Kuna negatives nyingi Ulimwenguni. Tunahitaji kujilinda wenyewe kwa kujinenea maneno mazuri
Wengi wetu tunajilazimisha kuishi katika maisha ya ukamilifu ili kujisikia vizuri. Niko hapa kukuambia kuwa Wewe ni mtu pekee unayeweza kujielezea na kuwa mtu mwenye kustahili.
Kama unataka kujua jinsi ya kujijengea heshima yako. Anza kujinenea mwenyewe maneno mazuri kila siku.
1.”Iam good enough”
Hata kama huamini leo, lakini utakuwa mtu bora kwa kadri unavyoendelea kujinenea maneo haya, utaanza kuamini ndani yako kwa kuwa yatasikika ndani ya ubongo wako.
2.Ni wa thamani
Ndivyo ulivyo , una thamani kubwa katika maisha yako, una thamani isiyoelezewa na mtu . kama watu wakikutendea baya . hilo sio tatizo lako. watabaki ni watu wa ulimwenguni.
3.Ni mtu bora leo
Hii inaweza kuwa imeshikilia mlango wa mtu mwingine au kwa urahisi ni kufahamu uwepo wao. kama unajitahidi kuwa mtu bora leo kuliko jana. tayari wewe ni mshindi.
4.Usipoteze lengo.
Jisemee hivi. kila siku , rudia. unahitaji kukazania lengo lako. kazania mipango yako, haijalishi ni kubwa au dogo kwa siku . weka akili yako kwenye tuzo.
5.Jua litatoa mwanga tena, kama sio leo.
Utaweza kuwa na siku mbaya . lakini siku zingine utakuwa na siku nzuri au mbaya zaidi kuliko siku zingine. lakini nakuahidi hio ni kwa muda mfupi tu. yatapita, na jua litatoa mwanga tena.
6”.Iam strong”
Nguvu zipo ndani yako. unahitaji kuzitafuta na kuzivuta nje. utaweza kukabiliana na mambo ambayo ulifikiri hayawezekani.
7.”Siwezi kutawala wengine lakini naweza kuzitawala njia nzuri na kuwa na tabia njema kwa wengine”.
Kabiliana na hili.kuna watu wazuri na watu wabaya kila mahali. huwezi kutawala tabia za watu ila unaweza kuitawala tabia yako, na hapo utaweza kuishi nao kwa amani.
8”.Iam beautiful”
Wewe ni mzuri ndani na nje, Unalo kusudi na unayo maana ya maisha katika kuishi na unahitaji kukumbatia huo uzuri. unahitaji kufahamu uzuri wako kabla mwingine kufahamu hilo.
9.Ninao ufahamu wangu
Wengi tunaweza kutumia ufahamu zaidi . kwa siku za leo, lakini wewe utakuwa mwenye ufahamu zaidi kila mahali, unapotembea hutajiumiza au kuumizwa na mtu yeyote. Huu ni ufunguo wa kuelewa mazingira pamoja na wale waliokuzunguka. itakusaidia kushughulikia mambo ya Ulimwengu huu.
10.Ninastahili
Unastahili kuwa na furaha, upendo na kupata ukweli kutoka kwa wale uliochagua kuwa nao katika maisha yako. usitulie kwa kitu kidogo. endelea kujinenea kila siku. Itakuwa ni kawaida yako.
11.Sijavunjika
Hujawahi, hutawahi kuvunjika kama akili yako inamaendeleo ya kutosha ya ndani yako. utakuwa na misingi yako , na utafahamu kuwa wewe ni nani.
12.Yaliopita ni kianzio changu cha hiki ninachokifanya na ninajijenga upya maisha yangu.
Yaliopita yamepita, hayatakurudisha nyuma, yamekuwa ni mafunzo katika maisha yako. yaliopita hayakuelezei kitu. lakini yanakuonyesha ni kitu gani unakitaka na ambacho hukitaki. Yaliopita yameokoa kusudi lako katika safari yako. imekusaidia kuwa mtu ambaye ulitaka kuwa.
Tunahitaji kuachana na negatives katika fikra zetu . na pia tunahitaji kufahamu kuwa hatutakiwi kuwa watu wagumu wa kuelewa.
Haya ni maisha yako. ni mwandishi wa historia yako. weka maisha yako vizuri, usiweke maisha yako mikononi mwa mtu mwingine. unastahili kupata kilicho bora.
Kuwa bora kwa ajili yako , jitambue. jinenea mwenyewe mambo haya mazuri kila siku na utagundua tofauti sehemu zote kiakili na kimwili. Nakuhakikishia utaona tofauti.
kama umependa makala hii
No comments:
Post a Comment