Pamoja na matatizo, furaha, kutoelewana kwa kila mmoja, lazima ufikirie kuhusu viapo vyenu mlivyoahidi kwa pamoja, Vina maana gani .kwa miaka yote ijayo? Mnaheshimu hivyo viapo? Vinaonyesha maana gani kila mnapotazamana kwenye macho na kukumbuka jinsi mlivyotamka kuwa utafanya hivyo?
Jibu fupi ni Ndio.Pia ni Hapana
Watu wanapoongelea kuhusu kuoa hufunika baadhi ya mambo. Lakini huangalia ni nani wa kualikwa, ni nguo gani za kuvaa, tutakula kitu gani, na tutasherehekea wapi.
Tunajifunza mambo mengi , hasa ambayo hatuyapendi yatokee kwetu kwa kupitia ndoa zingine zilizotangulia.
Wengi huishia katika ahadi ya nitafanya hivyo , kuwa nae katika shida na raha. Lakini tunasahau kuwa ndoa ni ahadi ya ngono, ndoa pia ina ahadi ya upendo, na kujaribu kuishi na mwenzako kwa usahihi.
Wakati mwingine naona kama hizi ahadi hazifanyiwi kazi ipasavyo. Nafahamu mtu kusema nitafanya hivyo kwa upendo, kubadilisha hisia na kuendelea hivyo. Lakini labda ningesema hapana kufanya sex na yeye maisha yangu yote. kuwa na hamu na kutokuwa na hamu. Kumwambia yeye aniahidi hivyo kuwa hatahitaji sex kila siku? nisingeweza kuweka ahadi ya kubaki kama nilivyo.
Ukweli ni kwamba , hakuna njia ambayo itakuonyesha kuwa mahusiano yatakuwa mazuri siku zote. Hasa kulingana na jinsi gani ulivyojiandaa, una matarajio gani na mahitaji yako ni yapi uliyonayo. Lakini bado utasema nitakupenda na kukufanya uwe na furaha siku zote za maisha yako. Lakini kitu gani hutokea kati yenu? Kama ulisema hakuna kitakachotutenganisha.
Kwa upande wangu naona hakuna ahadi kama hio inayoweza kutunzwa. Kwa nini? Kwa sababu sisi ni wanadamu tunaishi kwenye Dunia hii .
Wakati mwingine tunapendana na wakati mwingine hatupendani, tunagombana na kushindwa kuelewana.
Wakati mwingine utamfurahisha lakini kuna wakati utatamani kama usingekuwa naye.
Wakati mwingine inaweza kutokea kila siku; kwenye familia, kazini, nia zetu, uvumilivu, wema, na kujali.Naona kama hizi ni nyongeza ya viapo, kuwa ni vizuri. Kuna viapo ambavyo tunafanya kwa kufahamu au kutofahamu.
1.Naapa kwa kutojua
Yaani kuingia kwenye mahusiano bila kujua kama kuna muhimu au hakuna umuhimu. Haijalishi kuna ugumu gani, haijalishi tunapendana kwa kiasi gani, haijalishi ujuzi tulionao, tumepanga kuwa pamoja , tutakuwa tukijaribu siku kwa siku kurekebishana. Nitakupa mapenzi yote niliyonayo, na jinsi ulivyo nakupenda. Na kuishi wakati ulipo.
2.Naapa kuwa na furaha na Huzuni.
Kwa sababu vitu hivi vyote vipo, hata kama utakataa lakini vipo. Wakati mwingine ukijaribu kumwangalia mwenza wako hutaweza kuona ule upendo ambao ulikuwepo . unaweza kuona hasira, huzuni, wasiwasi, woga. Utapata wapi ujasiri. Ukweli Sijui . lakini kama ukirudi kwenye huruma ya kweli hapo utaweza kuona ukweli. Kwa sababu huruma ni kitu kinachoshikilia upendo na maumivu pamoja kwa wakati mmoja.
3.Naapa kuwa nitaudhiwa na kusumbuliwa
4.Naapa kujenga nyumba mahali ambapo upendo unatakiwa kuishi.
Inabidi kuelewa upendo wa kweli, upendo wa ndani, kwamba hauji kwa kuunganishwa na mtu mwingine, hauhusiani na hisia, sio ahadi ya kukaa, ni nia ya kuwa mkweli, mwema. Sio kufikiria hivyo. Upendo wa kweli ni wewe kujipenda kwanza na hapo ndipo utaweza kumpenda mwingine kama unavyojipenda wewe.
Huwezi kumpenfda mtu kama hujipendi wewe mwenyewe. Kumpenda Mungu ni kujipenda wewe, kwa kufanya matendo mazuri ya Mungu. Kujali, kujiheshimu. Kujikubali.
5.Naapa kuachilia.
Ni kweli tunaapa kuwa tutafanya hivyo.Hakuna kitu ambacho hakina mwisho. Kama kitu kimekuwa kigumu kwako Achilia. Kwa njia moja au nyingine. Kuna mahusiano mengine ni ya bahati mbaya. Tukubali tusikubali. Kutokana na Safari yetu hapa duniani. Tukubali kuwa tunapita kwenye milima na mabonde. Watu wanakua na kubadilika. Zipo nyakati, lazima tukubali. Kuna kukosea na kusameheana. Kuna kupenda na kuchukia kupo. Hisia zinabadilika. Lakini bado unaweza kuwa na mtu hata kama hauna hisia nae. Hakuna uamuzi mwingine maana ulishasema Nitafanya hivyo.
No comments:
Post a Comment