Upo usemi unasema kuwa kama unampenda mwache aende. Kwa nini imesemwa hivyo? kwa nini tunafuata usemi huo, tunajiwekea ukuta, tunatunza kwenye akili zetu? kweli, kuna kitu chenye nguvu katika kuwa mtu huru. kuwa mwanadamu usiyefungwa na sheria au mipango iliyopo.
Lakini , je ni kweli tunahitaji kupata kibali kama hicho?
Nafikiri ni muhimu kufikiria upya jambo hilo. Na naenda kinyume na kusema kuwa mtu unayempenda kweli ni vizuri kumwachilia aende. Usemi huo Sio mzuri. kwa wewe ambaye unaona unafaa samahani kidogo.
Kama kweli unampenda mtu, kama moyo wako unamkubali huyo mtu, Kwa nini usemi huo ukufanye umwache ? Kwa nini umwambie kwa heri na hali unampenda kwa dhati , na ukae naye mbali na akakae mikononi mwa mtu mwingine?
Kwa nini usijitahidi kujirekebisha katika sehemu ambayo unaona inaleta shida katika mahusiano yako ? Kwa sababu usahihi uko ndani yako, kosa liko ndani yako sio kwa mwingine . kwa nini basi usianze kujichunguza mapema kabla ya kuharibika kitu?
Labda kuna ukweli katika wazo hili kuwa upendo wa kweli huwa unarudi. kama utamwachilia aende. Naamini katika ukweli wa sentensi, kwa kufahamu kwamba kama watu walitakiwa kuwa pamoja watatafuta njia kila mmoja ili kutimiza ahadi hio. Lakini ina maana kwamba kumwacha mtu umpendae awe mbali na wewe, ili usonge mbele? Ina maana kuwa mwanaume huyo aliyeonyesha upendo wa kushangaza ,alikuwa anaigiza hisia hizo, hakuwa na ukweli ndani yake. Na kuwe na tumaini kwamba ipo siku tutakuwa pamoja tena?
Unapokuwa Unampenda mtu Usimwache aende.mwambie, kuwa naye, mjali.
Kama unampenda mtu hutaweza kumwacha wakati mambo yanapokuwa magumu. hutawasukumia mbali na kuacha kuwa karibu yao . hutakuwa na mashaka katika mahusiano yako. mwambie ni kitu gani anatazama kwa mtu mwingine.
Usiishi kwa kutarajia kuwa ipo siku atarudi na mtakuwa pamoja tena.
kwa sababu upendo haufanyi kazi ya aina hio.
Itakuwaje kama mtu uliyemuacha hakuwa anatafuta mtu yeyote zaidi yako, lakini imekuwa hivyo, kwa sababu hana maamuzi mengine? vipi kama utamwambia aende , na yeye akaondoka kweli na kusonga mbele . utakuwa mwenye furaha kweli? kwa sababu ulitegemea kuwa atarudi na hakurudi kwako tena.
Vipi kama utapoteza mahusiano yako mazuri, kwa sababu tu ya kuogopa kuchukua nafasi?
Kama unampenda mtu mwambie ukweli. ni rahisi, ni kitu tunachoweza kufanya. lakini ni kwa jinsi gani utaweza kumpata mtu unayempenda hata nyakati ngumu? hata wakati maisha yanapokuwa magumu? hata mnapojikuta kuumizana kila mtu kihisia?
Unao ujasiri wa kupenda? au wewe ni mrahisi wa kuachilia mtu aende hata kwa kosa linalorekebishika?
Kama Unampenda hutaweza kumwacha, ni rahisi kama hivyo.
Mtakuwa pamoja katika kila tatizo, hutakuwa muigizaji katika kupenda, mtapata maumivu pamoja na kupata furaha pamoja. Inaaminika kwamba upendo wako una nguvu.uko imara. Muungano wenu ni wa kweli. Kitu ambacho hutaweza kuona kama usemi unaosema kama ilitakiwa muwe pamoja mnaweza kuachana na kurudiana tena. Badala yake Utafanyia kazi kila kitu kwenye mahusiano yako sasa hivi.
Kumpenda mtu Sio kujaribu kumwacha Aende.
Upendo upo, wakati uliopo. ni changamoto,ni kujifunza, ni kutafuta njia ya kufanikisha. Upendo sio kumwacha mtu unayempenda aende kwa mtu mwingine. Ni kushikana pamoja na kupigania mlichokianzisha, kuepuka mambo mabaya ya Dunia hii. na kuwa katika umoja wenye nguvu.
No comments:
Post a Comment