Hisia
za mapenzi na msisimko huwa mkubwa kipindi ambacho upo kwenye penzi
jipya. Ukiwauliza watu wengi leo ambao wanateswa na mapenzi, wanatamani
siku zirudi nyuma ili warudie kufaidi mapenzi kama ilivyokuwa siku za
mwanzomwanzo.
Lakini wachache wanaojua nini cha kufanya
unapoanzisha penzi jipya ili hisia na msisimko unaoupata, udumu kwa muda
mrefu na uendelee kuyafurahia maisha ya kimapenzi. Mapenzi ni kama
nyumba, ukijenga msingi imara, nyumba yako itakuwa imara na ukijenga
msingi legelege, usitegemee nyumba yako kuja kudumu baadaye.
Kama upo kwenye mapenzi mapya na unatamani raha na msisimko unaoupata leo udumu, ni vizuri ukazingatia mambo yafuatayo:
MUONYESHE HESHIMA NA SHUKRANI
Wanandoa,
wachumba au wapenzi wengi, hulalamika kwamba wenzi wao hawawaheshimu,
hawana shukrani na ndiyo maana hawafurahii maisha yao ya kimapenzi.
Unapokuwa kwenye hatua za mwanzo za mapenzi, jenga heshima kwa mwenzi
wako bila kujali umri, cheo au hali ya kiuchumi. Hata kama mwenzi wako
ana udhaifu fulani, kwa sababu umempenda na kuamua kuwa naye, jifunze
kumheshimu.
Pia jifunze kuwa na shukrani hata kwa yale mambo
madogo anayokufanyia. Wengi huwa hawaoni umuhimu wa kuwashukuru wenzi
wao na matokeo yake wanajenga ufa ambao baadaye unasababisha matatizo
makubwa.
PATA MUDA WA KUMCHUNGUZA KWA KINA
Kuchunguzana
ninakomaani sha hapa, siyo kutaka kujua kabla yako alikuwa na nani
au amewahi kutoka na nani, wahenga wanasema bata ukimchunguza sana
huwezi kumla. Kuchunguzana ninakokuzungumzia hapa, ni vizuri kufuatilia
kwa kina ili ujue mwenzi wako anapenda nini, hapendi nini, kitu gani
kinamfurahisha na kitu gani kinamtia hasira.
Mchunguze akiwa na
hasira anakuwaje na akiwa na furaha anakuwaje, anapenda sana kufanya
mambo gani (hobi) au anapenda sana zawadi za namna gani. Ukishamjua, ni
rahisi sana kuishi naye hata pale anapokasirika au anapokerwa na jambo
fulani kwani tayari utakuwa unajua kwamba akiwa hivi, ujue amekasirika
au akifanya hivi ujue jambo fulani halipendi.
Pia itakusaidia
kwenda naye sawa kwa sababu akikasirika, utajua ufanye nini ili afurahi
kwa sababu tayari unavijua vitu vinavyomfurahisha. Ni makosa makubwa
kufanya jambo wakati unajua kabisa mwenzi wako hapendi.
JENGA UTARATIBU WA KUMUOMBA MSAMAHA UNAPOKOSEA
Wanaume
wengi wanaamini kwamba hata wakikosea, hawatakiwi kuomba msamaha kwa
sababu kuomba msamaha ni ishara ya udhaifu, matokeo yake wanaendekeza
mfumo dume bila kujua kwamba mapenzi ni demokrasia!
Bila kujali
kwamba wewe ni mwanaume au mwanamke, mkubwa au mdogo, una fedha au
huna, inapotokea umeziumiza hisia za mwenzi wako, iwe kwa jambo dogo au
kubwa, ni lazima uombe msamaha na kuahidi kutorudia makosa.
Ukishajenga
utaratibu huu, hata kama mwenzi wako hakuwa na kawaida ya kuomba
msamaha, taratibu utambadilisha. Utashangaa na yeye anaomba msamaha na
huo unakuwa mfumo wa maisha yenu. Kuwa makini kwamba ukiomba msamaha
leo, siyo kesho unarudia tena kosa lilelile, ataona unamfanyia
makusudi.
Saturday, April 7, 2018
Fahamu Nini cha Kufanya ili Kulinda Mahusiano Mapya
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment