Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Tuesday, August 22, 2017

SABABU ZA KAWAIDA KABISA AMBAZO ZINAHARIBU MAHUSIANO


Na utafanyaje Kurekebisha Haya.
Mahusiano sio jiwe kama watu walivyo sio mawe. Tunabadilika kila mara.Tunawezaje kushughulikia mabadiliko haya , ingawa tuna uwezo wa kutosha na sifa tunazo  lakini inatokea  tofauti kati ya moja kupona na lingine kutopona
Kama tuko active katika kufanyia kazi mahusiano yetu ,  kuwa na nafasi nzuri, kujifundisha maana ya mahusiano , kufurahia na kuweka muungano mzuri. Lakini tukiwa tegemezi kuhusu majukumu yetu muhimu — kama mahusiano ni box tunaloangalia kabla ya kwenda  lengo lingine— hii itaua mahusiano kwa muda mfupi.
Tunataka mahusiano yajawe na Mapenzi, upendo, ushirika, usalama na furaha. Kwa hio hapa kuna mambo yanaoua mahusiano yako na jinsi ya kupigana nayo.
1.Kuchochea hisia za kupigana mara nyingi
Hakuna mtu anayeingia kwenye mahusiano ili kumfanya mwingine awe na matatizo.Wengi wetu tunatofautiana pale tunapokutana na kazi za over time, kukosa muda wa pamoja.
Kutokuelewa kuwa kichocheo cha mara kwa mara ndio sababu.
Wengi wetu tunahitaji kujisikia kupendwa, kujiona kuwa tuko salama, kuwa team moja, . lakini tunapoona kuwa hakuna msaada huo , hakuna upendo , hakuna heshima, wala hakuna kukubalika, na kutaka  nafasi, hapo ndipo tunapata wasiwasi mkubwa.
Jinsi ya kushughulikia hili jambo ni kuelewa kitu gani kinasababisha mfarakano huu. Mara tutakapoelewa ni kukaa na kutatua tatizo hilo ili kuokoa  hali  ambayo ilikuwa inaharibu mahusiano yetu.
2.Kukata Tamaa.
Mahusiano ni watu wawili. Lakini wakati mwingine mmoja anapokuwa  amekata tamaa ya kufanyia kazi mambo  yaliopo ndani yake,  mzizi uliopo utaanza kukomaa na kukosa kufikia mahitaji yetu. Tunapohisi kutoshirikiana  kwa muda wa kutosha  na kuhisi mwenza hasikilizi , wakati kuna mambo yanahitaji kutatuliwa. Hapo ndipo tunapojiondoa kwenye ushirika na kushindwa kushughulikia hisia zetu .
Kuhamishia lawama kwa mwenza ni sawa na kumtupia kwenye mazombi.
Jifunze jinsi ya kuwasiliana  kwa kitu unachokitaka na na kuhitaji  bila ya  ya kulaumu upande mmoja. Acha kulalamika na unatakiwa kulenga  unachohitaji.
Badala ya kuanza kulalamika kuwa mwenza anakuja nyumbani kila siku kwa kuchelewa, badala yake mwambie kuwa unampenda na ungehitaji awepo mapema nyumbani na kupata muda wa kutosha kuwa pamoja.
Ni kutumia maneno ya busara ili kuyashusha yale mabaya chini.
3.Thamani tofauti na mahitaji tofauti.
Mambo yanayofanyika kwenye pesa, sex, watoto  ni kawaida?
Vitu hivi vyote bi kutokana na  tofauti ya thamani na mahitaji.
Changamoto kubwa wanandoa wanazokutana nazo mara nyingi ni katika  thamani zao  walizo nazo kutoka wakiwa wadogo.  Jinsi mtu alivyolelewa.
Kwenye pesa kwa mfano. Tunaweza tukawa tunatumia kiasi tu na kufurahia  tulichokipata,  lakini mwenza mwingine akawa anatumia zaidi kuliko familia  inavyotumia.
Kitu kizuri cha kufanya hapa ni kuwa timu moja. Watu  huanza kutowasikiliza wenza wao  na kusababisha kutoelewana. Ni bora kama mkikaa na kuongea jinsi ya kupanga matumizi kwa pamoja kuliko kuonyesha dharau  kutokana na kipato alichonacho mwenza mwingine.
Kitu kingine ni kutokana na tabia ya mtu jinsi alivyo. Kama ukimjua mtu tabia yake huwezi kusumbuka nae, kwa sababu  ndio alivyo. Huko kwao ndivyo walivyo. Kumbuka kuna tabia za makabila, na mila ,mbalimbali. Ni wachache ambao hubadilika  kutokana na mazingira , lakini kile kilivhopo ndani kwa mtu  huwezi kukibadilisha ila ni Mungu tu ndiye anaweza kufanya hivyo.
4.Hatujielewi wenyewe.
Mawasiliano ni kitu kikubwa  kwenye aina zote za mawasiliano.
Lakini watu hutazama mawasiliano kwa njia tofauti. Hufikiria tatizo ni la mwenza wake  badala ya kujiangalia kwanza yeye.
Hio ndio sababu unampa mwenza wako sehemu kubwa ya kufanyia kazi kuliko wewe.
Kama tunaogopa kutelekezwa, na kweli tunajikuta kutelekezwa ndani ya wenza wetu. Kama mwenza hakutendei utakavyo , ni kwa sababu wewe hutendi hivyo kwake.
Kitu kizuri cha kufanya ni kujitambua sisi wenyewe.
Kama utaanza kuona tatizo , anza kulitatua mapema wewe mwenyewe, kwa sababu mwenza wako hawezi kuona ndani unawaza nini. Wewe ndio solution.
5.Makuzi tofauti
Mahusiano hubadilika mara nyingi, unaweza ukaamka tofauti ukakuta hamna ushirika hata kidogo, unaona kama safari iko tofauti. Mmepata makuzi tofauti na sasa  mnaenda mwelekeo tofauti.
Kwa sababu mnakua na mahusiano yenu pia yanakua. Wakati mwingine ni mazuri na wakati mwingine sio. Mtaweza kuwa pamoja tu mnapofanya maamuzi kwa pamoja , na kujiona kuwa mko kamili, sio watu tofauti,   kila mahitaji yapo wazi . hapo ndio mtaweka safari yenu iwe rahisi.
Mahusiano ni kitu chochote lakini ni kama  tuli. Wanandoa wenye nguvu wanaelewa hili.  Yanakuwa imara kwa kutengenezwa.  Sio swali la kama ninge, lakini ni wakati  changamoto zikiwepo , kitu gani cha kufanya , hicho ndicho kinaleta tofauti.

No comments:

Post a Comment