Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Tuesday, February 28, 2017

KISA NA MKASA - USHAURI KWA WADADA

Nawasalimuni nyote ndugu zangu!!

Niwakati mwingine tena ningependa ku-share na nyie mkasa huu ulionipata!

Nilikua na boyfriend wangu ambaye wakati akiwa chuo mimi nilikua nafanya kazi, tumeishi pamoja sasa yapasa miaka 4 ikiendea na miezi 7, kwa kweli nilimpenda mwenzangu kutoka moyoni, shida yake ilikua yangu, huzuni yake ilikua yangu, familia yake ilikua yangu, katika kipindi chote tulicho kuwa pamoja sikuwahi kujuta hata siku moja, alikuwa ni. . ..
mwepesi kuomba msamaha anapokosea, nikasema jamani nimepata mume, baada ya kumaliza chuo, niliendelea kumsaidia kutafuta kazi pamoja na kutunza familia yake, mpaka siku alipopata appointment ya kuanza kazi sehemu fulani, nikamshukuru Mungu nikasema sasa tutasaidiana na mwenzangu.

Mpendwa huwezi amini, siku hiyo nikiwa katika harakati zangu za kulitumikia Taifa nikashangaa msg imeingia, kila nikiisoma sielewi, imeandikwa hivi, "IT IS MY HARDEST TIME SINCE MY HEART IS TROUBLED!! WHAT AM IN AND WHAT AM PASING THROUGH, IT IS VERY DIFFICULT SINCE IT IS IN THAT WAY, MY MOUTH FAIL WHAT 2SAY, MOYO UNANIUMA LAKINI LAZIMA NIKWAMBIE, NIMEPATA MSICHANA MWINGINE, I HAVE TO MARRY HER".

Sikuamini mboni za macho yangu, niliona kama lens ya miwani yangu imeharibika, nikavua miwani nikaifuta nikafikicha macho yangu, then nikarudia ile msg lakini haikuwa na mabadiliko, niliona kama ni mchezo wa kuigiza, niliona kama haiwezekani, siku yangu iliharibika, nikajirudia nyumbani mnyonge kama kinda la shomoro lililonyeshewa na mvua.

Mpendwa, huwezi kuamini baada ya siku mbili tu kupita, rafiki yangu mmoja aliniletea kadi ya harusi akiwa na tahamaki kubwa, akaniambia hivi umesikia fulani anataka kuoa? na kadi yake hii hapa nimepewa ya mchango, sikusema neno, nakumbuka ilikua cku ya jumanne, ilipofika jumapili baada ya ibada, binti mmoja akanifuata akaniuliza dada na wewe unakwenda kwenye kikao cha mtu fulani?? (akimtaja huyo aliyekuwa boyfriend wangu),baada ya hapo nikampigia simu mama mmoja rafiki yangu ambaye anahusika na mambo ya ndoa pale kanisani, nikamwambia kumbe mtu fulani anataka kuoa? akajibu akaniambia eeh anataka kuoa, nikamwambia kumbe alikua na mchumba, akanijibu ndio, mbona tangu mwaka juzi aliniletea mchumba wake akamtambulisha kwangu?? sikua na la nyongeza nikakata simu baada ya kuongea nae mambo mawili matatu hivi.

Wasichana wenzangu, nadhani mtakua mnajua hali ambayo napitia kwa sasa, kwa kua hata kama ww hukupitia hali hiyo, basi ndugu yako au rafiki yako alipitia hali ninayopitia kwa sasa!! nilirudi nyumbani nikalia sana, nikamuuliza Mungu kwanini umeacha jaribu hili linipate mimi, kwanini umeacha aibu hii inipate mimi, je kupenda ni dhambi? nililia niliponyamaza nikamwambia Mungu, sitaki kulia tena kwa sababu ya mwanaume, hakika nimetambua kuwa adui yako ni wa nyumbani mwako, ni kweli nimepoteza muda wangu mwingi, ni kweli nimekataa wanaume wengi walio taka kunioa, lakini jambo moja ninajua wewe ni MUNGU WA NYAKATI NA MAJIRA mimi nitasubiri tena!

Hili ndilo lililonipata mwaka huu, nilitaka niwashauri wasichana wenzangu mambo haya
1. usimwamini mwanaume wa aina yeyote, hata akuite majina gani mazuri.
2. Take a good care of yourself,
3. Love n dont count on anybody on that, at the end of the day it's u who live ua life! Live the life u want!
4. Usikubali relation ya muda mrefu hata siku moja
5. Yarudie rudie maneno haya moyoni mwako "Dear God, I want real love and to be loved unconditionally. Please forgive me of my sin and show me what is real love. I surrender my heart to you and ask that you take control of my life now. Thank you."

MAONGEZI YA KINAFIKI YA BAADHI YA WANAWAKE

*WAKIONGEA KWA SIMU*
Mary: Hello...! Sarah: Hello mpendwa, mambo yako jamani?
Mary: Niko poa shosti, nimeku-miss sana.
Sarah: Jamaniii.... na mimi pia wangu
Mary: Mhh na hapa nakupigia kukufahamisha kwamba baadae ntakuja kwako.
Sarah: Wooow, haina shaka mpendwa, dah nitafurahije jamani, nakutegemea basi mpendwa...! 
*MARA BAADA YA KUKATA SIMU*
Mary: Naenda kumtembelea tena yule malaya.
Sarah: Huyu mpumbavu anakuja tena, anadhani ntamnunulia vinywaji kwa hela zangu, labda sio mimi.
Wengi hupendana midomoni ila moyoni hakuna kitu kama hicho.

SIMULIZI : IMANI YAKO NDIO ITAKAYOKUPONZA

Salome alifunga ofisi yake na kwenda benki kuchukua fedha kwa ajili ya ada ya mwanae aliyekuwa akisafiri siku ya pili kwenda shuleni.

Mita chache baada ya kuchukua fedha akiwa anaelekea kupanda gari akakutana na mama mmoja aliyekuwa akiomba msaada wa fedha ya kula yeye na familia yake.

Kwa huruma ya kumwona mama mwenzie akitia huruma kuomba msaada wa chakula cha yeye na familia yake akafungua mkoba wake na kutoa noti ya shilingi elfu kumi na kumpa.

Alipofika nyumbani akashangaa kuona fedha zote kwenye mkoba zimetoweka na hakuwa na jinsi zaidi ya kulia kwa huzuni kwani hata alipofika ule mtaa alikomsaidia yule mama hakukua na dalili zozote za yule mama.

Suphiani yeye alitembelewa na baba mmoja dukani kwake na kumwomba msaada wa chenji ya shilingi elfu kumi.

Saa moja baada ya yule baba kuondoka suphiani hakuamini kuona droo yake ya fedha ikiwa tupu kwani hela zote zimetoweka.

Sara alibahatika kuwa dada mjasilia mali na alijiimarisha sana katika shughuli zake.

Akabahatika kukutana na rafiki mmoja wa kike walioshibana sana na kushauriana sana katika biashara.

Siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa sara yule rafiki alimpa zawadi ya mkufu mzuri sana ambao kamwe sara hakutamani kuutoa mwilini mwake kwa jinsi ulivyompendeza.

Siku hadi siku sara akashangaa kuona biashara yake ikizidi kushuka na kuporomoka kwa kasi kabla ya kwenda kanisani na kuombewa na kwa mshangao ule mkufu ukabadilika na kuwa kamba ya ajabu mfano wa hirizi.

Hirizi ile ikaongea kuwa alipewa sara na rafiki yake ili impotezee mafanikio yake na kumwacha maskini wa kutupwa atakaye hangaika maishani.

Ndugu kumbuka sio kila mtu unayemsaidia ana mpango mzuri kwako na sio kila zawadi unayopewa ina maana ya kukupa furaha.

Kila utakachokipokea kumbuka kukikabidhi mikoni mwa Mungu na kuomba ulinzi wake.

Sala yangu kwako

Kila msaada utakao utoa na uende kwa mhusika na Mungu akupe mara kumi ya kila utakachokitoa na kukubarikia furaha.

Kila zawadi utakayoipokea daima ikupe furaha na kukuongezea mafanikio na sio kukuibia mafanikio.

Comment AMEN na kisha share ujumbe huu kama nawe waamini ulinzi wa Mungu kwa kila unachokitoa na kukipokea.

PENZI HUFA...BESTFRIEND HUDUMU:

Watu huanza Mapenzi kwa Mbwembwe
sana...always..utaonyeshwa vitu mpaka utajiuliza
"Alikuwa wapi siku zote Malaika huyu wakati
nateseka na Mapenzi"..Muda unapokwenda Penzi
huanza kuchuja taratibu na unagundua huyu
"Malaika' nae ni walewale tu...Hii ni Law of
Diminishing Marginal Utility ,ipo tu kataa au kubali...Na hapo ndipo URAFIKI WA
KWELI huokoa jahazi
Wale ambao hupata mihemko ya kufunga Ndoa baada ya kukutana miezi 4 tu,kipindi bado Mihemko ya Penzi iko juu sana na kusahau kuna
LAW itaaply very soon ndo huangukiaga pua bila
kutegemea
ALWAYS GET MARRIED TO YOUR BESTFRIEND
-Huwezi kumdanganya Bestfriend wako
-Huwezi kumuumiza Bestfriend wako
-Huwezi kuona Bestfriend wako hana raha
-Huwezi kumkosesha Amani Bestfriend wako
-Huwezi kumuacha Bestfriend wako
-Huwezi kumsaliti Bestfriend wako
Wengi tunaoa WAPENZI WETU badala ya
BESTFRIENDS....So wrong...Wazungu wanasema
"Theres a thin line between Love and
Hate"...Watu wanaoana leo kwa
mbwembwe,miaka 3 unasikia Mme kamuua
Mkewe kwa Shoka...WHAT HAPPENED???Same
Love imegeuka kuwa Terrible Hatred!!
Ukioa/Kuolewa na BESTFRIEND WAKO ni raha
sana,unakuwa huru kuongea na kufanya lolote
mbele yake maana Bestfriend ni mtu
anayekuelewa zaidi kuliko hata babako mzazi
unayeweza kumuektia wewe ni mtoto mzuri
kumbe kitaani unakula wida
Huwezi kumjua Bestfriend kwa Miezi 3...Wazazi
wetu walikuwa na akili..Hawakukurupuka...Sisi
tunajifanya wazee wa ndoa za MKUKUTA na
FAST-TRACKING,Miezi 6 unaoa...Ndoa zote
unazoona Wanandoa wana miaka nenda rudi
wanapendana kama makinda ya Njiwa..Waulize
vizuri...utagundua wale sio WAPENZI TU....Ni
Bestfriends!!
Sahau PARAGRAPH yoote hii ila kumbuka hili
tu...MARRY YOUR BESTFRIEND.

SIFA 10 ZA MWENYE MAPENZI YA KWELI . .

Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.

*      Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .

*      Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatojali umeongea baya au zuri

*      Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha. Hatakuwa mtu wa kuvizia vizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.

