Kama umekuwa ukijiuliza ni wakati gani ambapo hisia za kupendana zinakuja kwako na kwa mwanamke acha nikuambie ukweli...si mara ya kwanza ambapo mtakutana kwa deti bali ni mara ya pili. Hapa ndipo uhusiano kati yenu wawili wa kimapenzi unaanza.
Hili ndilo tatizo kubwa ambalo wanaume wengi wanakosa kulielewa. Unapata
mwanaume anarusha silaha zake zote siku yake ya kwanza ya deti na
mwanamke...kosa kubwa kabisa.
Ok najua sahizi unafikiria nini. Ya nini kukutana na mwanamke deti ya pili ilhali unaweza kufunga bao mara ya kwanza mnapokutana? Well,
sikatai ya kuwa si vibaya kufunga mchezo siku ya kwanza. Mwanzo mimi ni
miongoni mwa wale ambao wanajivunia kupata mgao wa nafasi kama hio.
Lakini niamini nikikuambia ya kuwa baada ya muda flani itafikia level
ambayo utaacha gemu yako ya kuapproach wanawake na utataka kutafuta
mwanamke wa kawaida ili uanze mahusiano ya level nyingine. Kufanya mapenzi ni mwanzo tu. Hivyo ni bora uanze kutafuta mwanamke ambaye analingana na wewe kimawazo na mtizamo. [Soma: Tongoza kama bingwa kwa kufuata hatua hizi]
KILE NTAKACHOKUAMBIA SAHIZI KITAKUSHTUSHA...
Mawaidha mazuri ambayo nataka nikuambie ni kuwa jiepushe na kufanya mapenzi
siku ya kwanza ambapo utadeti ama kumtoa out mwanamke. Jikontrol na
ujizuie usionyeshe hisia zako za mapenzi hadi wakati mwingine ambapo
mtameet. Sababu ya kusema hivi ni rahisi. Mtakuwa mmebadilisha akili
yenu kutoka kudeti kikawaida hadi kudeti kunakoonekana serious. Hii
itakuwa deti ya hakika ambapo pia yeye atachukulia vivyo hivyo.
Sababu nyingine ambayo hufai kufanya mapenzi deti yenu ya kwanza ni
'kujutia baada ya kucha'. Hii mara nyingi hutokea kwa wanawake ambapo
wanajutia kwa kitendo walichofanya usiku uliotangulia. Hapa wanawake
wanaweza kuingiwa na hisia za kujutia za kuwa walishindwa kujizuia
kufanya mapenzi wakati ambapo walikuwa katika deti...mara nyingine hii
inaweza kumwathiri mwanamke kiasi cha kuwa anaweza kushindwa kuendelea
na mahusiano yenu. [Soma: Jinsi ya kujizuia kufanya mapenzi]
Ok. Je namaanisha ya kuwa deti yako ya kwanza na mwanamke unayempenda
hufai kulenga nyota yako kwa kutumia ujuzi wako wote wa kumteka hisia? La hasha.
Lile ambalo nasistiza ya kuwa mambo mengine unafaa kuyahifadhi hadi deti
yako ya pili. Kufanya hivi kutamfanya mwanamke kujiskia huru kuongea
zaidi kujihusu huku akijiamini ya kuwa bado ana uwezo wa kutumia ujanja
wake kama mwanamke.
Kufanya mapenzi na mwanamke kunamfanya kujihisi kama yuko uchi. Pia
atakuwa akiingiwa na maswali ya iwapo kama unampenda kweli ama uko hapo
kumtumia kujiridhisha wewe mwenyewe binafsi.
Ajenda yako kuu ni kutaka kumfanya mwanamke kama huyu akuone kama
boyfriend wa maisha yake. Ama sivyo? Hii inamaana ya kuwa mapenzi
utakuwa ukifanya naye muda wote ukijumlisha ya kuwa na mahusiano marefu
kati yenu.
So siri ya kufanikiwa hivi ni nini? Rahisi. Ni kumfanya ajiskie
huru, kujenga kizingiti cha uhusiano wenu na kumfanya ajitolee kukujua
zaidi....hivi vitu vitatu vitajenga mahusiano ya nguvu siku ya pili
mtakapokutana katika deti. [Soma: Hatua za kumzuzua mwanamke akupende milele]
Wednesday, May 2, 2018
Siri 1 Kuu Ya Kudeti Na Kutongoza Ambayo Wanaume Wengi Hawaijui
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment