Wao hawatumii simu kuwasiliana
Msingi mkubwa wa wanaume wa aina hii wanatunza siri kuhusu wao wenyewe na familia zao, kazi zao hata majina yao wakati mwingine
HAWATUMII SABABU YA KUWA KAZINI
Mara
nyingi mtu anaye cheat hutumia style moja ya kuwa kazi zinamfanya kuwa
busy kumbe anatumia muda na hawala yake, hivyo basi wadanganyifu wa
kiwango cha juu hawatumii sababu ya kuwa kazini kwani wanajua akianza
kushtukiwa jambo la kwanza ni kuangalia muda anaotumia kazini.
HUHAKIKISHA MKE ANA FURAHA MARA ZOTE
Kwa
kuwa atafanya kila njia kuhakikisha mwanamke anakuwa na furaha, hii ina
maana kwamba mwanamke mwenyewe atajisahau na kujiona kuna amani kumbe
ndani yake kuna udanganyifu mkubwa. Anaweza kukupa zawadi kila mara hasa
akisafiri, anafanya kila kitu kuonesha anakujali kumbe anakuzunguka na
inakuwa ngumu sana mwanamke kujua kwa sababu kila kitu anachohitaji
anapata.
HAWATUMII SIMU
Wanaume
wa aina hii si kawaida yao kuwapa mawahala namba za simu za mkononi,
nyumbani au kazini. Wanajua kupitia simu za mkononi text message tu
inaweza kuharibu mambo, acha kupigiwa simu kabisa. Pia wanajua wanawake
ni rahisi sana likitokea jambo lolote ambalo hajaridhika au
kukorofishana mara nyingi hupiga simu kwa wake wa hawa wanaume ili
kuvuruga zaidi. Ndiyo maana hawatumii simu.
WANALIPA CASH BILA RISITI
Kawaida
hawatumii credit card kulipia huduma zao kwani kuna bank huonesha
matumizi ya pesa yako kwenye bank statement (hasa nchi zilizoendelea).
Wanaogopa kwani kwenye account kunaweza kuonesha hotel na sehemu alienda
na jinsi alivyotumia pesa.
Pia hawataki risiti kwani anaweza kujisahau akiwa nyumbani risiti ikakutwa kwenye mfuko wa suruali au wallet.
WANABANA MATUMIZI
Kawaida
cheater mzuri hakopi pesa kwa ajili ya kustarehe na huyo mwanamke na
pia anahakikisha matumizi yana balance na kuwa kama kawaida, hawana
mambo ya ku-impress mwanamke kwa kutumia fedha nyingi hadi kukopa kwani
wanajua matatizo ya kifedha yakitokea lazima atiliwe mashaka na kushikwa
so mambo ya pesa wapo makini sana.
HAWADANGANYI OVYO
Hawana
tabia ya kudanganya sana na mara kwa mara, kwani wanajua ipo siku data
zitagoma bali wao huelezea uwongo unaofanana sana na ukweli ambao
anayeambiwa anadhani ni ukweli kumbe ndani kuna uwongo.
Pia hawezi kueleza kitu hadi aulizwe pia anakuwa na majibu mafupi yasiyo na maelezo mengi ili kuficha data zaidi.
HAWATUMII MARAFIKI
Kawaida
hawatumii marafiki au marafiki kuwasaidia kuficha siri zao. Wanajua
marafiki kwa kuchemka au kwa makusudi wanaweza kufikisha habari kwa
familia. Hujitunzia siri wao wenyewe na yeye tu ndo anajua kila kitu.
Hata mwanamke ataambiwa asimwambie mtu na akimwambia mtu urafiki unakufa
kwani anajua jinsi watu wengi wanavyojua issue basi uwezekano wa habari
kuzunguka ni mkubwa.
WANAENDA MBALI
Kawaida cheaters wa
aina hii si kawaida yao kutembea na majirani, marafiki, wasichana wa
kazi au wafanyakazi wenzao au mtu yeyote ambaye yupo connected na mke
wake, wao huenda mbali kabisa ambako hakuna mtu anawajua. Wanatumia ile
principle kwamba ukiona mwizi anaimba jirani ndo kukamatwa kumekaribia,
hivyo hawathubutu kuwa na wanawake wa karibu ambao jamii anaishi
wanamfahamu.
KUMBUKA
Kuwa mwaminifu katika ndoa yako ndiyo jambo la misingi na muhimu si maisha yako tu bali hata familia, ukoo wako na jamii nzima.
Kumbuka
kila mwizi ana siku yake ya arobaini hivyo basi hata kama hujagundulika
ni vizuri kuacha hiyo tabia mapema ili uanze kujenga familia bora na
yenye mafanikio pasipo wewe mwenyewe kuishi ndani ya guilt
No comments:
Post a Comment