*      Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatopenda kuwa kikwazo cha maisha yako, atakulinda daima.

*      Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani (pesa au mali)

*      Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine,hafichi hisia zake mbele za watu, atakutetea na kukufanya wa kwanza.

*      Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.

*      Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya maamuzi magumu .

*      Atakuwa tayari kuvumilia,hatak uwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu na ubabe.

VUNJA UKIMYA: SIMULIZI YA MAPENZI

 
1st year
Nikiwa nimekaa leacture room nikimuangalia msichana aliyekaribu yangu,niliyekuwa nikimuita "Bestfriend"nilikuwa nikimuangalia nywele zake nzuri na sura yake ya upole huku nikitamani awe wangu,lakini yeye hakuwa akitamani hilo na nilikuwa nikilitambua hilo.
Baada ya leacture,alikuja kwangu na kuniomba notes za siku ya nyuma kwa sababu hakuweza kuingia darasani hiyo siku iliyopita.baada ya kumpa akasema "asante" na kushikana mikono na mimi.I wanted to tell her,i want her to know that i don't want us to be just friends,i love her but i'm just to shy,and i don't know why
2nd year
Simu yangu iliita,kupokea alikuwa yeye alikuwa akilia akinielezea jinsi gani boyfriend wake broke her heart,she asked me to come over because she didn't want to be alone,kwa kuwa ni rafiki yangu kipenzi ilinibidi kwenda kumfariji,as i sat next to her on the sofa,nilikuwa nikimuangalia Machoni nikitamani awe wangu.Baada ya masaa mawili baada ya kuangalia nae movie mbili tatu na kula nae chakula pamoja akarudi katika hali yake ya kawaida,hivyo akaamua kwenda kulala,before akaniangalia na kuniambia "asante" na kunipa tabasamu tamu,i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.
3rd year
Siku moja kabla ya Tamasha la muziki chuoni alikuja kwenye meza yangu leacture room na kuniambia "Boyfriend wangu amepata udhuru hivyo naomba unipe campan katika tamasha la muziki leo usiku" kwa kuwa tuliwekeana promice kwamba ikitokea kila mmoja wetu amekosa mtu wa ku-date nae basi tutaenda pamoja just as "bestfriends".hivyo tukaenda.
katika tamasha baada ya kila kitu kuisha na muziki kufungwa,nilikuwa nimekaa nje ya ukumbi nikimuangalia jinsi alivyokuwa akicheka na rafiki zake,she saw me looking to her she smiled at me,i want her to be mine lakini yeye alikuwa hafikirii hilo kabisa na nilikuwa nikilitambua hilo,then she said to me "nimekuwa na muda mzuri na wewe asante sana" and she gave me a sweet smile.I want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.
Graduation Day
siku,wiki kisha mwezi ukapita ilikuwa ni mahafali yetu tukimaliza masomo ya chuo,akiinuka kwenda kutunukiwa shahada yake ya uchumi nilikuwa nikimuangalia akiwa amependeza sana siku ile,i wanted her to be mine,but she didn't notice me like that,and i knew it.
kabla watu hawajatawanyika kwenda makwao,alikuja kwangu akiwa na vazi lake la mahafali,na kulia pale nilipomkumbatia akainua kichwa chake na kuniambia "you are my bestfriend asante sana" i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.
Miaka michache baadae
Yule Msichana akiwa anaolewa sasa,nilimuangalia akisema "ndiyo nakubali " and drive off to new life,kaolewa na mwanaume mwingine,i wanted her to be mine,but she didn't see me like that,and i knew it.
but before she drove away,alikuja kwangu na kusema "asante sana" and kissed me on the cheek.I want to tell her to know that i dont us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why.
Kwenye Mazishi
Miaka ilipita i looked down katika jeneza lilokuwa na msichna ambaye alikuwa ni "bestfriend" wangu,Katika Service ya mazishi wakasoma diary ya Bestfriend ambayo alikuwa akiiandika enzi za maisha ya chuo'
Diary yake ilikuwa Ilikuwa ikisomeka hivi
I stare at him napenda awe wangu,but he doesn't notice me like that,and i know it,i want to tell him,i want him to know that i dont want us to be just friends,i love him but i'm just to shy,and i dont know why.I wish he would tell me he loved me!
Nilipiga magoti huku nikilia nikijisemea moyoni i wish ningemwambia tu ukweli,nimeshachelewa sipo nae tena katangulia mbele za haki i cried!!
Vunja ukimya
Be free when you love someone kuwa muwazi pia.
Share it up if it's touched your heart.

HADITHI YA MAPENZI : KUSADIKIKA

GIRL: Baby, hebu niambie harusi yetu itakuwaje?
BOY: Yaani hii haijawahi kushuhudiwa, ngoja
nikupe kionjo kidogo tu
GIRL: Enhee...
BOY: Kwanza siku ya kupeleka mahari nitaswaga zizi zima la ng'ombe napeleka kwa babu yako
GIRL: Ooh baby u care..
BOY: Siyo hivyo tu, baba yako ntamnunulia Range Rover Sport na mama mkwe ntampa Range Rover Evoque
GIRL: Baby u are awesome...
BOY: Halagu mdogo wako wa kiume ntampa Prado
Tx, na hapo nimesukutua tu mdomo sijaanza kula....
GIRL: Enhee...na sisi??
BOY: Sisi tutachukua mtaa mzima Oysterbay, kila wiki tutaishi nyumba tofauti
Halafu siku ya harusi yetu tutakodi zile meli zinabeba makontena ndiyo iwe ukumbi wetu, itatupeleka hadi Maldives
GIRL: Baby I love you
BOY: Tukitoka hapo tunaenda honeymoon Bahamas.... halafu tunaenda Taiwan shopping ya fenicha, kisha Japan shopping ya electronics, halafu tunaenda Dubai nikununulie vito vya thamani
GIRL: Ooh my sweetheart... halafu tukitoka huko??
BOY: Tukitoka huko nachukua ndoo ya maji nakumwagia uzinduke usingizini na ndoto yako imeishia hapo

CHOMBEZO - KIDUKU CHA MGUU MMOJA

“Mambo vipi kaka Eddy mzima wewe, samahani kaka sijui unakumbuka ulichoniahidi???…..najua haukumbuki lakini mimi nitakukumbusha ni kuhusu kunifundisha kucheza mziki” aliongea maneno hayo mwanadada Yasmin kupitia simu ya mkononi akimwambia Eddy, ambaye ndio kwanza alikuwa ametoka usingizini.
Eddy kwa hali ya kawaida alikuwa amesahau kabisa kuwa aliwahi kumuahidi mwanadada Yasmin kuwa atamfundisha kucheza mziki katika staili tofauti tofauti. Hiyo ilikuwa baada ya Yasmin kumwambia kuwa anatamani sana siku moja aweze kucheza mziki
“Aaah!!! Ok! Nimekumbuka sasa tufanye lini na wapi?? Samahani jamani” aliuliza Eddy huku akiomba radhi


“Mama amesafiri kaenda Pemba kumpeleka mdogo wangu kutembea kwa bibi yaani nimebaki peke yangu hapa nyumbani kwa hiyo sitaweza kutoka hapa labda uje wewe jamani samahani eeh!!” alijibu kwa sauti nyembamba ya kike mwanadada huyu.
Jibu hilo lilimtia Eddy nguvu sana na kumfungua akili yake. “Mama hayupo na baba hayupo kifuatacho???” alijisemea kimoyo moyo huku akiyakariri maneno ya Yasmin.
“Basi nitakuja, ulisema unataka staili gani vile nimesahau maana na wewe unapenda staili nyingi sana”
“Mdogo wangu ananicheka eti sijui kucheza kiduku na mimi nataka nijue halafu na kucheza mapanga yale ya TMK ya Wanaume Family….” Alijibu Yasmin huku sauti yake ikimuumbua kuwa alikuwa na aibu
“Ah!! Mapanga ya kizamani hayo nitakufundisha kiduku sawa dada….”
“Yaani nitafurahi kweli kikitoka huko Pemba nitakiringishia kweli” alijibu tena kwa furaha binti huyu kutoka familia bora sana aliyekuwa anaishi maeneo ya “masikini hajengi” ya Kidichi Spice mjini  Zanzibar.
“Kwa hiyo lini nije” aliuliza Eddy
“Siku yoyote saa yoyote unayotaka chamsingi mimi nijue kucheza kiduku, si nitajua upesi eeh!!….”
Baada ya maongezi marefu na kufikia muafaka wa lini waonane Eddy alikata simu na baada ya muda akaongezewa muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi elfu moja kutoka kwa Yasmin. Pale pale Eddy akajiunga huduma maarufu ya vijana wasiokuwa na pesa za kupiga simu yaani “Epic Nation ya Tsh 500/=” pale akawa ameunganishwa moja kwa moja na huduma ile ambapo alijinyakulia sms 300 na dakika 15 za Zantel kwenda Zantel, na kuanza kuchat na Yasmin.
Eddy: hivi Yasmin utaweza kucheza kiduku kweli
Yasmin: ntaweza kwani wanaoweza wana nini?? Kwani  ni kigumu sana eenh??
Eddy: Unajua staili ngapi za viduku?? Eddy akawa ameanza ualimu wake
Yasmin: Mi huwa nasikia kiduku kujiremba, kiduku mcharuko, kiduku cha kukuna nazi na cha kuendesha mtumbwi
Eddy: mh!! Hayo maviduku ya zamani kweli mimi nitakufundisha mpya kabisa hata watu hawaijui
Yasmin: Kinaitwaje hicho jamani yaani natamani hata ungekuja leo ili nijifunze upesi kabla dogo halijarudi.
Eddy: kinaitwa ‘kiduku cha mguu mmoja’ mdogo wako anakiweza hicho!!!
Yasmin:mh! Sijawahi kumsikia akisema hakiwezi hicho labda ndo maana hasemi, anavyopenda sifa angekuwa keshanambia
Eddy: sasa nitakuja leo jioni kukufundisha sawa?
Yasmin: usiache Eddy
Akili ya Eddy ilijizungusha haraka haraka na kuamini huu ulikuwa muda muafaka wa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na Yasmin kwa kutumia fursa hii ya kumfundisha kucheza kiduku.
Ni siku nyingi sana alikuwa anajaribu kumjengea mazingira ya kimapenzi lakini hata hisia za Yasmin hazikuonekana wazi kwake na yeye Eddy alishindwa kumtamkia.
Alikuwa domo zege!!!
Majira ya saa kumi na mbili jioni Eddy mtoto wa Mboriborini uswahilini alikuwa akipata juisi baridi ya embe katika sebule pana iliyopulizwa na kiyoyozi wakati wote, Yasmin alikuwa amevalia pensi iliyokuwa imembana na ilionekana dhahiri hakuwa na hakuwa na kitu chochote ndani.
Mate ya uchu yalimjaa mdomoni Eddy na kwa jicho la wizi wizi aliweza kuchungulia cheni iliyong’ara kutokea kiunoni mwa Yasmin. Maungo yake yakamsisimka!!!
“Yasmin usiku unaingia, nenda ukavae nguo za kuchezea Kiduku cha mguu mmoja” Eddy alimwambia.
“Ndio zikoje hizo mwalimu wangu unadhani mimi nazijua basi…..” alijibu Yasmin huku akimkata jicho la mahaba Eddy. Eddy nae  akakwepesha macho!!!
“Kavae kanga na kitop nadhani hapo itakuwa sawa” alijibu huku akiona haya kidogo kwa jambo alilotamka.
“Haya Mwalimu wangu…..” alijibu huku akiondoka
“pia usisahau kuweka hii Cd wimbo namba tatu…” alisisitiza Eddy.
Baada ya dakika kumi Yasmin alirejea, kama Eddy alivyoagiza Yasmin alikuwa amevaa kanga moja pekee na kitop kilichoachia kitovu chake nje kidogo.
Kwa mwendo wa kunyata aliisogelea redio na kuweka ile Cd kisha akachagua wimbo namba tatu, ulikuwa wimbo wa taarabu uitwao ‘mama nipe radhi’. Eddy aliangalia kwa wiziwizi upande wa nyuma wa Yasmin akatamani kumrukia, kwa kitendo cha haraka haraka bila Yasmin kugundua Eddy alitumbukiza mkono wake katika suruali yake akaweka mambo sawa asije kuaibika!!
Eddy akamsogelea Yasmin pale alipokuwa na kuizungusha mikono yake katika kifua cha Yasmin.
“Sasa inatubidi tuanzie kiduku cha kawaida halafu cha mcharuko kisha tutamalizia kiduku cha mguu mmoja. Yasmin hakuwa na pingamizi lolote alikubali kila kitu alikuwa na hamu kubwa ya kujua kucheza kiduku!!!, mikono ya Eddy ilivyogusa kifua cha vuguvugu cha Yasmin alihisi kuishiwa pumzi zake, alijaribu kufundisha lakini somo lilikuwa haliendi, kwa ujasiri mkubwa alipandisha mikono yake katika chuchu ndogo za Yasmin na ni wakati huo huo ulikuwa umemalizika wimbo wa Mama nipe radhi na kuingia wimbo wa marehemu Nasma Khamis Kidogo uitwao
‘SABALKHERI’ (wale wapenzi wa muziki wanautambua wimbo huu wa chombezo) Katika taarabu za asili ni wimbo huo uliomkosha sana Eddy na alikuwa amekariri mashairi yaliyokuwa yakiimbwa na mwanaume hivyo alishindwa kujizuia kuigiza sauti ile na bila kutegemea alishangaa mashairi ya Nasma Khamis Kidogo yakijibiwa kiustadi kabisa na Yasmin ambae wakati huo pumzi zake zilipishana kwa kasi tofauti na mwanzo
Eddy: Sabalkheri mpenzi waonaje hali yako
Yasmin: albanur azizi hali yangu kama yako
Eddy: wawaonaje wazazi nyumbani utokeapo
Yasmin: kawanusuru mwenyezi hali hofu yao juu yako,hebu nitoe majonzi unijuze shida yako.
Eddy:Shida yangu sijiwezi,dawa yangu sura yako.
 Mwingine we achomozi nakupenda peke yako
Yasmin:Daima nitakuenzi silitupi pendo lako
Yasmin: usiingie simanzi sura yangu mali yako
Eddy: nakuikosa siwezi sikia langu tamko
Yasmin: mwingine we hachomozi nakupenda peke yako
Eddy: nimefanya uchunguzi nakiri maneno yako, Naiona waziwazi ishara ya pendo lako.
Yasmin: milele nitakuenzi natoa ahadi kwako………
Eddy: kibaya sikivumbuwi ndani ya maungo yako
Yasmin: na mimi simtambui mwenye sifa kama zako……………..wallah sijitambui mgonjwa kwa raha zako
Waliendelea kujibishana maneno yale kwa sauti za chini wakati huo kanga ikiwa tayari imeanguka chini na Eddy akihesabu idadi ya cheni alizokuwa amevaa mwanadada Yasmin zilikuwa nne na shanga tatu!!!!, mwanga wa taa nyekundu pale ndani uliwapa hamasa zaidi hadi wakajikuta wote wapo uchi wa mnyama pale pale sakafuni wakati huo ukilindima wimbo wa mwanamziki  aliyejizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania Ommy Dimpoz uitwao “Baadae” tayari Eddy alikuwa juu ya kifua cha Yasmin na kilichokuwa kinaendelea pale ni “KIDUKU CHA MGUU MMOJA”, wakati miguu miwili ikiwa imetulia tuli mguu mmoja uliosalia ulikuwa bize ukicheza kiduku.
“Kumbe unakiweza kiduku dah!!!” Eddy alimsifu Yasmin aliyekuwa anaona haya wakati akivaa nguo zake
“Kumbe hicho ndo kiduku cha mguu mmoja?????” alihoji Yasmin, Eddy hakumjibu bali aliachia tabasamu tu!!!!!

Kiduku cha mguu mmoja kikawa kimechezwa katika mazingira ya ajabu.

Swali likabaki kwa Yasmin je atajisifia kwa mdogo wake kuwa anaweza kucheza Kiduku cha MGUU MMOJA????.

MAMBO 20 YA KUFANYA UHUSIANO WENU UBAKI KWENYE FURAHA SIKU ZOTE

1. FANYA UCHAGUZI SAHIHI

Hapa ndipo watu wanapotakiwa kutumia akili zao mpaka zile za akiba, ukikosea hapa ni rahisi sana kuvurunda hapo baadaye. Uhusiano wenye nguvu, hujengwa na penzi la kweli. Acha kukurupuka, lazima ujihakikishie kwamba uliyenaye ni chaguo kutoka ndani ya moyo wako.
Najua una maswali; kwamba utawezaje kumjua mwenye mapenzi ya kweli, hiyo ni mada ambayo nimeshaandika mara kadhaa katika ukurasa huu na gazeti damu na hili, Ijumaa. Kimsingi, kwa kufuata maelekezo hayo, mwenzi ambaye unatarajia kuwa naye katika maisha ya ndoa hapo baadaye, lazima msingi uwe ni uchaguzi sahihi.
Sikia, watu wengi waliokuwa na fedha, wamefilisika baada ya kuoa/kuoleawa na wenzi ambao si sahihi. Aidha, wapo wenye mafanikio makubwa sana, ambayo wameyapata baada ya kuoa/kuolewa na wenzi sahihi. Rafiki zangu, si jambo rahisi kumpata yule aliye sahihi. Inahitaji utulivu.
Yapo mengi sana ambayo unapaswa kuyaangalia, ambayo nimekwishaeleza sana katika makala zangu zilizopita. Wakati nahitimisha kipengele hiki, shika neno moja tu; unapomchagua mwenzi wa maisha yako, hakikisha ni yule aliye sahihi! Tuendelee na kipengele kingine.
 
2. JIELEZE
Migogoro mingi baina ya walio kwenye uhusiano husababishwa na wenzi kutowafahamu vyema wenzao. Usiingie katika mkumbo huu, ni suala la kujieleza tu. Kumweleza mpenzi wako ulivyo, kutamfanya ajue vitu unavyopenda na usivyopenda. Aidha, kama unao udhaifu wowote wa kiafya na kadhalika, mweleze mwenzako.
Kumweleza kutamfanya ajiamini kuwa anapendwa. Kunaonesha unavyojiamini na unayetaka mwenzako ashirikiane na wewe katika hali uliyonayo. Si vibaya mwenzio kukufahamu kwamba una hasira sana. Yes! Maana akishajua hilo, ataacha utani unaokaribia kukuudhi maana anajua vizuri kuwa una hasira za karibu.
Ipo mifano mingi sana, lakini kikubwa cha kushika katika kipengele hiki ni kuwa mkweli kwa mwenzako kuhusu maisha yako. Acha kumdanganya kwamba familia yenu ina uwezo mkubwa, wakati ni wa kawaida. Kuwa mkweli, mapenzi si utajiri, ni hazina iliyojificha ndani ya moyo.
Kama anakupenda, anakupenda tu! Siku akigundua kwamba unamdanganya, pendo lake litapungua kwa kiasi kikubwa sana. Jieleze kwa uwazi na ukweli kutoka ndani ya moyo wako. Naye atakuheshimu na utakuwa umetengeneza mwanzo mzuri wa kuelekea kwenye ndoa isiyo na migogoro.
3. MPE UHURU
Wengi wanaamini kumbana mpenzi ni njia sahihi ya kumfanya awe mwaminifu, si kweli. Kuna wenye tabia ya kuvizia simu za wenzao na kuzipekua, si utaratibu mzuri. Mpe uhuru, usimbane! Kuonesha kumwamini sana mpenzi wako, kunamfanya naye aishi ndani ya uaminifu.
Kumchunga hakumnyimi kuendelea na mambo yake, sana sana atafanya kwa siri kubwa. Kumpa uhuru, kutamwogopesha, atajua yupo na mwaminifu ndiyo maana hafuatiliwi, hapo utakuwa umechochea naye awe mwaminifu kama wewe.
 
4. ACHA PAPARA
Katika hatua za mwanzo kabisa za uhusiano wenu, hutakiwi kuwa na papara katika jambo lolote. Kila kitu kifanywe kwa utaratibu. Huna sababu ya kurukia mambo, hasa makubwa.
Wengi wamekuwa na haraka sana ya kukutana kimwili, haya ni makosa makubwa sana. Haraka ya nini kama unatarajia awe wako wa maisha. Ngoja nikuambie rafiki yangu, unapoanza kuulizia mapema mambo ya faragha, unamfanya mwenzako ashindwe kukuamini.
Kwanza, atahisi wewe upo kwa ajili ya kutaka kujistarehesha tu, lakini pia anaweza kufikiria kwamba unapenda sana mambo ya chumbani. Kumfanya agundue kasoro hiyo ni tatizo kubwa sana kwako.
Hata hapo baadaye mtakapoingia kwenye ndoa, ni rahisi zaidi kukumbuka mambo ya zamani, kwamba yupo na mtu anayependa sana mambo ya mahaba. Kwa maneno mengine, hata akihisi tu au kusikia kwamba una mtu mwingine pembeni, atapeleka moja kwa moja hisia zake kwenye kuamini moja kwa moja juu ya jambo hilo.
Papara si jambo jema kabisa kwa mwenzi ambaye unatarajia awe wako wa maisha. Tulia, mchunguze kwanza. Kumbuka unatakiwa kufikiria kuhusu mustakabali wa maisha yako ya baadaye, kama ndivyo, huna haja ya kuharakisha mambo ya mapenzi.
5. JENGA URAFIKI
Ukitaka kutengeneza uhusiano wenye nguvu, basi zingatia zaidi urafiki. Kumfanya mwezi wako rafiki ni silaha kubwa na yenye nguvu katika kuuimarisha uhusiano.
Mwenzi wako anapojiona kama rafiki, anakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumza chochote, ikiwemo matatizo na migongano mbalimbali kama rafiki zaidi.
Hawezi kukuficha siri zake. Atakuwa na wewe muda wote na atakusogeza karibu yake kwa kila kitu. Hata penzi lenu pia litakuwa na nguvu zaidi. Urafiki ni kila kitu ndugu zangu.
Acha tabia ya kumkaripia mpenzi wako, jenga mazoea ya kujadiliana zaidi kuliko kutumia kauli za ukali. Rafiki zangu, yote hayo niliyoyazungumza yanajengwa na jambo moja tu; urafiki!
 

