Punyeto ni kitendo cha mtu kujigusagusa au kujipapasa mahali popote mwilini kwa nia ya kujitosheleza kingono. Tendo hili linajulikana kama masturbation kwa kimombo.
Kwa mara mingi, punyeto hufanyika kwa kujigusa sehemu za uzazi mpaka kufikia kilele. Tofauti ya tendo hili ni kuwa mwanaume au mwanamke anayelitenda hamhitaji binadamu mwingine ili kujitosheleza. Hivyo basi, punyeto haikubaliki kama aina ya ngono.
Swali kubwa linalozunguka kitendo hiki ni je, kuna madhara ya punyeto?
Ukweli ni kuwa, ingawaje watu wengi husema kuwa punyeto ni kitendo kisicho na madhara yoyote, kuna madhara kadhaa yanayoweza kutokea. Madhara haya, kwa mara mingi, huwa si magonjwa. Madhara yanayoweza kutokea huadhiri mtu kimwili au kiakili. Baadhi ya madhara ya punyeto yameelezwa hapa.
- Kutoacha
Kitendo cha punyeto ni kama madawa ya kulevya kwani mtu anapokizoea, hawezi kuacha kwa urahisi. Ifikiapo kuwa mtu amelemewa kuacha, inabidi asake usaidizi kutoka kwa wataalamu wa afya.
Tena, kulemewa kuacha kunaongeza madhara mengine yatokanayo na punyeto kama yatakayotajwa hapa.
- Mawazo kuchafuka
Mtu anapotenda tendo hili, inabidi aufunze mwili wake kuona kuwa analitenda na binadamu ambaye hayuko pale.
Hivyo basi, fikira zake huwa kali zaidi na anapowaona watu wa jinsia nyingine, au sawa, basi anaanza kufikiria akitenda ngono nao. Hali hii huzidi na mtu hawezi kuiacha kwa urahisi bila usaidizi wa wataalamu wa saikolojia na afya.
- Kutizama ponografia
Muda unavyozidi kwenda, mtu anayetenda tendo hili huacha kupata hisia za kingono kwa kuwafikira watu tu.
Hivyo basi, inambidi aanze kutizama picha au kanda za ponografia ili kupata hisia hizo na kulikamilisha tendo la punyeto. Kama madawa ya kulevya au tendo hili, ni vigumu kwa mtu kuacha kutizama ponografia kwa urahisi. Hii pia ina madhara yake.
- Uchafu
Wanasayansi huhimiza wanaotenda punyeto kujaribu na kuwa wasafu kabisa kwani ni rahisi kwao kuchafuka. Hii ni kwasababu wanaweza kutenda punyeto mara kadhaa kwa siku na inaweza kuwa vigumu kuvisafisha vyombo wanavyotumia katika tendo hili.
Hivyo basi, wengi hulemewa na usafi huu na kuwa wachafu. Vitanda, nguo, vyoo na vitu vingine huwa vichafu nawatu wengine hawawezi kuvitumia.
- Aibu
Wanyama na binadamu waliumbwa kwa njia kwamba wanahitaji kiumbe mwenzao ili kujamiiana. Mtu anapotenda punyeto, hafanyi hivi.
Hivyo basi, iwapo watu wengine wataijua tabia hii yake, anaweza kuhaibika sana kwani hili sio tendo linalokubalika katika jamii. Aibu inaweza kumtenganisha na watu wengine.
- Magonjwa
Ingawaje punyeto haisababishi magonjwa ya zinaa, inaweza kuleta magonjwa mengine kulingana na mtu anavyotenda kitendo hiki.
Kwa wanawake wanaotumia vitu kama tango au ndizi kujitosheleza, wanaweza kupata magonjwa hatari kutokana na kemikali zinazotumiwa kupandia vitu hivi. Tena, iwapo mtu ni mchafu na vitu au mahali anapotendea punyeto ni pachafu, anaweza kujipatia magonjwa kama UTI (urinary tract infection).
- Unyonge
Tendo la punyeto hutumia nguvu nyingi ya mwili kama ngono. Hivyo basi, mtu anapozoea tendo hili na kulitenda mara kadhaa, basi hutumia nguvu nyingi. Hii huchangia kwake kuwa mnyonge kila anapolitenda.
Iwapo atazidi, basi huenda misuli yake ikalegea na kunfanya mvivu na mnyonge.
- Kupoteza muda
Wakati ambao hutumika kwa tendo hili huwa mwingi, sana sana mtu alemeapwo kuacha. Kwa mfano mtu aamkapo na kuanza tendo hili, anaweza kuchelewa kwenda kazini.
Pia, muda unaotumika wakati wa punyeto unaweza kutumika kufanya mambo ya faida zaidi.
- Msongo (stress)
Watu wengi ambao hutenda punyeto husema kuwa baada ya kumaliza, wao hubanwa na hisia mbaya. Wanaweza kujichukia au kuhisi kuwa hawajiskii kuhusiana na watu wengine.
Hisia hizi zinapozidi, huenda mwathiriwa akapatwa na msongo, yaani stress. Pia, msongo unaweza kupatikana kutokana na watu kujua kuwa mtu hulitenda.
- Shida za mfumo wa neva (nervous system)
Sehemu ingine ya mwili ambayo huathirika ni mfumo wa neva. Sehemu hii huathirika kwamba mtu hushtuka na hisia tofauti kuongezeka au kupungua.
Kwa mfano, anaanza kushtuliwa na vitu kwa urahisi. Pili, moyo wake hupiga kwa kasi na nguvu zaidi kuliko kawaida.
- Shida za nguvu za kiume
Wanaume hupata madhara haya baada ya kutenda punyeto kwa muda mrefu. Shida hii hutokea kwani njia watumizo kulitenda hazifanani na uke wa binadamu.
Kwa mfano, wengi hutumia mkono uliopakwa mafuta au kitu telezi. Mkono huwa mgumu na baridi kuliko uke. Hivyo basi, afanyapo mapenzi na mwanamke, uume wake huhisi joto jingi na ulaini zaidi, hivyo basi kupunguza muda wa kufanya mapenzi.
- Shida za nguvu za kike
Kwa wanawake, vifaa watumiavyo pia huathiri nguvu zao za kike. Vifaa wanavyotumia kama vile tango na vingine ambavyo huundiwa kazi hiyo huwa vigumu kuliko uume wa binadamu.
Hivyo basi, wanapovizoea, miili yao huzoea vitu vigumu na hawawezi kutoshelezwa na uume kwa kawaida. Hivyo basi, wanazoea vifaa hivyo na kuachana na wanaume.
- Uchoyo
Wanasaikolojia wanasema kuwa punyeto humfanya mtu kuwa mchoyo. Hii ni kwasababu mtu huzoea kujitosheleza na kutohitaji mwenzake. Tabia hii huathiri hata akili na kumfanya mtu kuwa mgumu na vitu vyake.
Mtu aliyekuwa mkarimu anaweza kugeuka na kuwa mchoyo zaidi. Hii huzidi na kumfanya mpaka kuwa mchoyo na mwili wake, yaani hawezi kufanya mapenzi na binadamu mwenzake.
- Shida katika ndoa
Punyeto huathiri hata ndoa. Iwapo mke au mume anatenda punyeto, basi madhara yaliyotajwa hapa huweza kuiingilia ndoa na kuiharibu. Kwa mfano, iwapo mwanamke hatosheki, shida huweza kutokea.
Tena, iwapo mwanaume hatosheki au hamtoshelezi mkewe, shida pia huweza kutokea. Shida hizi ni kama wao kuwa na uhusiano nje ya ndoa ua ndoa kuvunjika.
- Kupungua kwa mbegu za kiume
Kwa kawaida, mwili wa mwanaume hufaa kutengeneza mbegu za uzazi mara tu zinapotumika. Lakini, iwapo mwanaume ana mazoea ya kutenda punyeto mara kadhaa kwa siku, huenda akaathiri mfumo wa kuzitengeneza.
Mwishoni, mfumo huu huchoka na kuanza kutengeneza mbegu chache na hafifu. Hali hii ikizidi, mbegu hizo hupoteza nguvu za kuzalisha watoto wenye afya au kutozalisha kabisa.
- Tabia za ngono zisizo za kawaida
Punyeto huzidi kuongeza hamu ya kufanya mapenzi kwenye mwathiriwa. Hivyo basi, wakati hufika na mtu kuwa hawezi kujitosheleza kwa njia alizozoea. Hivyo basi, anaweza kujaribu njia zingine.
Hamu hii huchangia mtu kutenda vitendo haramu kama vile ushoga au kuwabaka wanyama. Kwa watu wengine, wao hufanya mapenzi na watu wa familia au hata kuwabaka watoto wadogo. Tabia hizi ni haramu na huweza kuleta shida kuu za kisheria.
Hitimisho
Kama uandishi huu unavyobaini, tendo la punyeto lina madhara kwa binadamu. Madhara haya huathiri mwili na akili pia. Hata hivyo, kuna madhara zaidi yanayotokea, sio haya tu yaliyotajwa.
No comments:
Post a Comment