Katika
hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja
suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara
kwa watu wanaoendekeza sana ngono.
Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.
Mtu
anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’
kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo
kwa sababu amelipa mahari.
Hilo
linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi
unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za
kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono.
Pamoja
na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na
kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema
tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika
kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya
miti kwa vile tu miili imetaka kufurahika.
KUPOTEZA HAMU YA TENDO
Watu
wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa
wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza
wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara.
Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.
Aidha
kukinai haraka staili za kimapenzi kunatajwa kujitokeza kutokana na
kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine sehemu
moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza kumfanya
mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye
na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.
KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA
Tabia
ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini
na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo
la ndoa bila kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa
kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi na kwa
wakati gani
Watu
wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndiyo wale ambao
kila wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake.
Hawa
ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa watumishi wa ndani au
kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa
zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi.
Unapokuwa
mtu wa kufanya mapenzi mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia
tamaa yako. Mumeo akiondoka siku mbili unatamani kuwa hata na houseboy
ili akukate kiu ya penzi.
KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO
Raha
ya tendo hutegemea sana hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na
kiu ya kufanya mapenzi, hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila
mara unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha
ambayo haikutoshi kumaliza tamaa yako.
Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo!
KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI
Madhara mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili.
Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya mwili uchoke.
Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.
Sambamba na hilo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa dhaifu.
KUPATA MAGONJWA
Kama
tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa na tamaa
na hujikuta wanafanya mapenzi holela ambayo huweza kuwasababishia
magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.
Ufanyaji
wa mapenzi usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa wanawake huwafanya
waishiwe msisimko na kuzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute unaoweza
kuwakinga na michubuko wakati wa kujamiiana na hivyo kuwasababishia
michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya haraka ya magonjwa ya zinaa
ukiwemo ukimwi.
Baada
ya kungalia madhara hayo machache ni vema kwa wapenzi kupunguza kiwango
cha kufanya mapenzi ili kuifanya miili iwe na uvumilivu unaoweza
kumsaidia mtu kukaa kwa muda mrefu bila kumsaliti mpenzi wake hata kama
atakuwa amesafiri mbali naye kimasomo, kikazi au kibiashara.
Sunday, April 8, 2018
Haya Ndiyo Madhara ya Kufanya Mapenzi au Tendo la Ndoa Mara Nyingi Kupita Kiasi
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment