Moja ya matatizo makubwa kwa wanaume ni unyoaji wa ndevu, kitu ambacho
wakati mwingine huwakera wahusika na wao kujiona kama ni wafungwa. Ndevu
huwafanya wanaume wengi kuhisi kuwa ni tatizo kubwa sana kwao kwani
wakati wa kuzinyoa huwa ni tatizo kubwa kutokana na wengine kuweza
kupata matatizo wakati wa kunyoa ndevu.
Ili kuondoa matatizo haya yafuatayo yanaweza kabisa kukusaidia kukuweka
katika aina Fulani ya raha kubwa. Chagua mashine ya kunyolea na wembe
ambao unadhani unaswihi ngozi yako, kuna aina nyingi sana za mashine za
kunyolea pamoja na nyembe zake ni muhimu kujua wembe ambao unatumia kwa
kuzingatia mahitaji yako hasa ya aina ya ndevu.
Weka uso safi na usio mchafu, Safisha kabla ya kunyoa, hii inakusaidia
kufungua matundu yanayoshikilia ndevu kabla ya kunyoa ili kuweza kupata
mnyoo laini na wenye uhakika.
Usisahau kuloweka kidevu chako vyema, hii inasaidia wenye kupita
kiulaini zaidi na kama unatumia kiwembe cha kawaida basi ni vyema sana
kufanya kazi hiyo ukitoka kuoga.
Tumia maji ya moto siyo yanayounguza kama inawezekana, yanasaidia sana
kufungua vishimo vya vinyweleo, pia unaweza kupata masaji ya chapchap
katika uso ili kusaidia kulainisha kidevu chako.
Chagua krimu hasa inayostahili kwako ya kunyolea kwa kutegemea ngozi
yako na chagua linalostahili unalotaka, jipake kiasi cha kutosha katika
sehemu zinazostahili kwani husaidia kuburudisha ngozi.
Baada ya kujinyoa, osha uso wako na ondoa krimu zote,tumia moistrurizer baada ya kunyoa.
No comments:
Post a Comment