Kusema ule ukweli, hakuna kitu kama formula ama mbinu ambayo inaweza
kukufanya upate deti ambayo imeshamiri na bora zaidi. Mwanzo ukiplan
kutumia ujanja na gemu katika deti yako ya kwanza, unaweza usifike
popote katika deti hio. Lakini hii haimaanishi ya kuwa hakuna mbinu
ambazo unaweza kuzitumia kuhakikisha ya kuwa unakuwa na deti muruwa
kabisa. Hivyo basi tumekuja na baadhi ya mambo ya kufanya wakati ambapo
utatoka deti kwa mara ya kwanza na mwanamke.
#1 Kuwa wewe mwenyewe
Inaweza kuwa na ukweli kiasi flani ya kwamba ni lazima uonyeshe mvuto
kwa mara ya kwanza unapotoka deti na mwanamke, lakini hii haimaanishi ya
kuwa unapaswa kuingiwa na wasiwasi kutimiza jambo hilo. Mwanzo, kuwa
wewe mwenyewe ni njia rahisi ambayo unaweza kuitumia kumteka mwanamke.
Pia hii haimaanishi ya kuwa unapaswa kujifanya kuwa mtu ambaye hafanani
na hulka yake. Kando na hayo yote, kama utaendelea kuiga tabia ambayo
haifanani na wewe usiku mzima, utamfanya afall in love na mtu mwingine.
Hivyo basi ni bora zaidi uwe wewe mwenyewe, na uendelee kuanzia hapo.
#2 Pumua
Haina haja ya wewe kujistress na deti yako ya kwanza ama kuhakikisha
kuwa kila kitu kinaenda sawa. Deti za kwanza kwa kawaida huwa si za
kueleza kwa kina, bali ni kupata kujuana wewe na huyo mwanamke. So hata
kama kuna jambo ambalo linaweza kufanyika usiku huo, wewe pumua na
kuchulia kosa lolote ambalo linaweza kutendeka kama mwanzo wa gumzo lako
ama unaweza kufanya mzaha jambo hilo wakati mwingine ambapo utakutana
katika deti ya pili. Pia, usisahau kuonyesha confidence na uonyeshe kuwa
wewe ni mwanaume alpha.
#3 Chagua sehemu bora
Kama tulivyotangulia kusema awali, deti za kwanza huwa lengo lake kuu
huwa ni kujuana zaidi kati yako na huyo mpenzi wako. So, weka simu yako
kando usiku huo, msikilize kwa makini mwanamke uliyetoka naye deti na
uhakikishe ya kuwa umechagua sehemu ambayo nyote wawili mtaiona bora ili
muweze kutangamana vizuri pamoja. Hii inamaanisha kuwa hupaswi kwenda
deti ya kwanza na mwanamke katika sinema, concerts ama sehemu za
michezo.
#4 Uliza maswali
Amini usiamini, kitu rahisi kama kuonyesha interest ya uhakika kwa
mwanamke katika deti kunaweza kumfanya apendezwe na wewe kwa muda mfupi
sana. Haijali kama utamuuliza swali tata au lisiloeleweka. Ilimradi tu
uendeleze mazungumzo yenu wawili huku ukimsikiliza kwa umakini,
utaonyesha idhibati kuwa wewe ni mwanaume anayejali. Njia hii unaweza
kumjua zaidi mwanamke aina hii na pia kupata ujuzi wa kuongea na
wanawake kwa ujumla, na kuwa na uunganisho wa haraka katika deti zako.
#5 Jienjoy
Hii inaenda sambamba na pointi tulioieleza awali. Wakati mwingi, wanaume
wengi huingiwa na wasiwasi na kibaridi wanapotoka deti kwa mara ya
kwanza kiasi cha kuwa wanasahau kujiachilia na kuenjoy deti hio ambayo
inaendelea. Unapaswa kujua kuwa mwanamke anayetoka deti na wewe
hatavutiwa kwako kama hutatabasamu wala kucheka na yeye hata kwa mara
moja.Tofauti na kama utamwonyesha mwanamke kuwa unajienjoy na kuburudika
na uwepo wake, basi naye pia ataenjoy company yako wakati wote. So,
jaribu kufanya mizaha, mchekeshe na mwonyeshe ishara za mapenzi kadri
uwezavyo. Usisahau kumwambia kupitia jumbe au simu kuwa ulienjoy kuwa
naye katika deti hio.
Sunday, April 29, 2018
Jinsi Ya Kuwa Na Deti Ya Kwanza Na Mwanamke Ambayo Itampendeza
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment