Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Wednesday, August 23, 2017

Majina Ya Watoto Wa Kiume (26)


Katika tamaduni nyingi, majina ya watoto wa kiume hutokana na majira au matukio ya wakati wanapozaliwa. Kwa mfano, wakati mmoja, mwanamke Mwethiopia alijifungua mtoto wa kiume. Shangwe yake ikageuka kuwa majonzi alipoona mtoto wake akiwa amelala bila kusonga.
Nyanya yake alipomchukua mtoto huyo ili amwoshe, kwa ghafla mtoto akaanza kusonga, kupumua na hata kulia. Hali hii ikawa chanzo cha jina la mtoto na hiyo wazazi wake wakaunganisha jina muujiza na neno  linguine la Kiamhara na kumwita mvulana huyo Muujiza Umefanyika.
Nchini Burundi, majina memgin yalitokana na wakati wa vita vilivyokuwemo mwanzo wa miaka ya tisini. Mtoto aliyezaliwa huku mzazi akijifichakutokana na machambulizi angepatiwa jina kama Manirakiza amabalo maana yake ni’Mungu Ndiye Anayeokoa’. Majina mengine ya wakati ule ni kama Twagirimana na Mwana wa Imana ambayo pia humaanisha mwana wa Mungu au mtu aliyeponea vita kwa muujiza wa Mungu.
Desturi hii ya majina ya watoto wa kiume imeenea kote ulimwenguni ambapo kuna majina mengi yaliyo na maana ya nyakati kam wakati wa vita, njaa, shjrehe, makumbusho au tukio amabalo watu hupenda kukumbuka kwa kuwapa watoto majina. Kuna  majina kadhaa amabyo ni mashuhuri sana ulimwenguni ;Noah, Liam, Mason, Jacob, William, Ethan, Michael, Alexander, James, Daniel na mengine.

MAANA MAJINA TUKIZINGATIA HERUFI YA JINA LA KWANZA (KIUME)

HERUFI  A

Watoto wenye jina linaloanza kwa herufi hii hupenda mambo makubwa,hujiamini sana na huwa na uwezo wa kutimiza malengo yao. Ni watoto wenye tahadhari,wachangamfu na hupenda matukio.
Kwa kawaida hupenda kuheshimiwa,hupenda mamlaka,na ana kiburi,watoto wapenda hasira.Kidesturi herufi hii huwakilisha nyota ya punda.

HERUFI  B

Mwenye jina linaloanziana na herufi hii ni watoto wakarimu,waaminifu na hupenda kazi sana. Ni wajasiri, shujaa na wakatili katika vita au popote pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.Herufi hii huwakilisha nyota yangombe.

HERUFI  C

Mwenye jina linaloanzia na herufi hii ni motto wa kubadilikana,ni washindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda.Ni watu wabunifu na wanapenda mawasiliano,herufi hii huwakilisha nyota ya mapacha.

HERUFI  D

Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni anayependa usawa,biashara ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi.Ni wajeuri na wenye msimamo. Herufi hii huwakilisha nyota ya kaa.

HERUFI  E

Mwenye jina linaloanza na herufi ni mtu mwenye roho nzuri,mwenye mapenzi na huruma,mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Ubaya  wake ni mtu asiyetegemewa na ni kigeugeu.Herufi hii huwakilishwa na nyota ya samba.

HERUFI  F

Mwenye jina linaloanza na herufi hii n mtu mwenye mapenzi,huruma,roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu,ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.Herufi hii huwakilisha nyota ya mashuke.

HERUFI  G

Mwenye jina linaloanzia na herufi hii ni mtu mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho,ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. Ni mtu mwenye hisia kali,msomi,mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri kutoka kwa watu.Herufi hii huwakilisha nyota ya mizani.

HERUFI  H

Mwemye jina linaloanzia na herufi hii ni mtoto mwenye ubunifu na nguvu katika biashara,hupata faida kubwa katika anayopenda kutokana na bidii, ni mwenye mawazo mengi,mchoyo na mbinafsi.Herufi hii huwakilisha nge.

HERUFI  I

Mwenye jina   inayoanzia na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda sharia,ana huruma na utu mzuri.Wakati mwingi ni mtoto mwenye kujiamini sana na mwenye hasira za haraka. Herufi hii huwakilisha nyota yam shale.

HERUFI  J

Mwenye jina inayoanzia na herufi hii ni mtoto mwenye matamanio,mkweli,mkarimu na mwerevu.Huwa asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa,wakati mwingine anakuwa ni mtoto mvivu na anayekosa mwelekeo. Herufi hii huwakilisha nyota ya mbuzi.

HERUFI  K

Mwenye jina linaloanza ha herufi hii ni mtoto mjeuri,mwenye msimamo thabiti,mpenda umashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu, ana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana,ni mtoto asiyeridhika. Herufi hii huwakilisha nyota ya ndoo.

HERUFI  L

Mwenye jina linaloanza ha herufi hii ni mtoto wa vitendo,mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha,hupatwa na misiba mara kwa mara.Herufi hii huwakilisha nyota ya samaki.

HERUFI  M

Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kujiamini sana,mchapakazi na hupata mafanikio,ni mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda.

HERUFI   N

Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mbunifu, mwenye hisia kali,hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya ngombe.

HERUFI  O

Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye subira,mvumilivu,na mwenye bidii ya kusoma.Ni mtoto mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.Herufi hii huwakilisha nyota ya mapacha.

HERUFI  P

Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye uwezo wa kuamuru na ana hekima kubwa.Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu. Herufi hii huwakilisha nyota ya kaa.

HERUFI  Q

Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtotto mwenye kupenda mambo ya asili,ni watu wasioelezeka,wako na uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya samba.

HERUFI  R

Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mtulivu,mwenye huruma lakini mwenye hasira za haraka.Muda mwingi yeye ni mpenda amani. Herufi hii huwakilisha nyota ya mashuke.

HERUFI  S

Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye mvuto kali wa kuleta utajiri,ni mtoto mwenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa. Herufi hii huwakilisha nyota ya mizani.

HERUFI  T

Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda ushauri wa kiroho,anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu, ni watoto wenye hisia kali na wepesi sana kushawishika.Herufi hii huwakilisha nyota ya nge.

HERUFI  U

Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye bahati kwa ujumla,anapenda uhuru katika mapenzi,ni mbinafsi,mwenye tama na anayekosa maamuzi. Herufi hii huwakilisha nyota yam shale.

HERUFI  V

Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mchapakazi,mwenye bidii asiye choka lakini ni watu wasiotabirika. Herufi hii huwakilisha nyota ya mbuzi.

HERUFI  W

Mwemye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye mawazo sana,mchangamfu sana,mwenye uwezo wa kutambua watu wabaya na wema, ni wenye tama na hufanya mambo hatari sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya ndoo.

HERUFI  X

Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto asiyependa kuwekewa vizuizi hasa katika anasa na ni rahisi kwake kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda.

HERUFI  Y

Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mpenda uhuru na hapendi kupingwa katika jambo lolote,ni watoto wanaokosa uamuzi na husababisha kupoteza bahati katika maisha. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda.

HERUFI  Z

Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda matumaini na amani,ni wenye msimamo mkali japo ni wenye kukubali ushauri . Herufi hii huwakiisha nyota ya ngombe.

No comments:

Post a Comment