Wanaume wanapaswa kufahamu aina ya vyakula ambavyo si rafiki kwao katika kuongeza kiwango cha homoni ya kiume iitwayotestosterone inayochochea sifa ya mwanaume yaani kuwa na nguvu za kiume. Baadhi ya vyakula visivyofaa kuliwa na mwanaume aliyetaka kuwa na nguvu za kiume ni vile vyenye asili ya homoni ya kike iitwayo estrogen. Hivyo sio kila vyakula vinafaa kwa mwanaume eti ilimradi tu vyakula hivyo vinasaidia kujenga mwili au kujaza tumbo wakati mtu akiwa na njaa.
Vyakula visivyofaa kabisa kuliwa na mwanaume kutokana na vyakula hivyo kupunguza homoni ya testosterone ni hivi vifuatavyo:
Bia (Beer):
Sipendi kusema habari mbaya kwa wanywaji wa bia. Hata hivyo ni vema kusema ukweli kuhusu athari ya bia kwa wanaume. Bia imetengenezwa kwa humle (hops) ambayo kwa kiwango kikubwa inaleta hali ya homoni za kike kwa wanaume (highly estrogenic). Humle (Hops) ina kiasi cha 300,000 IU cha estrogen kwa kila gramu 100 za hops. Kabla ya mwaka 1487 bia ilikuwa ikitengenezwa kwa viambata (ingredients) ambazo zililenga kuifanya bia inaponywewa na mwanaume humfanya mwanaume awe na hali ya uanaume kweli kweli (more aggressive, horny, and socially dominant). Hata hivyo baadaye Kanisa liliingilia uzalishaji wa bia na kutaka bia itengenezwe kwa viambata ambavyo vitamfanya mwanaume awe mpole au mtaratibu na sio mtu wa maguvu na ubabe ( to make men more feminine and sensitive). Hapo ndipo likazaliwa wazo la kutengeneza bia kwa kutumia humle (hops). Siku hizi bia hutengenezwa kwa viambata vitatu, hops, maji na malt.
Soya (Soy):
Ina kiwango kikubwa cha Isoflavones ambayo ni kiuhalisia ni estrogen. Ulaji wa soya ni sawa na kula kidonge kimoja cha uzazi wa mpango (birth control pill). Kwa kuelewa zaidi madhara ya soya kwa wanaume soma hapahttp://www.anabolicmen.com/soy-and-testosterone/
Spearmint:
Hutumiwa zaidi kama kiambata kwenye chewing gums, candies, na breath freshener au kwenye majani ya chai (herbal tea). Spearmint pia in akiwango kikubwa cha estrogen.
Lima beans:
Yana homoni za kike (estrogen) iitwayo inositol ambayo hupunguza kiwango cha homoni ya kiume (testosterone) kwa wanaume.
Whole grains:
Ina gluten ambayo huongeza prolactin ambayo hupunguza kiasi cha testosterone.
Soda:
Unapenda kinywaji baridi yaani soda? Je unajua soda zimechangia sana tatizo la watu kuwa na unene au uzito uliopitiliza (obesity)? Tukiachana na suala la obesity hebu tuongelee kuhusu namna soda zinavyopunguza homoni za kiume (testosterone). Chupa za plastiki ambazo hutumiwa na makampuni yanayotengeneza soda zimetengenezwa kwa phthalates ambayo hufanya plastiki ziweze kukunjwa katika umbo lolote (flexibility). Phthalates ni estrogen! Kawaida ili kuondoa phthalates kwenye chupa za plastiki makampuni yanapaswa kuziacha chupa hizo zikae kwa mwaka mmoja bila kuweka soda ndani yake. Hata hivyo makampuni hayo mara tu baada ya kutengeneza chupa hizo huweka soda ndani yake na kuzipeleka sokoni kwa walaji. Unajua nini kinatokea? Phthalates inaingia kwenye soda unayokunywa!!! Maana yake kama wewe ni mwanaume unaingiza homoni za kike mwilini mwako na matokeo yake unapunguza homoni za kiume!
Fast food:
Wewe ni mwanaume unapenda kula chakula kwenye Mgahawa wa Fast Food? Ngoja nikupe maneno kwa nini usiwe na upungufu wa nguvu za kiume wakati unafakamia vyakula Fast Food. Ukienda Fast Food unaagiza vyakula vya nyama iwe ni beef au kuku au burger na unaagiza na soda then unaona mambo safi, sio? Haya hiyo nyama au kuku imetokana na wanyama waliofugwa na kulishwa junk grains na kupewa madawa kama antibiotics na homoni za kukuzia wanyama ambavyo vyote hivyo vina asili ya homoni za kike (estrogen). Nyama hizo zinakaangwa au kupikwa kwa mafuta ya mimea kama vile soybean oil au sunflower oil ambayo yana estrogen! Baada ya hapo unashushia soda ambayo ina phthalates (homoni ya kike). Kwa ulaji huo unategemea kunako sita kwa sita uwe ‘super man’?!!
No comments:
Post a Comment