WANAWAKE wengi watakiri kuwa mavuzi ni kero hasa katika kudumisha usafi au kuonekana nadhifu wakati wa mahaba.
Sababu hii imewapelekea wengi kutafuta mbinu na bidhaa mbalimbali kuondoa nywele hizi na kuhakikisha kuwa sehemu hii inaoenekana wazi na nyepesi vilivyo kwa kunyoa kwa mashine, krimu au hata nyembe huku mabinti wengine wakiamua kuvumilia uchungu unaoambatana na utaratibu wa kutumia mchanganyiko maalum wa nta (waxing), mtindo maarufu siku hizi hasa kutokana na sifa yake ya kuacha sehemu iliyonyolewa ikiwa nyororo na laini kwa muda mrefu.
Aidha kampuni zinazotengeneza bidhaa hizi zimekuwa na kibarua cha kutoa bidhaa mpya kila kuchao, nia ikiwa kuvutia soko la wanawake wanaotaka sehemu hiyo kusalia nyororo kama ya mtoto mchanga.
Lakini huku majarida ya wanawake yakiendelea kuchapisha makala yanayopiga vita nywele hizi, maelfu ya wanawake katika sehemu zingine ulimwenguni wanatafuta mbinu za kuhifadhi vichaka hivi. Korea Kusini ni mojawapo ya nchi ambapo idadi ya wanawake wanaofanyiwa upasuaji kuongeza au kubandikwa nywele hizi inazidi kuongezeka kila kuchao.
Kulingana na makala yaliyochapishwa mwezi uliopita na Refinery29, mojawapo ya majarida ya masuala ya kimitindo na mahusiano nchini humo, asilimia 10 ya wanawake katika taifa hilo wanakabiliana na upungufu wa mavuzi hasa ya kinenani, hali inayofahamika kama “pubic atrichosis,” suala ambalo limewakosesha wengi usingizi.
Mvuto
Hii ni hasa ikizingatiwa kuwa utamaduni nchini humo unahusisha nywele hizi na uwezo mkubwa wa kuzaa na kudumisha mvuto wakati wa mahaba. Pia inasemekana kuwa wanaume wengi nchini humo wanaamini kuwa ni bahati mbaya kushiriki ngono na mwanamke asiye na mavuzi, suala ambalo limepelekea mabinti wengi kukimbilia utaratibu huu ili kujiongezea sifa za kike.
Inasemekana kuwa asilimia 74 ya wanawake nchini humo wamefanyiwa utaratibu huu, huku idadi ya wanawake wanaofanyiwa upasuaji kuongezewa au kubandikwa mavuzi ikiongezeka kwa asilimia 160. Hii ni licha ya utaratibu huo kugharimu dola 2,000 sawa na Sh180, 000.
Ni mtazamo ambao hata hivyo unaotofautiana vikali na utafiti uliofanywa miaka mitatu iliyopita nchini Amerika kubaini hisia za wanawake kuhusu nywele hizi.
Udadisi huo uliofanywa na Dkt Debby Herbenick, mtafiti wa kisayansi katika Chuo Kikuu cha Indiana na mwalimu wa afya ya kijinsia katika taasisi ya Kinsey nchini Amerika, ulionyesha kuwa wanawake wengi nchini humo wanaamini kuwa kuondolewa kwa nywele hizi kunaimarisha ashiki.

Hata hivyo suala la kuwepo au kutokuwepo kwa mavuzi halijazua mdahalo nchini Korea Kusini au Amerika pekee bali hata hapa nchini ambapo watu wana hisia tofauti kuhusu mavuzi.
Kuamsha ashiki
Kulingana na Charles, mwanamke aliyeotesha nywele hizi huamsha nyege zaidi akilinganishwa na yule aliyezinyoa kabisa.
Kulingana na Charles, mwanamke aliyeotesha nywele hizi huamsha nyege zaidi akilinganishwa na yule aliyezinyoa kabisa.
