie kwa matendo ili asiwe na shaka kwamba huenda ameingia kwenye penzi la kisanii.

ADHABU KUBWA YA MPENZI ANAYEKUSALITI HII HAPA!




Wanaume wengi wanapogundua kuwa wapenzi wao wanawasaliti, wanatunisha misuli kuonesha umwamba kwa kuwatwanga makonde wapenzi wao au kuwafanyia mbaya wale waliowanasa. Lakini uchunguzi wa watalaam wa mapenzi unaonesha kuwa ubabe haukomeshi tabia ya usaliti.
 Wapo wengi ambao wamewafumania wake zao, wamewapiga na kuwajeruhi, lakini wakajikuta hawakukomesha tatizo, zaidi ya kuwapa usugu wapenzi wao wa kuendeleza wizi tena kwa dharau na kejeli huku wakibembelezana kwa maneno kama vile: “mzushi kaenda kazini njoo sasa hivi Wanaenda zao Gesti au sehemu yoyote wanayoijua” au utasikia“vipi yule bwege alikuuliza jana ulipochelewa kurudi” Jamaa anaweza kumuuliza hivyo mke au mpenzi wa mtu.
 Katika hali ya kawaida usaliti ni jambo linalouma kwa kiwango kikubwa. Katika mapenzi hakuna suala la kuazimana mume/mke au mpenzi. Watu huazimana magari na pesa, lakini kwa mpenzi hakuna jasiri wa namna hiyo! Hivyo ndivyo inavyokuwa lakini, kupiga au kuachana baada ya kufumaniana kunasaidia? Jibu ni kwa hakusaidii, kwasababu ukimpiga adhabu inaishia hapo hapo,  kesho yake watakutana watakusaliti tena na kupozana machungu.Maamuzi ya kuacha naye hayasaidii kwani ukimwacha mpenzi wako hujamtibu, utakuwa umetoa mwanya wa yeye kuendelea kukusaliti na kukuumiza zaidi pale macho yako yatakapowaona wameshikana mikono mitaani kwa uhuru na raha zao.
 Kwasababu ukiamua kuua na wewe utauawa, huku wanadamu wenzako wakikucheka kwa uzembe wa kufikiri. Jamani usaliti upo kila siku, kwani si huwa tunawaona wake na wapenzi wa watu wanaingizana gesti kila siku?
 Sasa kama hujamfuma mpenzi wako leo kuna siku utakutana na meseji kali akibembelezana na ‘kidume chake’ mwingine kwa maeneo  fulani. Utafanyaje baada ya kubaini hivyo, maana kama ni tukio basi utakuwa umeona lile la stejini laivuuuuuu bila chenga. Twende pamoja ili tuelimishane kama wadau wa mapenzi njia sahihi ya kufanya ili kumwadhibu mpenzi msaliti.
 Kwanza, baada ya kuwaona uso kwa macho wakisaliti penzi, unatakiwa kutoa ishara zitakazoonesha kuwa umewaona, halafu ondoka eneo hilo. Ukishafika home, mtu mzima nini pale endelea kunywa zako maji ili kupoza presha. Akirudi mpenzi wako jitahidi kumkaribisha kwa bashasha, lakini usimuulize ulichoona mwache aendelee kujiuliza mwenyewe.Au kama umenasa meseji za kimahaba kutoka kwa mwizi wako, zitume kwenye simu yako kwanza, halafu baada ya kumaliza uchunguzi wako mtumie tena sms hizo mkeo/mumeo. Ukifanya hivyo usimuulize, endelea kumpenda na ikiwezekana ongeza matunzo. Nunua ‘mikuku’ akaange kila siku na umpe penzi moto moto.
 Nakwambia ukifanya hivyo mpenzi wako ataumia sana na hatoweza kukusaliti kwa kwasababu atakuwa anawaza unafikiria kumfanya nini? Na kwa yule uliyemshika naye, vivyo hivyo usizozane naye, mwache! Utashangaa anahama eneo maana atakuwa anafikiri unamwandalia kombora kumbe wewe wala, umeamua kujituliza tu!
 Wadau wa mapenzi hii ndiyo dawa ya mtu msaliti. Mwadhibu kwa upole, wanasaikolojia wameithibitisha adhabu hii ninayokweleza hivi sasa kuwa ina uchungu mara 1,000 zaidi ya kupiga au kukemea. Ukisema umwache siyo dawa kwani unaweza kutafuta mwanamke/mwanaume mwingine nayeye  akawa na tabia zile zile, sasa kama ikiwa utaamua kuacha, utaachana na wangapi katika maisha haya maana usaliti upo?
 Adhabu ya mpenzi anayekusaliti ni kumnasa kwenye usaliti wake kisha kumpuuza huku wewe ukiendelea na mambo yako kama kawaida, ukifanya hivyo utakuwa unamtibu ugonjwa wake wa kupenda penda hovyo na hii ndiyo dawa hasa ya kumponya msaliti, lakini pia inasaidia kupunguza maumivu ya penzi. Kumchunga na kumlilia machozi kili siku hakusaidii.

