Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Sunday, August 20, 2017

Habari Mbaya Kwa Wanaongalia Video za Ngono Kwenye Simu.....



Hatujaribu kumhukumu mtu yeyote kwa mazoea yake. Kila mmoja ana uhuru wa kutumia simu yake kufanya anachojisikia yeye (hata ikiwa ni kwa kuangalia video za ngono kutoka mtandaoni au zilizohifadhiwa ndani ya kifaa hicho).

Lakini inatakiwa uwe makini kama kuwa unapakua app za bure za ngono kwa kutumia simu yako ya Android, kama ambavyo mtaalamu wa ulinzi mtandaoni wa kampuni ya teknolojia ya Dell, Alex Dubrovsky alipogundua kwamba kuna udukuzi unaofanywa ili kuziathiri app hizo.

Wadukuzi wametengeneza mfumo wa kuiathiri simu unaofichwa ndani ya app hizo ambazo zina uwezo wa kuifunga simu ya mtumiaji na hata kukuzuia usiweze kuifuta app hiyo kutoka kwenye simu yako unapotaka kufanya hivyo.

Dubrovsky na timu yake ya watafiti walmebainisha kuwa wadukuzi wana uhakika kabisa wa kutumia app za ngono kufanya mashambulizi yao: mtumiaji anapakua app na kuwapa wadukuzi njia ya kuingia kwenye simu yako na kuitumia kama ipo kiganjani kwake na kwamba inawapa uwezo wa kufanya chochote. Na kwa wale wanatumia Android toleo la 4.4 KitKat, wadukuzi wanaweza kuifunga kabisa simu yako na kukuzuia usiweze kuifungua tena kama wakitaka.

 “Kutokana na teknolojia ya sasa, ushambuliaji wa aina hii bado unafanywa kwa kiwango kidogo lakini inaelekea utaongezeka kwa kasi kadri muda unavyosonga mbele,” ameandika Dubrovsky. “Kinachoshangaza ni kwamba mpaka sasa, waliofanyiwa udukuzi huu hawajawahi kuombwa pesa ili simu zao zifunguliwet, na pia kwakuwa bado waliokumbana na udukuzi huu wameweza kutumia tena simu zao ni ishara kwamba mfumo huu wa udukuzi haujaanza kutumiwa kwa kiwango cha juu.”

Kwahiyo, ingawa aina hii ya udukuzi bado ipo kwenye hatua za awali ambao kwa sasa walengwa ni watumiaji wa mifumo ya zamani ya simu za Android na kwa kutumia app za ngono pekee, inatabiriwa kuwa baada ya muda udukuzi huu utatumiwa kwenye mifumo ya kisasa zaidi na app nyingine nyingi zaidi (kama wadukuzi wakiweza kupita kwenye mfumo wa ulinzi wa  Google).

No comments:

Post a Comment