Baada ya kumhoji na kumuuliza maswali tulikuja kugundua kitu flani; alikuwa akilipuuza swala la mwonekano wake wa mwili.
Katika posts zetu za awali tumekuwa tukisistiza ya kuwa mwonekano wako si muhimu sana wakati wa kutongoza. Lakini je ukipatana na mwanamke ambaye kila wakati unapojaribu kumtongoza na kumshawishi anakuwa na maringo?
Jeuza na kuongeza mwonekano wako wa mwili ghafla!
Well, najua wakati ambapo unaaproach mwanamke mara ya kwanza fikra
inayokuja ya kwanza ni kuwa mwanamke kama huyu asikuhukumu na vile
ulivyovalia ama mwonekano wako bali aangalie tabia na maneno yako matamu
ambayo utakuwa ukimwambia. Lakini kwa bahati mbaya ni kuwa wanawake
wachache mno ambao wataangalia tabia yako, wengi huangalia mwonekano
wako. [Soma: Jinsi ya kumtongoza mwanamke kwa ktumia sanaa ya kiza]
Leo nimeamua kuandika post hii maksudi ili tuweze kuiteka hii asilimia
kubwa ya wanawake ambao huangalia mwonekano wa mtu badala ya tabia.
Zama nami.
1. Valisha utu wako
Utu wako ndicho kigezo kikuu cha kupima vile ambavyo utavalia na wala si
kuangalia nguo ambazo zinatrend wa maduka au soko. Ni mara ngapi
ushawaona watu unaowajua wakivalia nguo flani halafu ukasema "hizo nguo
haziendani na wewe"?
Kwa wanawake wao huwa kama polisi katika fasheni, hata kama hawana
taaluma hio. Ukivalia nguo ambazo haziendani na mwili wako, hazilingani
na utu wako ama kutofanana na wewe utajikuta ya kuwa unatengwa ama
kujiona samaki aliyetolewa baharini mbele ya wanawake. [Soma: Saikolojia kumfanya mwanamke akupende daima]
Hii ni sehemu ambayo inahitaji umakini wa hali ya juu, valia nguo ambazo
zinalingana na wewe na muda si mrefu utaona wanawake wakikutambua.
2. Tafuta fasheni ambayo haipo
Fasheni ambayo si ya kawaida kama kuvalia sigha ni njia rahisi ya
kupanua mwonekano wako. Unaweza kuvalia shanga, cheni, saa, pete nk ili
kujenga mwonekano wako. Wasanii wengi hutumia mbinu hii ili kuvutia
hadhira yao, hivyo sioni kama kuna tatizo iwapo utakuwa na mtindo huu wa
mavazi. Muhimu ni umridhishe yule mwanamke ama sivyo?
3. Viatu vya maana
Usiniulize kwa nini unafaa kuachana na viatu vyako vya tangu ulipokuwa
shuleni na kuanza kuvalia viatu vya fasheni. Wanawake wanakuwa na tabia
ya kushangaza. Kitu cha kwaza watakacho kukuangalia ni viatu vyako.
Hivyo iwapo kama unavalia viatu vya kutoboka ama vichafu hakikisha ya
kuwa unafanya bajeti ya kununua viatu vipya haraka iwezekanavyo.
[Soma: Hatua za kufanya ili umfanye mwanamke aingiwe na wivu kwa manufaa yako]
[Soma: Hatua za kufanya ili umfanye mwanamke aingiwe na wivu kwa manufaa yako]
Unaweza kuulizia viatu vizuri vinavyokufaa katika duka ambalo utaenda
kununua viatu ama unaweza kumchukua rafiki yako mwanamke akakuchagulie
viatu kulingana na vile atakuona.
4. Nywele za usoni
Wakati mwingine ambapo utatembelea kinyozi hakikisha ya kuwa ndevu zako,
masharubu, kionja mtuzi, nyusi (wanawake wengine huziangalia) na nywele
zote kwa kichwa chako zinalingana na mwonekano, mitindo, na tabia yako.
Hii ni kwa sababu zote hizi ni baadhi ya fasheni ambayo wanawake
huangalia kwa umakini.
Ingawaje kunyoa kipara na ndevu zote si jambo baya, jiulize kwa nini
mbona wasanii wengi wanapenda kuweka nywele za usoni na kuzishepu.
5. Safisha meno yako ama yafanye meupe
Wanawake wanatambua meno yako kwa uharaka sana hivyo unafaa kuyaweka
safi na meupe. Mwanaume ambaye ni mchafu wa meno meseji anayotuma kwa
mwanamke ni kuwa maisha yake ni machafu, kama utashindwa kutunza meno
yako bila shaka huwezi kudumu usafi mwingine. [Soma: Jinsi ya kumtongoza mwanamke kwa ktumia sanaa ya kiza]
Pia weka kwa akili yako ya kuwa mwanamke anatarajia ya kuwa mwisho wa siku atakuwa na mwanaume ambaye anaweza kumlaza hivyo ni muhimu kuwa makini na usafi. Meno machafu, meusi ama rangi ya njano yatakufanya utengwe na wanawake mara kwa mara.
Upo!? Sasa ingia hapa uongeze makali yako.

No comments:
Post a Comment