MAHITAJI YA MWANAMKE
1. Mvuto na ukaribu (affection) – maneno na matendo yachochee mvuto na ukaribu, Kwamfano. Kukubali alivyopendeza, kumsifia nk
2. Mazungumzo
(conversation) – mwanamke huumizwa sana na vipindi virefu vya ukimya,
sio tu kwamba wanataka mazungumzo bali mazungumzo yenye hamasa na mvuto
3. Kumwamini
(trust) – mwanamke anakiu ya kuaminiwa, anataka mtu aliye muwazi, asiye
ficha kitu chochote, anatamani umwamini na sio kuhofia kila
anachokifanya au kumhofu kila aliyeko naye
4. Ulinzi
(security) – mwanamke anapenda kuhakikishiwa ulinzi na usalama wake
kiafya, kihisia, na kiuchumi. Sio yeye tu bali na familia yake yote.
5. Ushirikishwaji
ktk mambo ya familia (participation) – Sio kila kitu kinafanyika yeye
hajuo, anaona tu vitu vinaenda kama vile yeye sio mmoja wa wanafamilia
na mzazi. Mfano, anagundua unasomesha ndugu yako pasipo hata yeye kujua.
Mwanamke anatamani kuona anashirikishwa katika yote yahusuyo nyumbani
kwake maana kwake nyumbani ndiyo kitovu cha maisha yake zaidi ya kazi
yake na marafiki zake
No comments:
Post a Comment