Njia 6 Za Kuuteka Nyara Moyo Wa Mwanamke

Tags
Je ungependa kujua na kufahamu mbinu za kumteka nyara mwanamke na kumfanya awe wako milele?
Relax, zama nami huku nikikueleza hatua za moja kwa moja za kufuata.

Kuteka nyara moyo wa mwanamke

1. Jizuie kumwambia hisia zako mapema
Ingawaje ni vizuri kumsifia mwanamke mara kwa mara, kumwambia hisia zako kwake ni jambo ambalo nalipinga. Unafaa umpatie muda wa kumfanya azungukwe na mawazo na maswali kukuhusu. Pia ni vizuri ujenge tenshen ya mapenzi kati yenu. Kando na haya yote, hisia zako kwake zinaweza kupotea baada ya miezi mifupi kama iwapo utagundua ya kuwa hamgawi maslahi yanayowiana. 
Hivyo, kama unampenda mwanamke jipatie muda mrefu wa kumsoma kabla hujamwambia chochote. Labda unaweza kumkeep buzy kwa kuingia kwa akili yake.
2. Mpe atenshen kwa kuwa makini
Ok najua unamuuliza maswali yafaayo ambayo yanamfanya avutiwe nawe, lakini swali ni je unamakinika na yeye ama ni runinga ama ni simu yako ndio inakukeep buzy?
Kosa ambalo wanaume wengi hufanya ni kutomakinika wakati ambapo wanazungumza na mwanamke. 
Kama kweli umepatikana na dharura basi ni bora kumwomba ruhusa ya kupokea simu nk. Kama hauna dharura yeyote, basi ni vyema kwako kumakinika na yeye. Bila hivyo mwanamke kama huyo ataona kama unampotezea wakati.
3. Jitenge na vifaa vya elektroniki
Baada ya kugusia swala la kumpa atenshen hapo juu, unafaa kujitenga na simu zako zote wakati ambapo unamtoa mwanamke deti ama out. Kama utashindwa kujizuia basi weka simu yako silent ama uizime kabisa ili usiingiwe na mawazo ya kufikiria simu yako.
Kufanya hivi hakutakupa nafasi ya kumakinika kwa mwanamke pekee, bali pia kutakusaidia wewe kuwa mbunifu, kuwa bila stress za kusumbuliwa kutaka kupokea simu za huyu na yule. Akili yako inatulia na kumakinika kwa kitu kimoja. Mwanamke.
Mwonyeshe ya kuwa unadhamini kikao chake na wewe. Mwonyeshe ya kuwa yeye ndiye kila kitu wakati huo na hauko tayari kupoteza muda huo ulionao na yeye kwa maswala mengine.
Kumbuka: Njia ya kuuteka nyara moyo wa mwanamke ni kuwa na maongezi ambayo yatamfurahisha na kumpendeza.
4. Hakikisha kila kumvutia kunahisabika
Kila mwanaume anafahamu umuhimu wa kumvutia mwanamke, lakini si kila mwanaume anafahamu umuhimu wa kila hatua ya kumvutia mwanamke. Wakati ambapo utakuwa unaongea na mwanamke, hakikisha ya kuwa kila kitu unachofanya unakichunguza na kutathmini. Hii nikuanzia miondoko yako ya mwili hadi hadi mwonekano wako.
Mwonyeshe wakati wote kuwa unajiamini na bila kusahau ya kuwa unajali maisha yako na ya wengine. Ukitelekeza chochote ambacho awali umemwambia basi kunaweza kuwa na tatizo kati yenu.
5. Msifie
Hapa ndipo wanaume wanapenda sana. Kumsifu mwanamke.
Well, hapa mnyeshee kwa kumsifu mara kwa mara lakini usipitishe mpaka. Iwapo kama umekuwa unadeti mwanamke kwa miezi sasa ni vyema zaidi kumsifia mara kwa mara ili usimfanye aone ya kuwa umechoshwa na mahusiano yenu. 
Kutomsifu mwanamke kwa muda mrefu kunatoa nafasi kwa wanaume wengine kuona mwanya wa kutumia kukuangamiza.
6. Usifiche siri yeyote
Kama unataka kuuteka nyara moyo wa mwanamke, basi usijaribu kumficha jambo lako lolote lile. Ufungue moyo wako na umwelezee chochote kile ambacho unaona anafaa kujua. Hii ni kuanzia changamoto unazopitia, maisha yako ya usoni na mambo mengine yanayofanana. Kufanya hivi kutamfanya mwanamke huyu kuona ya kuwa unamjali yeye. Wanawake hupenda wanaume ambao hawayafichi mambo yao. Well, si lazima umueleze kila kitu hapa. Muhimu ni kuwa unamwelezea mambo muhimu ambayo unayaona ya kuwa yanaweza kumuathiri kwa njia moja au nyingine.
 Ulikuwa ukiyajua haya yote? Kama ulikuwa huyajui mpira uko kwako sasa.

NAMNA YA KUONGEA WAKATI WA UTONGOZAJI, ILI KUMTONGOZA MWANAMKE KWA MAFANIKIO ZAIDI.

"Ulishawahi kujikuta unatamani kuliko kumtongoza msichana mzuri sehemu flani japo upate namba yake ya simu ila unajikuta huna jinsi yeyote au wazo juu ya nini cha kufanya au kuongea, unatamani kumfata nguvu miguuni zinakua zimekuishia unashindwa hata kupiga hatua moja kumsogelea, lile wazo pekee la kutaka kumsogelea linakufanya moyo uwende mbio, mikono iloane na jasho jembamba kukutoka huku akili yako ikishindwa kufikiria vizuri nini cha kuweza kuongea iwapo ukimsogelea?."
Unajua nini?, haipaswi kuwa hivi ndo maana Waulizewanaume ipo kwa ajili yako ili kumaliza maswala madogo madogo kama haya, kukuondoa katika mazingira ya kutokua na maamuzi dhabiti na kutokujua nini cha kufanya ndani ya sekta ya utongozaji na kukufanya uwe mwanaume kiongozi na mtanashati kwa kujua ni nini cha kufanya na mda gani unapaswa kukifanya ili kuwa mtaalamu katika sekta ya mahusiano.
Kujiamini ni kitu kinachochukua nafasi kubwa na ndo msingi mkubwa katika mahusiano na hasa wakati wa utongozaji, na ndicho kitu mwanamke hutumia kumpima mwanaume na kumpa nafasi ya uwezekano wa kuwa na yeye au la, ila mara nyingi mtu hushindwa kujiamini kutokana na hofu ya kutokujua ni nini cha kufanya au kuongea wakati wa utongozaji.
 
 DOWNLOAD APP NZURI SANA YA SMS ZA APENZI BOFYA HAPA ==> https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sms.za.mapenzi.za.kiswahili
 