6. MSIFIE
Wengine wanaweza kushangazwa na kauli hiyo, lakini nataka kuwaambia kuwa kati ya mambo muhimu kabisa kumfanyia mpenzi wako na kulifanya penzi kuwa jipya ni kumsifia. Unapomwambia mwenzako kauli nzuri za kumbembeleza kuwa yeye ni mzuri, anakuvutia kwa kila hali, unajenga penzi.
Unamfanya anajihisi wa thamani, atajiamini kuwa yeye ni mkamilifu, si kwa watu wanaomzunguka pekee, bali hata wewe ambaye umemchagua na kumfanya awe wako.
Kama huna utamaduni wa kumsifia mpenzi wako, huu ni wakati wako wa kufanya hivyo kwa lengo la kuzidisha mapenzi na kuyapa nguvu.
 
7. SAIDIA KUKUZA UHUSIANO WENU
Kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha penzi linazidi kukua siku hadi siku. Kwa maana hiyo, wewe kwa nafasi yako unatakiwa kuhakikisha unakuwa mstari wa mbele kukuza uhusiano wenu.
Kuna mambo mengi sana ambayo yakifanyika, yanakuza uhusiano. Vipo vitu vya kufanya, kutoka pamoja ni njia mojawapo ya kukuza uhusiano. Rafiki zangu, mnapokwenda katika matembezi, husaidia kubadilisha mapenzi na kuonekana mapya.
Si lazima kwenda nje ya mji, kikubwa ni kuzingatia mfuko wako. Hata mkienda mahali pa kawaida tu, mkanywa juice na keki, bado ni nafasi nzuri kwenu ya kukuza uhusiano huo.
Kila mmoja ana wajibu wa kufanya hivyo, lakini hutakiwi kumsubiri mwenzako afanye, wewe kwa nafasi yako unatakiwa kuhakikisha unamfanya mwenzi wako afurahie uhusiano wenu. Kufanya hivyo, kutampa deni na yeye la kufanya hivyo kwako.

8. MFANYE NAMBA MOJA
Kuna baadhi ya marafiki wana fikra potofu (hasa wanaume). Hawa wanaamini kumpa mwanamke nafasi katika maisha ni kumfanya akukalie. Si kweli. Mwanamke unapompa nafasi ya kwanza, anaufurahia uhusiano wenu.
Anajiona mwenye hadhi kubwa zaidi kwako, hutafuta njia za kukufanya umpende maradufu, kuliko kumuacha akijiona hana nafasi.
Ongozana na mpenzi wako kwenye kumbi za burudani, mialiko ya sherehe mbalimbali, lakini pia mpe kipaumbele kwa kila kitu. Hili halihitaji elimu ya darasani. Chunguza wenzako wanaowapa wenzi wao kipaumbele wanavyoishi.
Achana na mifumo ya kizamani, ukimpa mwenzako usawa anajiona ana nafasi kwako na thamani katika uhusiano mlionao.
 
9. MPE NAFASI
Hapa hakuna kitu kikubwa sana, ni kiasi cha kumpa nafasi katika mambo yako muhimu. Mathalan unataka kununua kiwanja Gongo la Mboto; Hata kama umeshaweka kila kitu sawa, lakini kumshirikisha tu, kutamfanya ajione mwenye nafasi kubwa kwako.
Hili si kwa wanaume pekee, hata wanawake nao wanapaswa kutoa vipaumbele kwa wanaume zao. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuongeza ladha ya mapenzi kwa wapendanao.
Inawezekana elimu hii imekupitia kushoto, hebu jaribu uone mafanikio yake.
Kumpa nafasi mwenzako katika mambo yako, tafsiri yake ni kumuamini na kumfanya azidi kujiamini kwako. Ni rahisi sana, lakini habari njema kwako ni kwamba, atakusikiliza kwa kila kitu, maana anajiona yeye ni sehemu yako kikamilifu.
 
10. MTAMBULISHE
Mapenzi ya siri yana ukomo wake marafiki zangu. Ngoja niwaambie, unapokuwa unapenda mapenzi ya siri sana, unampa wakati mgumu mwenzako.
Ni rahisi kufikiria kwamba, unafanya hivyo kwa kuwa ama hujiamini au una mtu mwingine. Weka mambo hadharani. Mtambulishe mwenzi wako kwa marafiki zako.
Jiamini, unapokutana na mtu uliyesoma naye zamani au kuishi naye sehemu moja, mwambie kwamba uliyenaye ni mwenzako na unatarajia kuingia naye kwenye ndoa.
Kufichaficha kunaondoa utamu wa mapenzi. Kunazidisha maswali ambayo hayana majibu. Kama yapo ni huyo mwenzako kujijibu mwenyewe. Kwa kawaida, hatajipa majibu mazuri.
Yatakuwa ya kinyume – yenye tafsiri mbaya. Kwamba yawezekana hutaki kumtambulisha kwa kuwa una mtu mwingine. Je, ni kweli? Kama ndivyo huna sababu ya kumpotezea muda mwenzako. Kama si kweli, basi amka. Gundua kwamba ulikuwa unafanya makosa na uanze ukurasa mpya.
 
11. GUSIA MAMBO YA KIIMANI
Kuzungumzia mambo ya dini kulingana na imani yenu, kutamsogeza mwenzako kwenye ukweli kuwa una lengo naye la kuungana katika maisha ya ndoa. Angalizo kwako ni kwamba, wakati unamweleza hayo, iwe kweli yanatoka ndani ya moyo wako. 

 12. WAHUSISHE VIONGOZI WA DINI
Ikiwa uhusiano wenu umekomaa, unatakiwa kuwashirikisha viongozi wa dini. Angalia mazingira, unaweza kwenda naye, au kwenda mwenyewe na kuwaeleza nia yako. Waambie wakuombee au wawaombee ili uhusiano wenu uwe na nguvu.
Kumbuka ndoa ni tendo la heri, hivyo shetani naye hutumia nafasi hiyo kuwaharibia! Kumuingiza Mungu katika uhusiano wenu kuna maana, mtakuwa katika ulinzi wenye nguvu zaidi.
Yamkini pia, kama uliyenaye si chaguo kutoka kwa Muumba atamuengua mikononi mwako na kukupeleka palipo sahihi. Usiogope, nenda kaonane na viongozi wa dini na uwaeleze kinagaubaga.
 
13. KAMILISHA TARATIBU ZA KIFAMILIA/KIMILA
Ikiwa una uhakika kuwa mwenzako ndiye uliyemkusudia (zaidi kwa wanaume) wajulishe wazazi wako, kisha anza taratibu za kimila na kifamilia. Tuma wazee wapeleke posa, lipa mahari, halafu sasa anza kutimiza maagizo mengine yote utakayoagizwa.
Ni njia ya kuelekea kwenye ndoa. Uhusiano wenye baraka za wazazi, si tu kwamba unakuwa na nguvu, bali una radhi za wazazi wenu wa pande zote mbili. Je, kwa hali hiyo uhusiano wenu hautaimarika? Bila shaka utazidi kuchanua.

14. JADILINI KUHUSU NDOA
Hii ni hatua ya muhimu kabisa katika kuelekea kwenye ndoa. Mnapaswa kuijadili ndoa yenu ni ya namna gani? Kama imani zenu zimetofautiana, nini kifanyike? Pindi mtakapojadiliana, mtaweza kupata muafaka juu ya ndoa ambayo ni sahihi kwenu.
Ndugu yangu, usilazimishe kumbadilisha mwenzako akufuate katika imani yako kama yeye hataki au pengine kuna vipingamizi katika familia yao. Kila mmoja wenu anapaswa kuweka hoja mezani na mnazijadili kwa mapana yake na mwisho muafaka utapatikana, mtaoana.
Hakuna kinachoshindikana katika majadiliano, tumia lugha nzuri kumshauri mwenzako ili ajue unamjali hivyo ni rahisi kuridhia ulichomshauri. Ieleweke tu ndoa yoyote mtakayokubaliana kupitia majadiliano yenu, basi itadumu kuliko mkitumia njia ya kulazimishana.
(b) Kwa wanandoa hapa sasa mnisome kwa makini maana wengi wamekuwa wakifeli katika hatua hii kutokana na kujisahau. Mikikimikiki ya maisha inapoibuka inaweza kuwafanya kila mmoja wenu akawa na maamuzi yake katika maisha hata kama mwanzoni (kabla ya ndoa) dhamira yenu ilikuwa njema.
Siku ya leo, Lets Talk About Love itakumegea vipengele sita ambavyo kimsingi ukivisoma kwa makini itakuwa ni dozi sahihi kama mwanandoa kuweza kujua siri hizi muhimu za kufurahia mapenzi yenu na nikushauri kuitumia kila siku.
15. WEKENI MIPANGO PAMOJA
Wanandoa wengi wamekuwa wakijisahau pindi wanapokuwa ndani ya ndoa. Inawezekana awali walikuwa na mikakati mizuri lakini baadaye mmoja wao huanza kujiamulia bila kumshirikisha mwenzake. Tatizo hili lipo zaidi kwa wanaume, mfumo dume unachukua mkondo wake. Utakuta mwanaume anafanya maamuzi peke yake akiamini yeye ndiyo kila kitu.
Jeuri hii inakuja hasa pale mwanaume anapoamini kuwa yeye ndiyo chanzo cha fedha wanayotaka kufanyia kitu fulani. Ataamua bila kumshirikisha mkewe kwa kuwa fedha anakuwa nazo yeye bila kujua mipango yote inapaswa kuzungumzwa pamoja kabla ya kufanya maamuzi.
Ndoa ni makubaliano baina ya watu wawili hivyo basi, katika kila jambo la maendeleo litafanikiwa pale tu mtakapolipanga pamoja. Ndugu yangu, acha kujiona wewe ni zaidi katika ndoa kutokana na kipato ulichonacho. Fedha si lolote si chochote katika maisha ya ndoa. Fedha zisibadilishe maamuzi ya mipango yenu, kila mnachotaka kukifanya basi mkifanye pamoja.
16. TUMIA MAJADILIANO ZAIDI
Yamkini wote wawili mlifanya majadiliano kabla ya kufikia maamuzi ya ndoa, basi ni wajibu wenu kuishi katika majadiliano kila siku. Wapo watu wasiopenda kuona ndoa za watu zinakuwa na furaha. Wataingilia na kuwafanya mgombane. Inawezekana pia mkapishana kauli katika mazungumzo, busara huhitajika.
Kutofautiana kwa kauli pamoja na vitu vingine, vinaweza kumalizwa kwa njia ya majadiliano. Jadilini katika lugha nzuri itakayomfanya mwenzio aone thamani yake.
Mkijadili yote kwa uyakinifu, mwisho mtagundua kumbe kilichokuwa kinawatatiza ni kitu kidogo ambacho hakikuhitaji nguvu kubwa kukitatua. Mnapojadiliana ni rahisi pia kutambua kosa lilikuwa wapi au lilisababishwa na nani, hivyo ni rahisi kumuepuka. 

