kuna sababu nyingi sana zinazoweza kuharibu mimba ya mama ikiwemo ugonjwa wa malaria, kaswende, kazi nyingi, magonjwa ya zinaa, u.t.i dawa fulani fulani mfano albendazole, misoprostol, metronidazole na kadhalika. lkiujumla sababu nyingi ambazo zinasababisha mimba kutoka huweza kuzuilika kwa kwenda kliniki mapema yaani pale tu unapohisi una mimba hata kama ni wiki mbili na kufuata ushauri wa wataalamu. sasa kuna wanawake wengi mimba zo huharibika na wao hushindwa kugundua mapema na matokeo yake anakaa na mtoto mfu hata miezi kadhaa bila kujua hivyo leo ntaongelea dalili za kuharibika kwa mimba kama ifuatavyo.
kutokwa na damu nyingi sehemu za siri; hii ni dalili kwamba mimba
imeanza kuachia na mlango wa uzazi umeanza akufunguka sasa ukienda
hospitali utakuta majibu mawili kwamba mtoto ameshafia tumboni au bado
hajafa. lakini kama imeshatoka damu nyingi mtoto huyu atakufa tu.
mtoto kuacha kucheza tumboni; kwa kawaida mtoto huanza kucheza
wiki ya 18 mpaka 20 kwa wanawake ambao hawajawahi kubeba mimba na wiki
ya 16 mpaka 20 kwa wanawake ambao wamehsawahi kuzaa sasa ikitokea mtoto
ameshawahi kucheza na sasa hachezi tena au muda huo umepitiliza na bado
kimya kuna uwezekano mkubwa ameshafariki.
kupotea kwa dalili za ujauzito; mara nyingi mtu akipata ujauzito
anakua na dalili nyingi kama kichefuchefu, kukosa hamu ya kula, kutapika
sana na kubadilika sana tabia sasa zile dalili zote za mimba zikisimama
ghafla basi ujue mimba imeharibika.
kuacha kuongezeka kwa mimba; tunategemea mimba kuendelea kua
kubwa kulingana na umri unavyozidi kwenda mbele sasa kama mimba mara ya
mwisho ilikua na miezi mitatu na leo ina miezi sita au mitano lakini iko
haijabadilika ukubwa ujue mimba imeharibika.
maumivu makali ya tumbo; maumivu makali ya tumbo hasa kwa mimba
kubwa sana au mimba ndogo sana kuna uwezekano mkubwa kondo imeanza
kujiondoa kwenye kizazi kwa mimba kubwa au mimba ndogo imeshindwa
kuendelea kukua. hii inaweza kua dalili kwamba mimba imeharibika.
kutoka kwa vipande vya nyama sehemu za siri; vipande vya nyama
huashiria kwamba kuna mtoto anakua ameharibika tayari tumboni na mama
kama huyu anatakiwa asafishwe kuondoa masalio yaliyobaki ili mama
asiweze kupata madhara zaidi.
No comments:
Post a Comment