 
Mwanamme ambaye huwa hafanikiwi kwenye utongozaji hufanya makosa madogo madogo kama kumpandisha hadhi mwanamke anayemtongoza mpaka kiasi ambacho anaifanya hadhi yake binafsi kuonekana ndogo na siyo tu anamtongoza mwanamke kwa wasiwasi na kutojiamini, bali anamtongoza hovyo hovyo bila mpangilio na zaidi ya hapo anamuweka wazi mwanamke kwamba anataka kumjua zaidi ya kawaida na anajitangaza bila kujijua kwamba, anahitaji na huyo mwanamke apendezwe naye hapo hapo.
Nayajua haya kwa sababu kwa muda mrefu na mimi nilikua hivi hivi, mtaalamu wa utongozaji huwa anasubira na huwa hapaparuki hovyo hovyo tu, kutongoza ni sanaa na inahitaji uelewa mkubwa na hata mimi iwapo ningelikua ndo huyo mwanamke sidhani kama ningelikubali hivi hivi, lazima atake kukujua kwanza ndo mambo mengine yafuate.
Ukitaka kuishia kusonywa na matusi juu ingia na mstari wa "Dada samahani nimetokea kukupenda nataka tuwe wote, kila nikikaa nakuwaza wewe, nikinywa maji nakuona kwenye glasi", bila kuangalia mazingira na papara za kusema yaliyo moyoni mwako, huu mstari lazima utakutokea puani, mwanadada ndo amekuona siku hiyo hiyo, hata alikua hajui mtu kama wewe upo katika hii dunia, hakujui na unategemea akuambie anakupenda
pia
, we vipi?, hapo unapoteza nafasi na utaishia kuambiwa usiyoyataka na kuumia moyo tu.
Naamini kabisa mwanaume yeyote mwenye mtazamo sahihi na mwenye hamu ya kujifunza anaweza kuelewa jinsi ya kutongoza mwanamke sehemu yeyote na mahali popote pale, kutongoza hakuitaji kukalili mistari ya kutongozea wala kumpulizia dawa kutoka kwa mganga, kama unania ya kujifunza endelea kusoma nakala za waulizewanaume.
Mwanaume mtongozaji hajishushi na anatumia mbinu ya kuonyesha ujasiri wa kimaongezi na akiongea na mwanamke, mwanamke hutambua ya kuwa huyu jamaa ana nia naye kutokana na lugha anayoitumia wakati wa maongezi.
Makosa makubwa mawili ambayo nilikua nafanya wakati wa kutaka kumtongoza msichana, nilikua nasubiri na kusita kwa muda mrefu na kutojua nini cha kuzungumza.
"Unakuwa na dakika tatu kutoka unapomuona msichana anayekupendeza na mpaka pale utakapomsogelea na kuanzisha mazungumzo yanayompendeza, ukisubili sana nafasi yako itakupita kama upepo na kupoteza nafasi hiyo muhimu".
Kama ni kwenye sherehe ndipo ulipomuona, piga moyo konde na mwendee na mwambie,
>>"Nimekuona kutoka mbali ila moyo wangu ukang'ang'ania mpaka nije nikusalimie, mambo?"
>>"Siku yako inaendaje?"
>>"Upo upande wa bibi harusi au bwana harusi?"
>>"Oooh, upande wa bibi harusi, ndo maana dada yako amewahi kuolewa!, ukoo wenu mzima inavyoonyesha umelaaniwa kwa uzuri!"
Mchokoze kwa maneno matamu, muulize maswali ya kumfanya afurahie maongezi na kama ukiwa unatoa sifa ifiche ndani ya sentensi inayovutia, ukitaka kumjua uliza maswali ambayo majibu yake ni mepesi na rahisi, kama ukitaka kujua anachofanya muulize,
>>"Kwa hiyo familia nzima mwanafunzi amebaki ni wewe tu, maana dada yako tayari ameshaolewa?"
Kwa maswali ya namna hio atajikuta anajiongelea kuhusu yeye na kukufanya akuzoee mapema, na ukiona maongezi yanaelekea ukingoni unatakiwa unakuwa shapu na mbunifu kwa kuanzisha mada nyingine inayovutia zaidi, itakayoleta maongezi matamu zaidi.
Kujua kitu cha kusema wakati wa kutongoza ni ngumu, ila inabidi ujiamini na ufanye kujisahau na kuweka akili kama upo unaongea na dada yako ila maongezi yaweke yawe ya kuvutia zaidi na uyapambe kwa sifa bila kuonyesha nia yako moja kwa moja, mwisho wa maongezi muombe namba ya simu au omba umtoe mtoko akuonyeshe maeneo hayo maana wewe ni mgeni na maongezi yamekupendezea na ungependa kuyaendeleza siku nyingine.
"Ukweli ni kwamba haijalishi utakachokiongea, unaweza ongelea kitu chochote kile ili mradi maneno yawe katika hali nzuri kihisia, onyesha tabia ya kujiamini na mipaka yako."
Acha kuwa na wasiwasi na kufikiria nini cha kuongea, we mfate kwanza na maongezi yatajitengeneza yenyewe kwa jinsi ya mazingira mliyopo na weka akilini kitu kimoja, huyo msichana unayeenda kumtongoza inawezekana anatongozwa mara tano au zaidi kwa siku tokea alipokuwa na miaka kumi na nane, kwa hiyo inawezekana ameshatongozwa zaidi ya mara 1000, kwa hiyo usifanye vitu ambavyo ameshavizoea kila siku na kuishia kutoa maamuzi ya kutokubali maombi yako kama wengine waliokataliwa waliotoa maombi yao hapo mwanzo kabla yako, kuwa mbunifu na tumia mazingira yako kwa usahihi na uzuri zaidi.
Hakikisha katika maongezi yako usiongelee wala kugusia vitu vifuatavyo,
  • Usimsifie sana, atakuona kama unambeza.
  • Usijaribu wala kumuuliza kama ana mtu, ana mshikaji wake au anamahusiano na mtu yeyote yule.
  • Usimuulize maswali magumu ambayo yanahitaji uelewa wa kitu fulani.
Vitu vifuatavyo ni ambavyo hutakiwi kuvifanya wakati wa utongozaji,
  • Usiongee kwa sauti ya juu sana,
  • Usijibu kitu au jambo kwa haraka sana,
  • Usiwe unaondoka ondoka au kuhamisha mapozi, usiwe na papara na kuwa mtulivu.
Kitu cha kuweka akilini zaidi usifikilie sana unachokiongelea, ukifikiria sana utakaribisha wasi wasi na kutokujiamini.
Wakati wa maongezi yako ya utongozaji, hakikisha unahusisha mambo yafuatayo,
  • Vitu ambavyo anashauku navyo na anavipendelea,
  • Vitu ambavyo unashauku navyo,
  • Hadithi zenye vichekesho na mguso wa mahaba,
  • Jifunze jinsi ya kuhadithia hadithi za kuvutia,
  • Mfanye acheke na kutabasamu kwa kile unachokiona,
  • Michezo ya furaha na ya kuvutia,
  • Unaweza kujikweza kidogo ila usipitilize.