  17. PALIZI YA NDOA
Kama ilivyo kwa mazao yakiwa shambani yanavyohitaji kupaliliwa ili yaweze kushamiri, vivyo hivyo katika ndoa. Ndoa inapaswa kupaliliwa kila siku. Jaribu kila wakati kusoma alama za nyakati, vitu gani anavipenda mwenzako basi umfanyie kila wakati.
Mfano unaweza kupanga siku moja katika wiki ukamchukua mkeo au mumeo na kumtoa nje kimatembezi. Ndoa hupaliliwa na vitu kama hivyo. Zawadi za hapa na pale zisipungue, acha kuishi kwa mazoea eti kwa kuwa tayari ni mkeo au tayari ni mumeo.
Unapoipalilia ndoa katika staili za zawadi, mitoko na vitu vingine huifanya ionekane mpya kila siku. Mnunulie mkeo au mumeo vazi unaloona linaendana na wakati mlionao.

18. KINYWA CHENYE LADHA
Inawezekana ukaona labda nazungumzia kitu cha kawaida sana, lakini kama ukitafakari kwa kina na kwa mapana yake, utagundua kwamba ni mjadala wenye maana katika ndoa.
Hata kwenye Kitchen Party, sherehe za ndoa n.k, suala la kinywa chenye ladha nzuri huzungumzwa sana, ila hapa nitakuongezea baadhi ya vitu vingine usivyovijua.
Kwa kawaida, wanawake ndiyo ambao huaswa zaidi katika kuwa na kauli nzuri kwa waume zao. Wanaume wamesahaulika kabisa. Wanaonekana kama wao hawana wajibu wa kuwa na kauli nzuri kwa wake zao; jambo hili si la kweli hata kidogo.
Wote wanapaswa kuweka masikilizano kwa kauli ya pamoja, huku kila mmoja akiwa na shabaha ya kuhakikisha mwenzake haudhiki na maneno yake. Ni jambo jepesi sana – kuwa na ulimi wenye ladha.
KUJITAMBUA kwamba unayezungumza naye ni mke/mumeo. Hebu jiulize, ikiwa mwanzoni wakati wa uchumba wenu mliweza kuwa na kauli nzuri, kila mmoja akiwa na hamu ya kumsikiliza mwenzake muda wote, iweje katika ndoa?
Jibu la swali hili litakuwa mwongozo mzuri zaidi wa kuinakshi ndoa yenu kuwa bora yenye furaha siku zote. Ndugu zangu, furaha ndiyo kila kitu katika uhusiano wowote ule. Kukiwa na furaha, hakuwezi kuingia tatizo lolote. Litapitia wapi, wakati mioyo ina amani?
Ikiwa kinyume chake, ni rahisi hata kugombana, maana hata mgombanishi hupata nafasi zaidi sehemu isiyo na amani, isiyo na majadiliano, pasipo na maelewano. Usikubali kuwa katika ndoa ya namna hiyo.
 
19. EPUKA MANENO YA KUUDHI
Kipengele hiki hakina tofauti sana na kilichopita, lakini hapa kuna la zaidi la kuongezea. Kuna wakati wenzi wanaweza kuingia katika mtafaruku ambao chanzo chake ni cha ajabu kabisa! Kwa mfano, unakuta mpenzi anamwambia mwenzake: “Mh! Na wewe unanuka sana mdomo!”
Kauli gani hiyo kwa mpenzi wako? Mwanaume unalala naye kila siku, kwa nini umwambie ananuka? Wewe ukifanya hivyo, huko nje wamuambieje? Kwanza kama ni kweli ana tatizo hilo, ni jukumu lako kumtibu, lakini pia kumtunzia siri.
Kama nje anachekwa, ndani ya familia pia anachekwa, wapi atapata faraja? Yapo maneno mengi sana yenye kuudhi, lakini hapa nitataja machache. Wengine wanawaambia wenzao wananuka kikwapa, hawajapendeza, hawana akili nk.
Haya ni maneno ya kuudhi. Hebu fikiria kauli kama hii mtu anamtamkia mkewe! “Yaani kweli wewe huna akili, kitu kidogo kama hicho kweli unaweza kukosea? Ndiyo maana wenzetu wanafanikiwa kimaisha, wanatuacha. Sijui nilikutana na wewe wapi?...maisha yangu yanazidi kuwa giza tu, nikiwa na wewe!”
Acha maneno ya kufuru, kwani siku zote hukuona upungufu wake? Kuwa makini na kauli zako. Ndoa yako utaivunja wewe mwenyewe, pia kama ni kuijenga, utaijenga wewe mwenyewe!
 
20. UBORA KATIKA TENDO LA NDOA
Hapa ndipo panapotakiwa kupewa heshima kubwa zaidi kuliko vipengele vyote vilivyotangulia. Katika masomo yaliyopita, nimewahi kufafanua hili kwa undani zaidi, leo nitagusia juu juu tu!
Rafiki zangu, tendo la ndoa ni la heshima. Halitaki papara na linatakiwa kupewa nafasi na kila mmoja kuridhika. Acha kujifikiria mwenyewe, maana hapa ndipo panapopatikana mianya ya kutoka nje ya ndoa.
Hakikisha mwenzako anaridhishwa na wewe mnapokuwa chumbani. Tafuta elimu zaidi ya kufurahia tendo hilo ili mwenzako awe na sababu ya kuwa na wewe. Sikia nikuambie, tendo la ndoa kwa wanandoa hasa waliozoeana linachosha!
Huu ni ukweli ambao wengi wanaupinga. Yes! Linachosha na kukikanaisha. Hakuna kipya. Mwanaume yule yule. Kitanda kile kile, chumba kile kile. Lazima umchoke.
Hata hivyo, ukiwa mbunifu utaendelea kumuona mwenzako mpya kila siku. Badilisheni mazingira, tafuteni muda wa kutoka pamoja angalau mara moja ndani ya miezi mitatu – kwa mwaka mara nne.
Yapo mengi sana, elimu hii ni pana, hasa kama utakuwa mbunifu na mwenye kuisaka kila siku. Rafiki zangu, nadhani mnafahamu namna inavyokuwa vigumu kueleza kila kitu hapa gazetini, lakini kikubwa cha kumalizia mada hii ni hiki; unapokuwa na mwenzako faragha, ujue kuwa anategemea zaidi wewe kumfanya afurahie tendo hilo.
Ukijua hivyo, naye akajua hivyo, furaha ya tendo la ndoa itadumu siku zote za ndoa yenu.

AKILI ZA USIKU: SIMULIZI YA MAPENZI

Kuna siku nilikuwa maeneo ya Mjini kati (City Center), nikaipenda suruali moja ya shilingi 15,000/= na pesa sikuwa nayo ikabidi niende kutoa kwenye ATM ya Postal.
Nimefika pale sikukuta mtu hivyo niliingia moja kwa moja, nimefika mle ndani nikakuta Pesa Kibao zimemwagika pale kwenye kitundu cha kutolea pesa, ATM Card ilikuwepo pale imetokezea na Pembeni kulikuwa na Pochi ya Kike iliyoonekana kutuna vilivyo.

Kwa woga mimi huku nikitetemeka mapigo ya moyo yakiwa yameongezeka nikatizama nyuma yangu sikuona mtu, nikachukua zile Pesa harakaharaka, ATM na ile pochi.

Ile natoka nje kuna dada mmoja alikuwa anakuja kwa kasi maeneo yale nikapata uoga nikamuuliza “Samahani dada, kuna kitu umesahau humu”, yule dada hakunijibu kitu kaingia kwenye chumba cha ATM akachomeka Kadi kutoa hela mi nikaondoka zangu fasta kuelekea home.

Nimefika home nikajifungia ndani na kuzibwaga zile pesa kitandani, nikafungua wallet nikakuta imejaa dollar, Vipodozi, iphone na ki-Nokia kidogo cha tochi, ATM Card mbili za Benki tofauti ambazo zilikuwa zimezungushiwa karatasi iliyokuwa na namba za siri za ATM zote, moyo ukanilipuka paaaa!!! Nikaona bora Nipumzike kwanza kitandani!!
Muda si mrefu ile iphone ikaanza kuita, nilipoangalia halikutokea jina nikaona bora nipokee nimsikilize anasemaje, ilikuwa sauti ya kike iliyoongea kwa huzuni kwa kubembeleza huku akilia na alijitambulisha vizuri kuwa ile mali ni ya kwake! Huruma ilinijia nikamwelekeza nilipo aje kuchukua...

Hakuchukua muda akawa amefika nami nikamkabidhi vitu vyote naye akavihakiki na kukuta viko sana: Milioni 3 za Kibongo na Dollar 500. Dada kanishukuru na kunipa ile Millioni 3 ya kibongo mi nikazikataa kwasababu ni mali yake na alizisahau tu.

Alinitoa hofu kwa kunisihi nichukue tu, mi kama binadamu mwenyezi Mungu atanilipa, nikakataa... Mwishowe akaomba namba yangu na kuondoka zake, akawa ameniacha ndani huku njaa sasa nikaanza kuisikia, nilikuwa na buku mbili nikaenda kula viepe kavu na soda nikawa powa.

Sasa jana kanipigia simu kuwa anakuja nimsubiri, dakika tano tu akanipigia tena kuwa ameshafika yupo nje yupo ndani ya Prado mpyaa nikaingia tukaondoka akaenda kunionyesha kwake kisha tukaelekea kwenye nyumba nyingine iliyokuwa ndo imekamilika kujengwa akaniambia hii itakuwa yako akanikabidhi baadhi ya nyaraka na funguo zote sikuamini...!!

Akanisindikiza kwangu, kufika home ananiambia hiyo gari (Prado) nayo ananiachia ni kwa mema tu niliyomfanyia, ndani ya ile gari kulikuwa na brifcase iliyokuwa na pesa akaniambia pia hii pesa itakuwa yako ya kuanzia maisha, na kumbe yule dada alikuwa kanipenda akanikumbatia kwa nguvu nikiwa pale kwenye seat oooh!! umasikini baibai...

Akiwa kanikumbatia akihema kwa kasi juu ya kifua changu nikahisi mtu akinishika begani na  kuniita kwa sauti.
“Anko ankoo we ankoo... amka rafiki yako Salim anakuita!!!”.

“ALIKUWA MTOTO WA SISTA ALIKUWA ANANIAMSHA !!”.
Kumbe muda wote nilikuwa nikiota Dah...!!

