Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya saratani ya koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama ‘Oral Sex”. Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo pia huambukizwa kupitia njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili, pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.
Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanyangono wakitumia midomo hasa ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.
Katika utafiti huo wa hivi karibuni, ulibaini wanaume 747 na wanawake wakiwa 472hugundulika kila mwaka kuwa na saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka niwanaume 444 wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.
Soma: Jinsi Ya Kutambua Kama Ni Mtoto Wa Kike/kiume Wakati Wa Ujauzito?
Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45wanatumia staili ya kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni kuwavutia wapenzi wao katika kushiriki ngono.
Vijana wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku wengi wakiwa hawajui athari zake. Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment