Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Sunday, August 27, 2017

Wanaume handsome na wanawake warembo ni shida kwenye ndoa



Katika hali ya kawaida, kila mtu anapofikiria suala la kutafuta mpenzi kwa mwanaume lazima ataangalia msichana mrembo, mwenye muonekano mzuri huku suala la tabia likiwa halipewi umuhimu sana.

Hata kwa wanawake nao huwa wanaangalia wanaume ‘handsome’ ambao hata wakiwa wanatembea pamoja mtaani watavuta macho ya watu na kusifiwa.

Mimi sidhani kama wanaoangalia vigezo hivyo wanakosea hasa kama wanatafuta wapenzi na wachumba watakaotengeneza njia ya kuelekea kwenye ndoa.

Soma: Baadhi ya mambo yanayostawisha mahusiano na ndoa.

Naomba katika hili nieleweke kwamba, suala la muonekano wa mtu si kigezo tosha cha kumruhusu awe sehemu yako katika maisha ya ndoa. Wapo ambao ni ‘handsome’ na warembo lakini kiukweli hawastahili kupewa nafasi ya kuingia nao kwenye ndoa.

Tatizo la wanaume ‘handsome’

Utafiti nilioufanya ambao siyo rasmi unaonesha kwamba, ni wachache sana waliooa wanawake wazuri na wakaishi muda mrefu tena kwa furaha na amani.

Tunachotakiwa kujua katika hili ni kwamba, kuna baadhi ya wanaume ambao wanajijua wanapendwa sana na wanawake kutokana na muonekano wao. Kwamba ni warefu, ni watu wa mazoezi, wana sura nzuri na sifa nyinginezo.

Wenye sifa hizi ni chaguo la wanawake wengi. Kutokana na hilo sasa, wapo ambao wana kaulimbukeni f’lani ka’ kushindwa kutulia na mwanamke mmoja. Wanaweza kuingia kwenye ndoa lakini bado wakashawishika kutembea na wanawake wengine kwa kuahidiwa fedha na vitu vingine.

Mbaya zaidi, wanaume wa dizaini hii watakuwa wanajisahau kwamba nyumbani wana wake zao ambao wamewakabidhi mioyo yao na hawatarajii kusalitiwa.Hapo ndipo tatizo litakapoanzia na kumfanya hata mke mwenyewe ajute kuingia kwenye ndoa na mwanaume ‘handsome’. Sisemi kwamba wanaume ‘handsome’ wote ni tatizo kwenye ndoa, la hasha!

Wapo ambao ni watulivu, wasio viruka njia, kwamba wakipenda mmoja wamependa na hata wakishawishiwa na wengine, husimamia hisia zao na kuangalia heshima yao mbele ya jamii.
Tatizo ni kwamba, kuna ambao kwa muonekano huwezi kuwajua lakini ukishakubali ndoautashangaa usumbufu utakaopata.

Utaona mumeo ana marafiki wengi wa kike na ukimuuliza anasema ni marafiki tu. Mara utamuona anabadilisha magari na ukifuatilia utaambiwa ni magari ya mwanamke f’lani mwenye nazo. Hapo sasa ndipo utajua kwamba kumbe hujapenda peke yako, wapo wengine waliopenda na wakapewa nafasi kutokana na ushawishi wao.

Ndiyo maana nasema kuolewa na mwanaume ‘handsome’ tena ambaye ni limbukeni, utapata tabu sana. Utaambulia ile sifa tu ya kwamba umeolewa na mwanaume mzuri lakini kumbe hafai kuitwa mume!

Wasichana warembo nao!

Jaribu kuchunguza utabaini kuwa, asilimia kubwa ya wanaume wanaoteswa na ndoa zao,wameoa wasichana warembo lakini wasiojua thamani ya ndoa. Watakuwa wanaona sifa kuolewa lakini bado hawajui namna ya kuzitunza ndoa zao.

Soma: Adhabu kubwa kwa mpenzi msaliti

Watakuwa warahisi kushawishiwa na wanaume wakware na wakati mwingine wakiona wanatongozwa sana kutokana na uzuri wao, wanavimba vichwa.Wanakuwa si watulivu kwenye ndoa zao, siyo watiifu kwa waume zao na wanafanya hivyo wakiamini kwamba hata wakiachika, watapata wanaume wengine wa kuwaoa.

Ndiyo maana huwa nasema mara kwa mara kwamba, ukitaka kuoa ni lazima uangalie mwanamke mzuri unayemuona wewe. Lakini usiishie hapo, angalia na tabia zake ili usije ukaingia kwa mtu ambaye hawezi kukupa furaha ya ndoa uliyotarajia.

Katika hili naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, ukitaka kuingia kwenye ndoa epuka sana kuangalia muonekano wa mtu. Tukijichanganya macho yatatuingiza mkenge!Unaweza kumuona msichana mzuri, mwenye figa na sura ya kuvutia au mwanaume ‘handsome’, mwenye sifa zote za kupendwa na kila mwanamke lakini kumbe linapokuja suala la ndoa, hamna kitu!

Ni suala la wewe kuwa makini sana hasa pale unapotafuta mpenzi au mchumba! Achana na ile tabia ya kutafuta sifa kwamba eti ‘kapo’ yenu inavutia, swali ni je, anaiheshimu ndoa na siyo macho juujuu?

No comments:

Post a Comment