Sunday, February 12, 2017

KWA WADADA MSIISAHAU NA HII

Msichana ana miaka 22, anafuatwa na mvulana na kuambiwa kwamba anataka kuolewa, mvulana yupo kamili, kajiandaa na anamaanisha, msichana anakataa kwa visingizio vya kipimbavu, mvulana anaachana nae. Anachokifanya ni kumfuata mtu ambaye hana mpango wa kumuoa, kisa gari kisa fedha anataka kuitwa mpenzi na mambo kuishia kitandani. Haiishii hapo, anapofika miaka 23, 24, 25, 26 hali inakuwa hivyo hivyo, kwake, anajiona hana haja ya kuolewa, anaamua kuwa na mpenzi tu, leo huyu, kesho huyu na keshokutwa yule. Siku hazimsubiri, miaka 27, 28, 29 na 30 inaingia, hapo ndipo anashtuka kwamba kapoteza muda na anatakiwa kuolewa. Hahaha! Mungu sio chizi. Mungu aliyajua maisha yako ya mbele, akakuletea wanaume mbalimbali wa kutaka kukuoa lakini ukakataa kwa sababu zisizo na mantiki. Kuolewa hauolewi, unaanza kuhangaika huku na kule, kila mwanamme kwako anaonekana kuwa muhimu. Yaani wakati ambao hukuuhitaji ndoa, ndoa ilikuhitaji na wakati ambao unaihitaji ndoa, ndoa haikuhitaji. Kwa mahesabu, kama una miaka 30 inakupasa kuolewa na mwanaume mwenye angalau miaka 33 au 35. Je kuna mwanaume mwenye umri huo ambaye yupo tayari kuoa? Mwanaume hataki kuitwa babu na mtoto wake, anataka kuitwa baba. Mwanaume anapofikisha umri wa miaka 30 anaweka jiko ndani lenye miaka chini ya 25. Sasa katika kipindi alichokuwa na miaka 30, ukamkataa, wewe ukiwa na miaka 30 mwenzako ana 35, keshaoa kitambo. Sikulazimishi uolewe ila unapopata mwanaume aliye radhi kukuoa, kubali tu, ndoa ni bahati, kuna wanawake wanafikisha miaka 40 na bado hawajaolewa na kila siku wanatamani kuolewa. Unapoipata bahati, fanya mambo. Siku zote mwanamme anapokwambia kwamba anataka kukuoa, ukaleta pozi weeeeee, akija kwa mara ya pili, huyo si muoaji, atakuja, atakuchezea na kukuacha, alikupa nafasi ukailetea pozi. 
WANAWAKE WAPO MILIONI 29 TANZANIA NA WANAUME MILIONI 25. HALAFU WEWE UNALETA POZI...HAYA, NGOJA TUONE MWISHO WAKE.

Monday, February 6, 2017

MAMBO TISA MUHIMU KUHUSU SIKU YA VALENTINE

NAAM. Ni wakati mwingine wa Valentine, ile siku ya wapendao ambayo huangukia mwezi huu. Wapo wapenzi, hususan wanaume ambao hawana wasiwasi wowote kuhusiana na ‘sikukuu’ hii. Lakini pia wapo wale ambao wanakuna vichwa, wakifikiria watawapa nini wapenzi wao ili kuonesha kuwa wanawapenda kweli.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhX2JaIRc05lMSQlvmTA5jEGjp3ZZ2yclSuwUmTCf6UhOceSbPcesKTUWAP8BWw7jtnpbTodnPMo7qY3fuoRivWPcegJcmvzNOTeMU99i0wjk0DlEJpNtGlii6NGBa-VeF_zE03cTrRKa_M/s1600/734-let-love-be-your-greatest-aim.jpg
Katika zama hizi, wasichana wengi wameingiwa na utamaduni wa Valentine na wapo wanaosubiri ili wapime mapenzi ya wapenzi wao kwa kuangalia jinsi watakavyofanyiwa siku ya Valentine ambayo mwaka huu inaadhimishwa kesho Jumatatu Februari 14, 2011.

Hata hivyo, hupaswi kuwa na shinikizo wala wasiwasi kuhusiana na suala hili, kwani pamoja na suala zima la zawadi, Valentine ni wakati muafaka wa kumfurahisha mpenzi wako na kumwonesha kuwa unamjali.

Zipo imani ambazo watu wamezishika tangu enzi na enzi kuhusiana na jinsi ya kusherehekea siku ya wapendanao. Kutokana na imani hizo, baadhi ya watu hupenda kupuuza taratibu za mapokeo na kutaka kufanya kitu kipya kwa mpenzi.

La msingi ni kutafuta njia iliyo rahisi zaidi kwako, ya kumfurahisha laazizi wako. Na kama bado unasitasita, mambo yafuatayo yanaweza kukusaidia: -

1. KUTOADHIMISHA VALENTINE'S DAY

Baadhi ya watu husema si lazima kusherehekea siku ya wapendanao, kwani si utamaduni wetu.

Ni kweli kwamba maadhimisho ya Valentine yameanzia Magharibi, lakini unapaswa kuangalia matazamio na matamanio ya mpenzi wako.

Mwanamke mwingine anaweza kujiona kama hapendwi anapobaini kuwa wanaume wengine waliwaandalia wapenzi wao hafla ya Valentine.

Kwa hiyo, badala ya kuipuuza kabisa siku hii, waweza kuipa umuhimu mdogo tu na ukatafuta njia zako mwenyewe za kuisherehekea.

Mathalani, waweza kupanga shughuli maalumu kwa ajili yako na mpenzi wako, ambayo mtaifanya kwa ushirikiano, huku akitambua kuwa siku hiyo ni siku ya wapendanao.

2. NI LAZIMA KUADHIMISHA FEB. 14?

Hakuna msahafu unaosema lazima siku ya wapendano iadhimishwe Februari 14. Kwa hiyo unaweza kuchagua siku nyingine kama huna nafasi siku hiyo, kwa ajili ya kumwonesha mpenzi wako kuwa unamjali na kumpenda.

Uzuri ni kwamba siku hiyo nyingine mnaweza kupata utulivu zaidi kwani hata katika kumbi za starehe hakutakuwa na watu wengi.  Mwanamke anayejali, hatajali mmeadhimisha lini, bali ataiangalia nia yako ya dhati ya kumfurahisha na kumwonesha kuwa unamjali.

3. MATUMIZI MAKUBWA YA FEDHA

Baadhi ya watu hufanya maandalizi makubwa kwa ajili ya siku ya wapendanao. Hata hivyo, kama una jambo jingine muhimu zaidi la kufanya, mathalani unasoma, hupaswi kutumia fedha nyingi kwa ajili ya siku hiyo.

Badala yake, kuwa mbunifu na kufanya jambo ambalo kwa hakika litamwonesha mpenzi wako kuwa unamjali kwa siku hiyo maalumu. Mathalani, mnaweza kufanya mtoko mdogo tu wa kwenda nje ya mji kwenye utulivu na kutafakari uhusiano wenu.

Atafurahi kuwa pamoja na majukumu mengi uliyo nayo, bado umekumbuka kuadhimisha mapenzi baina yako na yeye na kumfanya kujiona maalumu kwako.

4. WAPENZI AMBAO HAWAJAZOEANA

Baadhi ya watu ambao bado ni wapya katika mapenzi wanaweza kuona tatizo kusherehekea Valentine, maana hawana uhakika sana kama wanapendana.

Ni kweli kuwa si vema kufanya mambo makubwa na mpenzi ambaye hujafahamu mwelekeo wake, lakini haina maana kuwa umpuuze kabisa siku ya wapendano.

Iwapo utaipuuza kabisa V-Day anaweza akawa na shaka kuhusiana na mapenzi yako kwake, akidhani yamkini huna mapenzi ya dhati kwake.

Kwa hiyo, andaa kitu, si lazima kiwe cha kimahaba. Mathalani, waweza kuandaa shughuli ambayo inachangamsha, ambayo mtaifanya pamoja siku hiyo, au kumpeleka kwenye ukumbi wa maonesho ya sanaa, ambako mtapata nafasi ya kucheka na kufurahi pamoja.

5. CHAKULA SIKU YA VALENTINE

Watu huandaa chakula siku ya Valentine, kwa ajili ya kula na wapenzi wao, au wanaweza hata wakaenda kwenye migahawa ya bei mbaya katikati ya jiji kwa ajili ya kubadilisha mazingira.

Hata hivyo, si lazima kuingia gharama zisizo za lazima kwa ajili ya chakula. Katika jamii za Magharibi ambako ndiko ilikoanzia Valentine, watu hujishughulisha zaidi na mambo ambayo huwaweka pamoja, mathalani kuogelea, au kujifunza kitu chochote mathalani kupika, kucheza muziki na kadhalika na si lazima chakula. Waweza hata kumpa ofa ya kupaka rangi kucha zake na sherehe ikawa imeisha.

6. ZAWADI ZA CHOKOLETI NA MAUA

Kama ilivyobainishwa katika suala la chakula, chokoleti na maua si mambo mabaya kumpa mpenzi wako siku hiyo, lakini vimezoeleka na vinaweza visilete tofauti katika suala zima la mapenzi.

Badala yake, wakati watu wengine watakapovamia maduka ya maua , chokoleti na zawadi nyingine, wewe tafuta kitu ambacho ni ubunifu wako mwenyewe.  Mtafutie mpenzi wako kitu ambacho si mazoea.

Kama anapenda kusafiri na ikatokea kuwa siku hiyo haendi kazini, mpe tiketi ya kwenda mahali ambako mtakwenda pamoja. Kama anapenda muziki, mpe tiketi ya kwenda kwenye onesho maalumu la wapendano na kisha nenda naye.

7. ZAWADI ZA BEI MBAYA

Watu wenye fedha huweza kutumia fedha nyingi kununua zawadi za ghali kwa ajili ya wapenzi wao siku ya wapendanao. Lakini upendo wa dhati ndio muhimu katika siku ya wapendano.

Kwa sababu hiyo, mpe zawadi ndogo lakini yenye maana kubwa. Unaweza kufikiria zawadi yoyote rahisi ambayo una uhakika kuwa ataichukulia kuwa ishara ya mapenzi makubwa uliyo nayo kwake.

Wakati mwingine zawadi inaweza isiwe ya kitu halisi. Pengine ana wasiwasi kuwa humpendi, basi siku hiyo ndiyo siku ya kumhakikishia kuwa unampenda.

8. UTARAJIE ZAWADI KUTOKA KWAKE?

Mara nyingi watu huidhania sikukuu ya Valentine kama sikukuu ya kumfurahisha mwanamke na pengine ndivyo hata makala hii inavyoashiria.

Hata hivyo, hakuna sheria inayomzuia mwanamke kumfanyia kitu kikubwa mpenzi wake katika siku hiyo. Kwa hiyo hata usipotarajia zawadi kutoka kwake anaweza akakupa.