“Wakati wa mahaba, nywele hizi zitakupa hisia kuwa mwenzako ni mwanamke kamili, tofauti na binti aliyenyooka kabisa katika sehemu hii,” asema.
Lakini kulingana na Vincent, mhudumu katika duka moja la jumla jijini Nairobi, hakuna raha inayotokana na mgusano wa nywele hizo wakati wa mahaba. Anasema kuwa mkwaruzo huo huhusishwa na jinsia ya kiume kumaanisha kuwa mwanamke anapaswa kuwa laini vilivyo. Kulingana naye nywele hizo ni ishara ya uchafu na kuwa mwanamke huyo hajishughulikii vizuri.
Japo hakubaliani na sehemu hiyo kufanana na kichaka, James, mchuuzi wa bidhaa za rejareja jijini anasema kuwa binti anaponyoa hapaswi kuziondoa zote.
Japo hakubaliani na sehemu hiyo kufanana na kichaka, James, mchuuzi wa bidhaa za rejareja jijini anasema kuwa binti anaponyoa hapaswi kuziondoa zote.
“Badala ya kunyoa kabisa, zipunguze kuhakikisha kuwa sehemu hiyo haikwaruzi wakati wa mahaba na wakati huo huo zile hisia za mapenzi zinadumishwa,” aeleza.Jecinter, mhudumu wa saluni moja viungani mwa jiji la Nairobi, asema kuwa nywele hizo ni kero kwani husababisha changamoto inapowadia wakati wa kudumisha usafi.
“Ni sababu ambayo huenda imepelekea idadi ya wanawake wanaotembelea saluni yetu kufanyiwa 'waxing’ kuongezeka,” aeleza.
Lakini katika makala yake 'End to War on Pubic Hair’, Dkt Emily Gibson wa Chuo Kikuu cha Western Washington, nchini Amerika anatoa wito kusitisha vita dhidi ya nywele hizi.
Lakini katika makala yake 'End to War on Pubic Hair’, Dkt Emily Gibson wa Chuo Kikuu cha Western Washington, nchini Amerika anatoa wito kusitisha vita dhidi ya nywele hizi.
Kulingana na mtaalamu huyu, kasumba ya kulainisha eneo hili imesababishwa na nadharia zinazohusisha urembo na mavazi ya kuogelea kama vile 'bikini’, mitindo inayomhitaji mwanamke kuwa nyororo katika sehemu hii kumaanisha kuwa nywele hizi hazifai.
Anasema kuwa tafiti kadha za kimatibabu zinaashiria kuwa nywele hizo kamwe haziathiri usafi wala afya ya sehemu hii, na badala yake husaidia dhidi ya mikwaruzo inayosababisha majeraha.
Anasema kuwa tafiti kadha za kimatibabu zinaashiria kuwa nywele hizo kamwe haziathiri usafi wala afya ya sehemu hii, na badala yake husaidia dhidi ya mikwaruzo inayosababisha majeraha.
Athari
Anasema kuwa kinena kilichonyolewa hukumbwa na hatari kubwa ya kupata maambukizi ya maradhi kama vile 'herpes’, kutokana na majeraha ambayo huwa wazi kwa virusi vinavyopatikana kwenye viungo vya uzazi.
Kulingana na Chris Hart, mshauri wa masuala ya mahusiano, suala la mahaba limewakanganya wengi kudhani kuwa nywele hizi huimarisha maisha haya.
Kulingana na Chris Hart, mshauri wa masuala ya mahusiano, suala la mahaba limewakanganya wengi kudhani kuwa nywele hizi huimarisha maisha haya.
“Mahaba ni suala la kisaikolojia. Kuna watu wanaofurahia nywele hizi ilhali kuna wengine ambao hisia zao za mahaba huamshwa na mazingira mepesi, kumaanisha kuwa hakuna kiwango kamili cha jinsi sehemu hii inavyopaswa kuwa,” aeleza.
No comments:
Post a Comment