Wakati unapofika, kunakuwa na msukumo ambao humfanya msichana kutaka kuolewa, inawezekana ni umri , au ni matakwa ya mwili, inabidi msichana atulie hapo kabla hajaanza kutafuta mtu wa kuishi nae. sio tu mwanaume anaetafuta mtu wa kumuoa , na msichana nae pia hutafuta mtu wa kuolewa nae, labda utajiuliza kivipi.
Kwa sababu huendi tu kuolewa na mtu yeyote ni lazima kuwe na sifa uzitakazo.Sifa 23 za kijana anaestahili kuwa na wewe binti. hapa kuna mambo mengi , maana kuna wasichana ambao hujitangaza kuwa wapo tayari kuolewa , wako single n.k. unatakiwa ujifunze kwanza, na utambue kuwa kuna mtu utakuwa nae kwenye mahusiano , na kama wewe ulishawahi kuwa kwenye mahusiano kabla. lazima utambue kuwa ipo nafasi kubwa ya kuingia tena kwenye mahusiano mengine.
Kama unahitaji mahusiano ya kudumu , basi jifunze hivi vitu vifuatavyo kabla ya kuingia huko.
1.jiulize, shida yako ni nini?
Unatakiwa kutuiza akili yako na uwe na mtazamo sahihi , kwa sababu sio kuingia ndani ya mahusiano na mtu, na kama unataka mahusiano yawe ya kudumu, lazima ujifunze kwanza maana humo kuna zaidi ya kile unachotafuta wewe, lazima upate mtu anaekuthamini na wewe umthamini.
shida yako ni nini katika maisha na katika mahusiano? jitahidi kujua hivi vitu, utaepuka kumpenda mtu ambae sio wa mtazamo wako, na sio chaguo lako.
2.Jinsi ya kuwa huru.
Jifunze kuwa huru kwanza kabla ya kuingia kwenye ndoa, usitake mwanaume akukimbize katika maisha yako. kwa maana kama huwezi kujitunza , na kujisimamia wewe mwenyewe , utawezaje kuja kujisimamia mwenyewe na kumsimamia mumeo. au endapo utakuwa ni single huwezi kujiheshimu , utakuja kujiheshimu vipi ukiwa kwenye ndoa.
Jifunze kutokuwa tegemezi mapema kabla ya kuolewa, usije ukawa mzigo , na ukaanzisha matatizo mengine ambayo yana majibu wazi.
3.Jifunze jinsi ya kuwa na furaha.
Jifunze kuwa mtu wa furaha , furahia maisha yako kila siku iitwapo leo, uwe makini na yule mwenye hia , anayetafuta kuleta urahisi wa kukushambulia ili ukose furaha. jitahidi kushinda hivyo vitu. hapo sasa hata ukipata huyo mtu wa maisha yako , utakuwa ni mtu wa furaha siku zote , maana hutakubali mwenye hila akupotezee furaha yako.
4.hivyo huhitaji mtu.
kumpata mtu ambae ndio nusu yako , ya kwamba ni kweli huyo ndiye, inahitajika uwe ni mtu mtulivu sana .Naamini kuwa mahusiano yasingekuwa ni kiungo muhimu , ambacho kinakamilisha furaha ya maisha ya mtu, lakini basi isiwe ndio chombo cha kukufanya wewe upate furaha, nielewe vizuri hapa. huhitaji kusubiri mtu kwa ajili ya furaha yako. mweke mungu awe wa kwanza na mengine yafuate.
5.Jinsi ya kuwa wewe.
Tumefanya wote hayo,kujaribu kuwa pekee, kufikiri kuwa tunahitaji mtu wa kutufanya ili kuwa wewe ndiye. lakini huhitaji kubadilishwa na mtu au kuchukua mawazo ya mtu mwingine anavyotaka uwe, hapana. jifunze tu kuwa wewe. unahitaji kupendwa jinsi ulivyo. ndoa nzuri ni ile mtu kukupenda jinsi ulivyo, na kukuelewa ni aina gani ya mtu alienae.
6.Una nini cha kutoa.
Kuwa ndani ya ndoa sio tu kupata mtu sahihi kwako , je wewe ni sahihi?, lazima wewe nawe uwe na kitu cha kutoa, isiwe ni upande mmoja tu. jipime kama ni muda sahihi na mazingira sahihi au ni sehemu sahihi? au bado hujakamiika , unahitaji kwanza kukaa single ili ujiandae.
7.Ni wapi ulipokosea kabla.
inabidi ujiulize ni wapi ulikokosea ni wapi ulikojikwaa na kuanguka kwa mara ile ya kwanza ulipoingia kwenye mahusiano ya kawaida. kutokana na hayo makosa ya kawaida ulioyafanya ili usirudie makosa yale yale, lazima uwe na mtazamo tofauti. jifahamu kwanza wewe kabla hujaanza kumfahamu mtu mwingine. utapata furaha na mafanikio katika maisha yako.
Angalia jinsi gani unajipenda na uangalie tabia zako zikioje. ndipo utapata mtu sahihi .
No comments:
Post a Comment