Lakini kama suala la zawadi linakusumbua na pengine ungependa uwepo usawa katika maadhimisho, basi waweza kuzungumza naye na mkashirikiana kupanga jinsi mtakavyoadhimisha siku yenu.

9. NI ZAWADI GANI MUAFAKA?

Hakuna sheria inayosema kuwa zawadi ya Valentine lazima iwe ya kimahaba, au kitu fulani tu. La muhimu zaidi ni kuifanya siku hiyo kuwa ya furaha na kuchangamka.

Baadhi ya watu hupenda kuwanunulia wapenzi wao nguo za ndani katika siku hiyo, lakini mara nyingi hiyo huwa sehemu tu ya safari ya kuelekea katika mapenzi.

Jambo muhimu zaidi la kuzingatia ni kuhakikisha kuwa unaweka mazingira ya ubunifu kwa ajili ya kumfurahisha mpenzi wako siku ya Valentine. Epuka kumwingiza katika mazungumzo yatakayomkera, bali zaidi tafuta kumfurahisha na kumchangamsha.

Siri ya kuifanikisha siku ya wapendano ni kuifanya kuwa siku yako, kisha kuwa mbunifu wa mambo ambayo una uhakika yatamfurahisha mpenzi wako na kumwonesha kuwa ni mtu wa pekee na muhimu kwako.

Siku ya Valentine haiko mbali. Ni kesho. Kwa hiyo kama una lolote unaloliwaza kuhusisana na mpenzi wako, ni vema kutafakari maelezo yaliyotolewa hapa, ili ujue jinsi ya kusherehekea.

Ifahamu Historia Ya Siku Ya Valentine’s Day

Kwa mujibu wa makala zilizoandikwa Birgit and Roger pamoja na www.history.com.Katika historia ya kanisa Catholic huko Rumi,http://stylespk.com/wp-content/uploads/2013/02/Ferozeh-Valentine%E2%80%99s-Day-Beautiful-Red-Dresses-2013-Collection-for-Girls-2.jpg
miaka 2000 iliyopita inasadikiwa kuwa taifa hilo lilikuwa kwenye vita ambapo Rumi kama mataifa mengine walihitaji askari wa kutosha kwa ajili ya shughuli hiyo.
Ilikuwa ni karne ya tatu wakati nchi ya Rumi ambayo kwa wakati huo ilikuwa ikitawaliwa na mtawala Cladius wa pili ambaye alitoa hoja ya kuhitaji askari vijana waajiriwe kwa wingi kwa ajili kwenda katika mapambano.Kwa imani aliyokuwa nayo wakati huo, Mtawala Cladius wa pili aliamini kuwa askari mwanaume kijana ambaye hajaoa huwa ni askari shupavu sana awapo katika mapambano ya vita. Hivyo basi, uongozi wa wakati huo ulipitisha amri ya kuwa vijana wote waliopo wajiunge na jeshi na iwe marufuku kwa kijana yeyote kuoa au kufunga ndoa ili waweze kushiriki kikamilifu katika kazi ya jeshi.
Baada ya amri hiyo kutolewa, raia wote walitii katika nchi ya Rumi. Ilikuwa ni uamuzi mzito sana hasa kwa vijana. Lakini kama tujuavyo, panapokuwa na jambo zito kama hilo si ajabu kwa binadamu kama tujuavyo kuanza kuwa na mbinu mbadala. Nilazima kutakuwa na mambo ambayo yatajitokeza katika kuzuia au kukwamisha amri kama hiyo ili mradi tu kuwe na mpango fulani bila kujali kuwa ni wa kujenga au kubomoa usifanikiwe kwa asilimia fulani.
Basi alikuwepo Kasisi mmoja wa kanisa Katholic ambaye aliamua kuendelea na kufungisha ndoa kwa vijana lakini kwa njia ya siri sana. Kasisi huyo alijulikana kwa jina la Valentine au Valentinus na ilikuwa ni miaka kati ya 270 baada ya Kristo (270 AD).Valentine alifanya kazi ya kufungisha ndoa kwa vijana wengi. Aliifanya kazi hiyo katika usiri mkubwa sana. Hivyo, siku jinsi zilivyokuwa zikisonga, mtawala Cladius alishangaa kuona vijana wengi aliowatarajia kuifanya kazi ya jeshi wengi wao walikuwa wameshafunga ndoa.Jambo hili halikumpendeza kabisa Mtawala Cladius maana ilikuwa ni kinyume na matazamio na matarajio yake kutokana na amri aliyokwishatoa.Siku zilivyozidi kwenda, siri hiyo iligundulika na Kasisi Valentine alikamatwa na kufungwa jela kwa kosa la kukiuka amri ya Mtawala wao. Alipokuwa kifungoni, kulikuwepo na makundi ya vijana ambao waliunga mkono huduma yake aliyokuwa anaitoa huduma kwa jamii, kwani waliamini kwa kufanya vile Father Valentine alikuwa akiwaokoa vijana wengi wakirumi kutokwenda kuishia jeshini. Vijana hawa walikuwa wakimtembelea mara kwa mara na kumtia moyo.Historia inasema kuwa, katika watu hao pia alikuwepo binti mmoja ambaye Valentine alimpenda na siku moja kabla kesi yake haijatolewa hukumu Father Valentine alimwandikia barua binti huyo na mwishoni aliweka sahihi yake kama ‘Kutoka kwa Valentine’ au kwa lugha ya kiingereza tungeweza kusema ni ‘From your Valentine’ maneno ambayo mpaka leo yanatumika kama Valentine ni mpendwa au mpenzi wako.Hali hii inadhihirisha kuwa, Fr. Valentine ndiyo aliyekuwa mtu wa kwanza kuhamasisha jamii kuendelea kupeana salamu za upendo kwa kila mmoja na kuita kuwa ni salamu za Valentine. Hivyo basi Fr. Valentine ndivyo alivyokuwa, nay eye ndiye Muasisi wa siku ya wapendao.Jambo lingine la muhimu, ni kufahamu kuwa kwa nini sherehe hizi zikachaguliwa ziwe zinafanyika mwezi wa Februari katika tarehe za katikati ya mwezi huo, hii ni kwa sababu Fr. Valentine baada ya kuhukumiwa alipokuwa kifungoni, hukumu yake ilikuwa ni kunyongwa, na alinyongwa katika majira hayo hayo ya katikati ya mwezi Februari hiyo ndiyo sababu ya kuweka tarehe 14 Februari kuwa ni siku ya ‘Wapendao’ au ‘Valentine Day’ kwa kuzingatia kuwa mwezi February una siku kati ya 28 au 29 tu.Vilevile, inahisiwa kuwa mbali na siku ya wapendanao kuhusishwa moja kwa moja na Fr. Valentine, vilevile hii ni siku ambayo mazao ya nafaka ambayo ni chakula kizuri kwa watu wengi wakati huo ndio majira ya uvunaji na upandaji wa mazao mbalimbali katika nchi ya Rumi (Roman).Pia wapo waliokuwa wakisema kuwa, mwezi Februari umetambulikana kama ni ‘Siku ya Wapendanao’ katika nchi yetu na kwingineko, kwani wakati huo huwa ipo aina Fulani ya ndege jike huwa ndiyo majira yao ya kukutana na ndege dume. Ambapo hii hudhihirisha kuwa tarehe 14 ya mwezi wa pili ni siku ya wapendanao na kwa wale wenye kuwakumbuka wazazi wao ama ndugu wa karibu.Nchi kama Uingereza, tarehe 14 Februari ya kila mwaka kuanzia karne ya 17 na 18, pia huadhimisha siku ya ‘Wapendanao’, kwa wapenzi na wachumba. Jambo hili lilianza kuzoeleka kidogo kidogo na baadaye kuweza kujengeka katika nchi ya Rumi yote na baadaye kusambaa kidogokidogo.Siku za mwamzoni, watu wengi walikuwa wakitumiana salamu hizi kwa kuandikiana barua, ambapo baadaye kidogo kwenye karne ya kumi na nane hali hiyo ilianza kwisha na kuingia kwa Kadi maalumu ambapo zinakuwa zimejaa katika maduka mbalimbali pamoja na maua ya kupeana kwa wale wapendanao. Na sasa baada ya teknolojia kuongezeka salamu zinatumwa mno kwa njia ya text meseji za kwenye simu za kiganjani.Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa karibia kadi za Valentine bilioni moja zilikuwa zikinunuliwa na kutumwa sehemu mbalimbali hapa duniani, hii inafanya kuwa ni sikukuu kubwa ya pili duniani kwa watu kutumiana kadi, sikukuu ya kwanza ni X-mass ambapo inakisiwa karibu kadi zipatazo bilioni 2.6 hutumwa sehemu mbalimbali za dunia katika kutakiana heri ya X-mass.Aidha, imegundulika kuwa, pamoja na wanunuzi au waandalizi ya shughuli hii kuwa wengi, lakini inakisiwa kuwa asilimia 85 ya washabiki wa masuala hayo ni wanawake.Kwa ufupi kutokana na ufafanuzi huu, angalau wengi twaweza kufahamu nini kinajiri katika suala zima la Valentine Day.Namalizia kwa kusema, maadhimisho ya ‘Siku ya Wapendanao’ yaanzie katika familia zetu, majirani zetu na hata makazini. Waandishi wa habari tupendane wenyewe kwa wenyewe ikiwa kama ishara ya kudumisha nia na malengo ya kazi zetu katika kuielimisha jamii.
Happy Valentine Day!!!!

Sunday, February 5, 2017

JE UNAELEWA CHANZO CHA VALENTINE'S DAY NA NINI UNATAKIWA UFANYE


Februari 14 kila mwaka, dunia nzima imekuwa ikisherehekea Siku ya Wapendanao, maarufru kama ‘Valentine’s Day’, kwa wengi wao kutumiana zawadi za maua, kadi na nyinginezo, ambazo hufungwa ndani ya maboksi mekundu.

Katika miaka ya karibuni, sikukuu hii imepata umaarufu zaidi nchini kwa kuifanya kuwa sherehe kubwa, ingawa bado haijatambuliwa kitaifa lakini imeonekana kuwagusa watu wengi.

Katika makala hii tungependa kuzungumzia kwa undani kuhusu sikukuu hii, ikiwamo historia na namna ambavyo inatakiwa kusherehekewa na makosa yanayofanywa katika sherehe hii kwa kizazi cha sasa.

Historia yake
Mwanzo wa kuanza kuisherehekea sikukuu hii ilikuwa ni karne ya tano, ambako Kanisa Katoliki lilieleza nia yake ya kutaka kumaliza ukuaji wa mila za wapagani ambazo wananchi wa Roma walikuwa wakizisherehekea kila mwaka tangu karne ya nne BC.

Kutokana na mila za Waroma wakati huo, walikuwa wakifanya siku ya Februari 14 aina ya kamari maalumu waliyokuwa wakiwashirikisha vijana wao wa kike na wa kiume kwa ajili ya kupeleka zawadi kwa ‘mungu wao’ waliyekuwa wakimuita kwa jina la Lupericus.

Hivyo vijana wa kike walishiriki katika kamari hiyo kwa kuweka majina yao kwenye kiboksi na kasha la vijana wa kiume na baada ya kufanya hivyo vijana wa kiume walitakiwa kuchagua majina hayo na msichana aliyebahatika kuchaguliwa na mvulana fulani, hapo huwa na mvulana huyo kwa mahusiano ya kimapenzi kwa kipindi chote cha mwaka mzima hadi kamari ya mwaka unaofuata.

Kanisa halikufurahishwa kabisa na mpango huo wa kiibada za Waroma ambazo zilikuwa na nia ya kufanya mapenzi kiholela kupitia kamari na likaamua kutokomeza mila hiyo kwa kuchagua ‘mpenzi’ ambaye huozeshwa badala ya mila ya kamari ya ‘mungu Lupericus’.

Ili kufanikisha hilo, kanisa likamchagua Askofu Valentine, mtu ambaye alihukumiwa kuuawa katika karne ya 3 AD kutokana na kukaidi amri ya mtawala (Emperor Claudius).

Mtawala huyo alipiga marufu watu kuoa kwa madai kuwa wanaume wanaooa wanafanya vibaya vitani na wakati mwingine huwa hawataki kuacha familia zao na kwenda vitani.

Askofu Valentine alikuwa akipinga amri hiyo na badala yake alikuwa akiwaalika na kuwafungisha ndoa kwa siri wale waliokuwa wakihitaji kufanya hivyo.

Baada ya kubainika kufanya hivyo kisiri, aliuawa na kabla ya kuuawa alituma ujumbe wa mapenzi kwa binti wa mlinzi wa jela aliyewahi kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi.

Ujumbe wake ulikuwa ukisomeka kwamba: ‘Kutoka kwa Valentine wako (from your Valentine)’.
Barua hiyo ilipata umaarufu na neno hilo likatumiwa na Kanisa Katoliki na kuchagua Askofu Valentine awe mfano wa kuigwa kwa wapendanao na kutokemeza ibada za kipagani za kufanya mapenzi kiholela kwa kuchagua mwanamke kwa njia ya kamari na badala yake wakishapendana wafungishwe ndoa.

Lakini kutokana na nidhamu ya kidemokrasia kuibuka katika nchi zao na watu kuacha mafunzo ya kidini na kuburuzwa na fikra za ‘uhuru’, siku hiyo ikawarejesha kule kule katika zama za wapagani kwa kuhamasisha uchafu wa zinaa nje ya ndoa.

Makosa yanayofanywa kuisherehekea
Pamoja na makusudio hayo, lakini kwa sasa kumekuwa na makosa ambayo yamegunduliwa kufanyika katika sherehe hii ambayo ni maalumu kwa wapendanao kuzidisha upendo.
Katika sikukuu hii wanaume hasa ndio wamekuwa wanaelezwa kufanya makosa ambayo wameyaona ya kawaida kwao bila ya kujali yanaathiri mahusiano yao kwa kiasi gani.

Kosa la Kwanza: Kutozungumza maneno ya hekima
Hakikisha katika siku hii unazungumza maneno ya busara ikiwa ni pamoja na kumwandikia meseji mpendwa wako za kumfurahisha kwani katika uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa wanawake wengi wanapenda kuzawadiwa kadi na kuandikiwa maneno mazuri ya mapenzi huku wakiwa sambamba na wapendwa wao.

Pili: Uchaguzi wa zawadi
Mtaalamu wa masuala ya saikolojia ya mapenzi, Dk. Terri Orbuch, anasema zaidi ya asilimia 75 ya wanawake wamekuwa wakipenda kupewa zaidi. Lakini wanaume wengi wamekuwa wakishindwa kuwanunulia zawadi kutokana na fikra potofu wakidhani zawadi nzuri ni kubwa peke yake ndiyo itaweza kumpatia heshima.
Wanafikiria zawadi ni lazima ununue vitu kama magari au vito vya thamani na kumbe wanawake hufurahia zawadi za kawaida kama chocolate, kadi na maua ikiwa ni pamoja na kuambiwa maneno matamu ya kimahaba.
Ni vizuri katika siku hii kwenda dukani na kumnunulia mpendwa wako zawadi za maua mazuri, vitabu vya mahaba, DVD za mapenzi, mishumaa, chocolates na nyingine za aina hiyo.

Yakupasayo kuyafanya
Jitahidi kuonyesha tabasamu lako unapokuwa na mpenzi wako na kununua zawadi za kawaida, kwani hii humsaidia mpenzi wako hasa yule asiyekuwa na uwezo naye kukununulia kama hiyo, kwani wengi wamekuwa na mtindo wa kurudisha zawadi inayofanana na ile uliyomnunulia.
Tahadhari nyingine kwa siku hii ni kuepuka kumuonyesha mwenzako mambo ambayo unajua yataleta maudhi kwake, hivyo kufanya siku hiyo kuwa mbaya kwenu.
Suala la kuchati kwa wapendanao siku hii ni muhimu ambako linasaidia kuongeza upendo kwa wawili na hii haijalishi ni njia gani unaitumia iwe kutuma meseji za simu au barua pepe za mtandaoni au unaweza kutumia mitandao ya Facebook na Twitter, hii itamfariji hata yule aliye mbali nawe.
Wakati mwingine unaweza kutumia barua ambayo itakuwa na maneno mazuri, ikiwa sambamba na picha ambayo nyuma yake ukiwa umeiandika ujumbe mzuri wa kimahaba ikiwa ni pamoja na CD iliyojaa nyimbo za mapenzi ili asikilize ukiwa umempatia kama zawadi.

Namna ya uvaaji
Siku hii pia ina namna yake ya kuvaa ambapo kwa mwanamke ni vema ukavaa gauni jipya na fupi ambalo litamvutia mwenzio huku mwanamume yeye akitakiwa kuvaa suruali ya kitambaa na shati la mikono mirefu au mifupi na si vibaya kama utavaa tai ndogo. Pia si vibaya kuvaa suti.

JIFUNZE NJIA SAHIHI KUMI ZA KUMTAMBUA MKE,MME AU MCHUMBA MWENYE MAPENZI YA DHATI

Wengi wamejikuta wakiitwa wahuni kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na makundi ya wanaume au wanawake. Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya mapenzi wanasema idadi kubwa ya wapenzi si kigezo sahihi cha kupima tabia ya mtu na kumhusisha na uhuni.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhBiGQEAUpPwLa2x1Vr4ZrSQ0CGnQHhLeB45Sia2Nmr_EixuoRgBMeK0LJ3n5LUTzXUoVKwA8lOulHSNF9iwjl53gQw-lKoVekoKAthDP_SkK_iW_9Dry8QEVy5GYUM3z8WBgXcnPlaSvE/s640/black-couple-happy.jpg
Watalaam hao wanataja safari ya kupata chaguo halisi la mwanaume/mwanamke wa maisha ndiyo inayowaponza wengi kiasi cha kujikuta wameingia katika kashfa ya kuwa na uhusiano na dazeni ya wapenzi.

Wanasema msichana/mvulana anayeingia katika uwanja wa mapenzi kwa kuwa na hisia za kufanya ngono, hukosa umakini wa nani anafaa kuwa mpenzi wake kutokana na kukosa elimu ya uhusiano kutoka kwa wazazi wake.

Kwa mantiki hiyo, bila upembuzi wa kina, mtu asiye na elimu ya jinsi ya kumpata mpenzi wa kweli hujikuta ameangukia kwa mwanaume/mwanamke asiyemfaa, ambapo baadaye huamua kuachana na huyo na kwenda kwa mwingine kujaribu bahati tena ya kupata penzi la kweli.

Zinatajwa zawadi, hitaji la kusaidiwa kimaisha, mvuto wa kimahaba na mazoea kuwa ni vichocheo vinavyowaangusha wengi kwenye mapenzi na wasiowafaa.

Ukweli ni kwamba mtu aliyenaswa kwa ‘ujinga’, huwa hakatwi kiu ya penzi na mwanaume/mwanamke asiye chaguo sahihi la maisha yake. Hivyo hufikia maamuzi ya kujiingiza katika uhusiano mpya mara 2,3,4,5 na kujikuta wakiambulia wanaume/wanawake wale wale wasio sahihi kwake.

Mwanamnke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jai kuniomba ushauri, akasema amechoka kuchezewa, maana kila mwanaume anayempata anakuwa si chaguo lake. Lakini kibaya zaidi kuachia ngazi au kutemwa huku akiwa tayari ameshafanya mapenzi na wanaume hao.





Ni madhumuni ya somo hili kufundisha vigezo vya kumpata mwanaume/mwanamke halisi wa maisha, bila kufanya naye mapenzi. Njia hii ina faida kwa pande zote mbili yaani kwa mwanamke na mwanaume kwani kuacha au kuachwa bila kufanya mapenzi ni bora kuliko kuwa muonjaji, tabia ambayo huathiri kisaikolojia na ni hatari kwa afya.

Ifuatavyo ni njia ya kisaikolojia ambayo mwanamke anaweza kutumia kumpata mwanaume mwenye kumfaa bila kufanya naye mapenzi tena ni jibu sahihi la kuondokana na mchezo wa kubahatisha kwa wanaume wanaosaka wapenzi wa kweli na si taksi bubu ambazo mchana huweka namba za njano usiku nyeusi.

KWANZA- Ni ya mwanamke/mwanaume mwenyewe kujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi anayemhitaji katika maisha yake. Ifahamike kuwa kila mwanaume ana wake na kila mwanamke anaye wake wa maisha pia. Hivyo asiyekufaa wewe anawafaa wengine, kinachotakiwa ni wewe kujitambua kwanza ili umtambue umtakaye.

Wanawake/wanaume wengi hawafahamu wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewe na kuumizwa moyo bure.

PILI- Ni kuketi chini na kuorodhesha vigezo stahili vya mwanaume/mwanamke unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume/mwanamke unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika, ana upungufu wake.

TATU- Anza kumsaka kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume/wanawake na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kurithika na mwili kusisimka.

NNE - Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.

Katika uchunguzi huu mwanamke/mwanaume anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume/mwanamke anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.

TANO - Ajipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume, kisha aketi chini na aanze kujumlisha alama za vigezo alivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa.

Ikibainika mwanaume aliyechaguliwa amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizikosa anaweza kusaidia kuzikamilisha polepole wakati wa maisha ya ndoa.

Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume/mwanamke akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.

SITA - Kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda.

Hata hivyo watalaam wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu.

SABA - Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huacha kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana

NANE - Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu hilo na kuamua ufanyaji huo wa mapenzi una lengo gani, kama ni kuburudisha miili basi suala la afya na uzazi salama litazamwe.

TISA - Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si busara ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.

KUMI - Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidia, kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya na hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake.

Mwisho ni kwamba kanuni hizi huwafaa watu wazima mapenzi ya kitoto hayawezi kujenga misingi hii imara mara nyingi ni kudanganyana, kuharibiana maisha, kupeana mimba na maradhi.