Ushawahi kugundua ya kuwa wanawake kikawaida huvutiwa na wanaume ambao
wana hadhi ya juu? Kama ni kweli, najua kwa akili yako unafikiria ya
kuwa iwapo unataka kuwavutia wanawake warembo lazima uwe na umaarufu ama
tajiri ama zote mbili. Ni kweli?
Ok hapa NESIMAPENZI tunasema La! Unaweza kumwonyesha mwanamke kuwa pia
wewe una hadhi ya juu....na si lazima uwe na pesa nyingi wala kuwa staa
wa Bongomovies...
Mwanzo kuwa na hadhi ya juu ni nini? Je, kuwa mtu wa hadhi ya juu ina
maanisha kuwa tajiri ama maarufu? Ok hebu fikiria hivi: Kama mtu tajiri
zaidi ulimwenguni ameamua kusafiri hadi kisiwa flani kisichojulikana
ambacho hakina runinga wala redio... mtu huyu atakuwa na umaarufu kiasi
gani? Pesa ambazo anazimiliki zitakuwa na umuhimu gani?
Ni hivi, kuwa na hadhi ya juu ni mauzauza. Ni mauzauza ambayo yanajengwa
na maoni ya watu ambao unahusiana nao karibu. Mfano, unaweza kuwa na
hadhi ya juu ya maingiliano wakati ambapo unatangamana na familia yako,
tofauti na kuwa katika chumba ambacho kimejaa watu ambao huwafahamu.
Hivyo kama unataka kuonyesha hadhi ya juu kwa mtu flani, kuna mbinu mbili ambazo unaweza kutumia...
Kwanza: Nufaika na koti ya nyumbani
Katika michezo, kunufaika na koti ya nyumbani inamaanisha kuwa una
nambari kubwa ya mashabiki ambao watakupa sapoti na ambao wanayaelewa
mazingira uliyomo. Hivyo unaweza kutumia mbinu hii katika maisha yako ya
kujamiiana na watu kwa kuchagua sehemu mahususi ambazo utakuwa 'mtu wa
kawaida' katika hizo sehemu.
Kwa mfano, kuwa mtu wa kawaida katika baa ama klabu ina maana kwamba
unaenda sehemu hizo mara kwa mara, na pia wafanya kazi wote katika
sehemu hizo wamekuzoea mpaka wanakujua kwa jina. Kwa ufupi ni kuwa
umepandisha hadhi yako ya kujamiiana na wengine katika sehemu hizo kwa
sababu unaonekana sehemu hizo mara kwa mara.
Fikiria hili jambo wakati mwingine ambapo utahudhuria sehemu nyingine
ambayo hujawahi kuitembelea hata mara moja. Ni tofauti gani ambayo
utaihisi iwapo umekuwa ukiitembea sehemu hio kwa miaka mitatu iliyopita?
Je si ingekuwa rahisi sana kuwaonyesha wanawake waliokuzunguka kuwa
wewe ni mtu wa hadhi ya juu?
Bila shaka ingekuwa... mwanzo kama mwanamke mwenyewe si mtu wa kawaida
katika hio sehemu! Ungemtembeza sehemu hio na kumtambulisha kwa
"marafiki" zako wafanya kazi pamoja na wateja uliowazoea wa kawaida.
NB: Nenda utafute sehemu mbili ama tatu ambazo utakuwa mtu wa
kawaida katika sehemu hizo. Hakikisha ya kuwa sehemu hizo ni ambazo zina
wanawake wengi ambao wanaweza kustahili kuwachagua.
Pili: Jenga uhusiano mwema na koti ya nyumbani
Pindi ambapo ushatambulisha sehemu zako ambazo zitakuwa "manufaa ya
koti-nyumbani", anza kujenga uhusiano mwema na watu ambao wanakuwa hapo
wakati mwingi. Sehemu nzuri ya kuanza ni kwa wafanya kazi, kwa kuwa kila
wakati huwa hapo na mara nyingi huwa jamili.
Jifunze majina ya watu na angalau ujue jambo moja linalowavutia.
Hakikisha ya kuwa unakuwa mkunjufu kwa wafanya kazi na pia kuwapa
bahshishi mara moja au nyingine. Pia usisahau kutambulisha majina ya
wafanya kazi wengine iwapo utakumbana na wafanya kazi wengine wapya.
Hii itasaidia kugundua ya kuwa wewe ni mtu ambaye unajulikana na wafanya
kazi wale wengine, na itasaidia kuonyesha hadhi kuu kwako kwao. Fanya
mazoezi ya mara kwa mara na uwe na subira, na uanze pia kutangamana na
wateja wa kawaida katika sehemu hizo.
Kwa muda wa wiki kidogo, itakuwa rahisi kwako kumuonyesha mwanamke
yeyote ambaye unakutana naye kuwa wewe ni mwanaume wa hadhi ya juu
katika sehemu hizo.
Upo!?
Monday, April 30, 2018
Jinsi Ya Kuonyesha Kuwa Una Hadhi Ya Juu Kwa Mwanamke
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment