
Inawezekana
wewe ukawa mmoja wao, sasa huna sababu ya kukata tamaa na kuona kuwa
huna thamani tena kwa mpenzi wako. Kwa kufuatilia vyema vipengele 10
vifuatavyo, nina imani utakuwa mpya na penzi lako litazidi kudumu zaidi
na zaidi.
1. MWANZO WA PENZI
Siku
zote nimekuwa nikisisitiza kuwa, jinsi unavyoanza ndivyo
utakavyomaliza! Kama ulianza vibaya uhusiano wako tegemea kumaliza
vibaya, lakini kama
Kama
unatarajia kuingia katika uhusiano na mpenzi mpya hakikisha hujionyeshi
tofauti na hali yako halisi ilivyo! Jifunze kujikubali, hata kama
unafanya kazi ambayo unadhani ni hadhi ya chini, mbainishe mpenzi wako
hali halisi ilivyo. Kama anakupenda, kazi yako haiwezi kupunguza mapenzi
baina yenu.
Ikiwa
ndiyo kwanza mnaanza uhusiano, zingatia hili, na kama mpo katika
uhsiano kwa muda mrefu ukagundua wazi kuwa kuna mahali ulikosea, anza
kufanya mabadiliko kuanzia sasa. Bado hujachelewa, mwambie ukweli naye
atakuheshimu kutokana na ukweli wako.
Kudanganya
hakuna mantiki, kudanganya ni utumwa, usikubali kuingia katika utumwa
au kifungo cha aina hiyo. Ukweli ni silaha ya kwanza katika mapenzi,
anza hivyo kuanzia mwanzo na kama ulikosea, ulijisahau au hukujua, basi
anza leo!
2. USIJICHUKIE
Itakuwa
kichekesho kama utasema unampenda mpenzi wako wakati wewe mwenyewe
hujipendi! Huwezi ukasema unamthamini mpenzi wako wakati thamani yako
mwenyewe huitambui.
Naamini
tunakwenda sawa, kama unashindwa hata kuoga na kubadilisha nguo safi
nani atakayekupenda? Huwezi kuwa wa kisasa kama huzingatii usafi, hakuna
atakayevutiwa na wewe kama wewe hutaki kujivutisha. Sio ajabu mpenzi
wako akakutosa kwa sababu tu huna muonekanano mzuri kwa rafiki zake.
Nani atakayekupenda wakati wewe mwenyewe huonyeshi kama unajitambua?
Jikubali,
jithamini! Kuwa msafi wakati wote, kauli zako ziwe safi siku zote
mpenzi wako atakuwa huru kuwa na wewe. Isifikie hatua mpenzi wako
akataka kutoka na wewe lakini akasita kwasababu hajui ukija utakuwa
umevaa nguo za namna gani. Upo hapo?
3. MWONEKANO WAKO
Mwonekano
wako unaweza kukuanisha jinsi ulivyo kwa wanaokutazama, wakati mwingine
inawezekana ukatafsirika tofauti na ulivyo kutokana na jinsi unavyovaa
na tabia zako zingine!
Lazima
uwe kijana wa kisasa, kwa kuzingatia hilo unapaswa kuwa makini kwa kila
kitu kinachoonekana kwa wanaokutazama. Jenga mazoea ya kutambua aina ya
nguo na mahali ulipo, usivae nguo za ufukweni ofisini au nguo za mtaani
ukavaa ofisini!
Wanaokuangalia
wanapata taswira ya jinsi usivyo makini au makini kutokana na mavazi
yako. Vaa nguo safi kila wakati, labda kama unafanya kazi ambayo
inakulazimu kuwa mchafu, ila baada ya hapo unapaswa kuwa msafi.
Ukizingatia hili utamfanya mpenzi wako afurahie kuwa na wewe siku zote.
Amini popote ulipo, jinsi ulivyo ndivyo anavyoonekana mpenzi wako.
No comments:
Post a Comment