Acha tuwe waadilifu kiasi...
Baadhi ya wengine wetu wanashindwa kupata deti na mwanamke.
Baadhi ya wengine wetu wanaweza kupata deti mara ya kwanza lakini wanashindwa kupata deti ya pili.
Wengi wanadhania ya kuwa si makosa yao - eti ni makosa ya mwanamke mwenyewe.
"Nilimwita tukatoka deti mara ya kwanza, nilipomwambia tutoke deti ya pili alikataa. Sijui tatizo liko wapi"
So tatizo huwa linajitokeza wapi?
Kulingana na tafiti tulioufanya katika blog hii, tumekuja na sababu tatu
kuu ambazo zinachangia wengi kushindwa kutoka deti na mwanamke mara ya
kwanza au mara ya pili.
#1. Haujitayarishi kutengeneza deti ya pili wakati ambapo deti ya
kwanza bado haijakamilika. Pia itakuwa hujamsisimua vizuri kuhusu
wakati ambapo mtakutana tena katika deti ya pili.
Ok mpango mzima huwa hivi, iwapo unataka deti ya pili na mwanamke
itendeke, lazima umwelezee na mapema kuhusu deti yenu ya pili. Pia iwapo
unataka deti ya pili na mwanamke lazima umsisimue kuhusu deti yenu ya
pili, mfano unaweza kumdokezea kuhusu mambo ambayo unatarajia kumfanyia
mtakapo kutana mara ya pili nk.
#2. Itakuwa haujitahidi kuwa wewe mwenyewe. Itakuwa unababaika na
kuwa na wasiwasi wa kutaka kuhakikisha ya kuwa husambaratishi deti yako
naye, jambo ambapo linafanya deti yako na mwanamke kuharibika.
Kwa kawaida mwanamke hupenda mwanaume ambayo yuko wazi, mwenye nishati
na pia hisia. Hivyo ni rahisi sana kwa mwanamke kutambua iwapo mwanaume
ameingiwa na wasiwasi ama uoga.
#3. Hausikilizi kile ambacho anasema. Tatizo hili humkumba
mwanaume wakati ambapo anajaribu kufikiria sana kuhusu mambo ambayo
anataka kumuuliza ama kumjibu mwanamke ili kutafuta vitu mnavyohusiana
pamoja badala ya kumakinika na kumsikiliza mambo ambayo anayasema.
Ok... kwa kifupi ni kuwa hizi sababu tulizozieleza hapo juu huchangia
kwa mwanaume kushindwa kuzuia deti kwa mara ya kwanza kwa mwanamke au
kwa mara ya pili.
Kama umetoka deti na mwanamke kwa mara ya kwanza, sioni tatizo la kwako
kushindwa kutoka naye deti mara ya pili, tatu, nne na hata ya tano na
mwanamke unayemfukuzia.
Kile unachopaswa kuzingatia ni kuangalia vile ambavyo unawatendea katika
deti, ujanja wako wa kutumia mbinu kadha wa kadha za kuwashawishi, na
cha msingi ni vile ambayo utamakinika kutaka kujua vitu ambavyo mwanamke
anataka katika deti.
Monday, April 30, 2018
Sababu 3 Kuu Ambazo Zinakufanya Ushindwe Kumtoa Mwanamke Deti
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment