Upo kwenye mahusiano na unataka iwe hivyo kwa njia hio .Lakini baada ya ndoa , mambo yanaanza kwenda tofauti , na kabla hujafahamu , unavunjika moyo .
Ni mambo yanayotokea kila siku. Watu wanaacha kila mara . kwa hio utafanyaje ili kuepuka kuwa katika kundi la watu kama hawa? Kwa kuanzia Epuka makosa haya ya kawaida.
Kosa la kwanza.
1.Kuanzisha Mahusiano Kwa Sababu Unahisi Unahitaji , Sio Kwa Sababu Unataka Mahusiano.
Watu wengi huwa wanachanganya katika kuhitaji na kutaka. Unapohitaji kitu fulani , unaweza kuwa unahitaji kwa sababu uko mwenyewe na unaogopa kwa kuwa uko mwenyewe, kwa ajili ya usalama wa pesa, au unakuwa huna uhakika wa kupata kitu kilicho bora
Unapotaka kitu fulani haijalishi kitu gani kitatokea, haijalishi ni ugumu gani utapitia , utabaki kushikilia kutaka hicho kitu . kwa hio huo ndio upendo.
Kosa kubwa na la kawaida sana ambalo linafanyika ni pale mtu anapokuwa anahitaji mtu wa kumkamilisha. Lakini ukumbuke kuwa hakuna mtu atakayeweza kukukamilisha isipokuwa ni wewe peke yako unaweza kujikamilisha. Kitu kimoja cha muhimu cha kuwa nacho kwenye kutunza mahusiano mazuri ni uwezo wako wa kuwa mwenyewe peke yako kwanza.
Kosa la pili
2.Rebounding
Wachunguzi waligundua kuwa rebounding inatokea kwa sababu ya ubongo unatamani kupata mtu ambaye ni sawa na jinsi ubongo unavyofikiria .inawezekana hata wewe uko hivyo na ukakutana na mwingine ambaye anatamani anachokitamani.
Unahisi kwamba unahitaji mtu wa kuziba mahali ambapo pako wazi huenda kuna mtu alikaa halafu akaondoka. Na mahli hapo bado ni wazi . kwa hio unategemea mtu fulani kuziba pengo hilo. Jaribu kuliziba wewe mwenyewe, ingawa ni ngumu katika hatua hio .
lakini ni muhimu kufanya hivyo. Kwa sababu ya kuepuka kupata mtu ambaye naye anatafuta mtu wa kuziba pengo. Mwenza mwenye kuleta matatizo zaidi ya uliokuwa nayo.
Wakati mwingine utakapoona vigumu kuachilia yaliopita na kuwa na mashaka kama kuwa labda ungeweza kurudi kwa Ex wako. Kumbuka hii theory. Usifanye makosa kama hayo tena . Utakuwa ni mwenye furaha katika maisha yako na katika mahusiano yako kama utafanya nguvu ya kuvunja hii mifano ya kawaida.
Umependa hii makala? Washirikishe wengi wajifunze.
No comments:
Post a Comment