e kuna kitu ambacho kinafurahisha zaidi (kando na kufanya mapenzi)
ambacho kinasisimua zaidi kuliko kuwa na mazungumzo ya kufurahisha na
mwanamke? Ok. unajua vile mazungumzo aina hii hutokea, wakati ambapo
unayaona mazungumzo yako na mwanamke yanaenda na wimbi moja, unajihisi
kana kwamba mko mkondo mmoja, na cha kufurahisha zaidi ni kuona ya kuwa
mnamaliziana sentensi zenu bila wasiwasi halafu...
Ghafla inatokea situation ambayo kuna kuwa na kimya. Wakati ambapo
umebakia unang'ang'ana angalau upate kitu cha kufanya maongezi yenu
yarudie tena , kuna ile hisia ya pole pole inayokuja ambayo unajihisi
kana kwamba unapoteza nafasi yako na mwanamke huyo kuendeleza
matangamano yenu. Kibaya zaidi ni kuwa, kadri kimya kinapoendelea
kuzidi...ndipo unazidi kuwa na mawazo ambayo hayana msingi ambayo
unayajaribu kuyasema.
"So, anga ya leo unaionaje?" ama "leo kuna jua kali!" ni maneno ambayo
unabakiwa nayo kuyasema ukijaribu angalau ufanye ukimya wenu upotee...
Well, kama umekuwa ukikumbwa na changamoto kama hizi wakati ambapo
unajaribu kuongea na mwanamke... acha tuongee jinsi ya kuhakikisha ya
kuwa unakwepa jangamizi hili wakati ambapo unakuwa na mwanamke.
1. Usipange kuhusu maongezi yako ya mbeleni sana... lakini...
Ingawa itakuwa ni jambo mwafaka la kupanga kitu cha kusema mbeleni
wakati ambapo unakumbwa na hisia za shoto (awkward), hii inaweza kufanya
kutangamana kwenu kuonekana shoto zaidi. Walakin kuna njia kadhaa
ambazo unaweza kusema wakati ambapo unakumbwa na kimya kirefu. Maneno
haya yatasaidia sana haswa wakati imetokea situation kama hii.
Hizi ni baadhi ya sentensi unaweza kutumia wakati kimya kimewajia ghafla katika maongezi yenu:
"Ushawahi kujiuliza ni kitu gani kinachofanya kimya kirefu kuleta hisia za shoto?"
Ukifikiria vizuri kuhusu hili swali, utaliona kuwa ni swali zuri ambalo
linasisimua na ambalo linaweza kujenga maongezi marefu. Swali kama hili
pia linakupa wewe nafasi ya kuweza kupata kuijua haiba ya mwanamke
unayeongea naye.
"Ulikuwa wajua ni njia gani rahisi ya kuonyesha kuwa unamtambua na
kumfahamu mtu flani? ---mpe nafasi akujibu--- "Wakati ambapo inatokea
ukimya wenu mumeuzoea kuwa ni sehemu yenu ya mazungumzo. Je, uligundua
hilo?"
Hii tena inatoa nafasi kwako kupata kumwelewa zaidi mwanamke unayeongea
naye na bila shaka inaweza kumfanya mwanamke kuvutiwa kwa mazungumzo
ambayo utakuwa ukiyaendeleza. Kutumia mbinu hizi pia kunasaidia kufanya
ukimya wenu kuonekana kama kitu ama jambo la kawaida bila kuleta hisia
za shoto. Hii ni kwa sababu mambo ambayo huonekana kama hayajazoeleka
yakiwekwa wazi na kuzungumziwa kwayo inayafanya yaonekane kama mambo ya
kawaida.
Hii ni kweli kwa sababu hisia za shoto ambazo zinajitokeza katika
maongezi ni sawa na jambo lolote lile ambalo huonekana kama ni geni.
Lakini pindi ambapo mtaamua kuweka wazi na kuliongea swala hilo, inatoa
hisia zozote ambazo zinaweza kuharibu maongezi yenu.
NB: Anza mazoezi ya kutumia mbinu hii kwa kuwauliza marafiki zako
na watu unaotangamana nao kabla ile siku ya kuanza kuongea na deti
wako. [Soma: Mada ambazo zitaua upendo kwa mwanamke]
2. Mtie ufunguo yeye ndie awe anayeongea
Wanaume wamebarikiwa sana kwa kuwa wanawake ndio wamepewa talanta ya
kuongea. So kwa mwanaume akicheza karata zake vizuri, hahitaji kufanya
mengi ikija kwa maswala ya maongezi. Kile kinachohitajika ni kujua
wakati na maswali ambayo unafaa kumuuliza mwanamke na kuwa msikilizi
mzuri.
Ukiwa mbora zaidi wa kusikiliza anachosema ndipo unapomfanya azidi kuwa
interested na kuongea na wewe. Pia utakuwa ukimfanya ajiskie huru kwako.
Mwanzo iwapo utamfanya ajihisi yuko huru kwako utafanya maongezi yenu
yawe marefu zaidi kuzidi yale ambayo ulikuwa ukiyatarajia.
Ufunguo hapa ni kujua jinsi ya kuyaandaa maswali yako kulingana na kitu
ambacho anaongea. Kama anakuambia kuhusu kitu anachopenda, muulize kwa
nini anakipenda. Kama ni kitu asichokipenda, muulize kwa nini hakipendi.
Kuuliza swali la 'kwa nini' huwa inasaidia sana kuingia katika mzizi wa
haiba yake na kutakufanya umuelewe kiundani zaidi kumhusu. Kadri
unapozidi kufanya hivi, ndipo unazidi kumfanya afunguke na kuongea vitu
zaidi ambavyo utakuwa na nafasi ya kuuliza maswali zaidi kwayo.
Kando na hio usijisahau ukaingia katika wingu la wanaume wengine wengi
feki ambao hupenda kujibu maswali na neno moja. Ni muhimu kuhakikisha ya
kuwa wakati ambapo yeye pia atakuuliza swali uhakikishe ya kuwa
unafunguka na kuelezea kila kitu ambacho unaona kinafaa kwa yeye kujua.
Kawaida ni kuwa kadri unapofunguka kujieleza kwa mwingine, ndipo pia
yeye anafunguka kukuelezea yake...na hii huchangia mazungumzo yenu kuwa
wazi na marefu. [Soma: Jinsi ya kuongea na mwanamke umvutie]
Monday, April 30, 2018
Jinsi Ya Kuyafanya Maongezi Yako Na Mwanamke Yawe Marefu
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment