Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Monday, August 21, 2017

MASHAIRI YA MAPENZI HADI RAHA

Mashairi huwa yana maana mengi kulingana ya mtu anvyoelewa mauthui yake. Mashairi ya mapenzi huzingatia mahaba.
Mashairi ni fasihi ambayo inaweza tumika kuonyesha mapenzi kwa mtu ama kumtongoza mtu unayemtamani. Mashairi ya mapenzi san asana huzingatia ama huongelea hisia za mtu kwa wapendanao.
Mashairi Ya Mapenzi

Mpenzi Wangu

Mpenzi tumepitia mambo mengi duniani,
Siku, miezi, miaka imepita,
Lakini bado nina tabasamu,
Ya kwamba naweza bado kukuita mpenzi wangu,
Tulipopatana Maisha yangu hayakuwa na hamu,
Ukaja ukanipa raha na kwa roho yangu,
Ulinichukuwa nilivyokuwa,
Kwa hali na mali, ulizingatia mapenzi,

Mvutano umekuwa kati ya marafiki,
Familia zetu hawakupenda mimi na wewe,
Lakini waambie kwamba mimi ndiye wako mpenzi,
Kwani letu limewekewa baraka na mwenyezi,

Sikujua nitapenda tena,
Mwanzoni niliyempenda alinivunja roho,
Akasema sina kitu akamwendea Joho,
Akanivunja hisia na mawazo,
Akaniwacha kama mtu asiye na uwezo,
Lakini wewe ukaja kama baraka mwenzio,
Na kunionyesha naweza sahau ule wa mwanzo,

Shida zangu za mbeleni,
Ukaja ukazifunika sakafuni ndani,
Ukanipa mwelekeo mpya wa Maisha,
Ukanionyesha naweza penda,
Na kwamba mapenzi yaweza dumu,

Napokutazama kila siku,
Namwomba Rabana akakuongezee maishani siku,
Kwa vile ulinipenda kwa dhati,
Nami nakuahidi kukupenda kama mfuko na shati,
Mapenzi yetu yawe ya kudumu,
Niite baba wa watoto wako,
Nami nikuite mama wa watoto wangu.

Wewe Ndiwe

Kwa Maisha yangu wewe ndiye nahitaji,
Macho yangu hayatasita kutazama uso wako unaopendeza na kung’aa
Wanipa tumaini maishani kwa tabasamu lako,
Pambaja lako lanipa utulivu wa maumivu yote moyoni,
Wewe ndiwe wanipa raha maishani

Moyo wangu nimekupa bila kusita,
Maisha yangu yote nakupa wewe mpenzi,
Wakati wangu, tuwe nawe siku za usoni,
Chochote utakacho nitafanya,
Kwani wewe ndiwe wanipa raha maishani,

Umekuwa kando yangu kwa shida na raha,
Umenisamehe nilipokukosea,
Ulionyesha njia kila nilipopotoka,
Hakuna kitu chocho duniani kinachoweza kulipa,
Yote ambayo umenitendea,
Nakuenzi mpenzi, wewe ndiwe..

Ninapokumbuka yote mpenzi, machozi yanitoka,
Nashukuru Mola kwa kukupata wewe,
Una ukarimu, uzuri wa matendo na aliye na mwelekeo mzuri,
Nakupenda mpenzi, malaika wangu,
Wewe ndiwe..

Maisha ni Kupendana

Babu alinifunza mara kwa mara,
“Mtunze mke wako naye akutunze,
Mwanamke ni kiumbe apendaye mapenzi,
Mpe kiasi cha haja”

Nilipokuona nilijua ni wewe nahitaji,
Kama mwenye kiu ya maji,
Nikaapa hata mbele ya jaji,
Kwamba nitakuwa nawe milele tukavishwa taji,
Tukafunga ndoa na kubebwa na bajaji,

Tulisema kwa hali na mali,
Tutapendana kwa kila hali,
Ukasema ndio sio la,
Tukaahidi hatutakuwa na mbadala,
Mimi na wewe atubariki Jalala,

Mwaka umepita, na Mola katubariki,
Mwana mrembo kafanana na wewe
Kila siku tabasamu lake lanikumbusha wewe,
Wewe mpenzi uliyetuacha,
Kifo chako bado chanipa kiwewe,
Madaktari walijaribu wawezalo,
Lakini Mola kakupenda kutuliko.

Macho yake, namwita Baraka,
Yanikumbusha penzi lako,
Tabasamu lako, busu lako mpenzi wangu,
Nilipenda tuzeeke pamoja,
Lakini Maisha mviringo,

Picha yako machoni,
Nikikumbuka tulivyo panga kimaisha,
Mipango yetu ya kulea watoto wetu pamoja,
Kama mama na mie kama baba,

Nakuahidi mpenzi wangu,
Mwana wetu atakuwa na malezi mufti,
Atakuwa mja Mungu na mwenye busara,
Kama mamake alivyokuwa,
Nitakupenda daima mpenzi wangu,
Tuliagana ni mimi na wewe maishani,
Maisha ni kupendana,
Yangu mie nawe yamekamatana.

Siweza kukuambia 

No comments:

Post a Comment