Je wewe ni single boy? Au bachela kama wengi ambavyo hupenda kujiita?
Kama jibu ni ndio basi naomba utambue ya kwamba suala la kupata mke si
kazi bali kupata wife material ndio kazi. Hivi hujawahi kusikia wahenga
wa zamani wakisema ya kwamba ni heri ukosea njia utauliza kwa pita njia
kuliko ukosee kuoa? Hii ina maana gani? Hii ina maana ya kwamba wakati
unafanya mchakato wa kutafuta mke wa kuoa ni lazima uzingatie misngi na
mchakato mzima wa kupata mke bora na si ke bora.
Miongoni mwa misingi hiyo ni lazima uchagua mwanamke ambaye atakuwa na sifa hizi:
1. Mwanamke ambaye hana tamaa ya pesa.
Katika maisha ya sasa mwanamke anayependa sana pesa ukikubali awe mkeo
mtasumbuana sana. Kwa maana hiyo mwanamke ambaye utagundua hana tamaa ya
pesa, kwamba ikiwepo, ikikosekana anabaki kuwa yuleyule wa siku zote,
huyu ni ‘wife material’.
2. Mwanamke anayependa watoto
Utajuaje kama mwanamke uliyenaye ana mapenzi na watoto? Iko hivi; katika
uhusiano wenu ukiona ni mtu wa kupendapenda sana watoto wa marafiki
zake, kuwanunulia zawadi, kuwashauri wenzake namna nzuri ya kuwalea
watoto, hata akija kupata wa kwake itakuwa ni hivyohivyo, huyo ni wife
material unatakiwa kumoa haraka.
3. Mwanamke ambaye ana heshima ya kweli.
Msichana ambaye anaheshimu kila mtu, mdogo na mkubwa, anawapenda na
kuwaheshimu ndugu, jamaa na marafiki zako, huyu ana sifa ya kuwa mkeo
pia.
4. Mwenye uwezo wa kujishusha.
Ogopa sana mwanamke ambaye anataka usawa, yaani yeye hata akikosea
anakuwa hayupo tayari kusema samahani msichana wa aina hii hafaai bali
Anayekufaa ni yule anayejua yeye ni mke, nawewe ni mume. Anayetambua
kuwa, mwanaume ndiye kiongozi wa familia.
5. Mtu ambaye anakushauri kwenye mema.
Kama mpenzi wako ni wa kukutaka kila siku muende baa au mfanye madili
hatari ili mpate pesa, huyu hana sifa ya kuwa mkeo. Mke ni yule ambaye
atakuongoza kwenye kutenda mema na kuacha mabaya. Kwa mfano kama
unakunywa pombe atakushauri uache, kama siyo mtu wa ibada, atakushawishi
umjue Mungu wako na mambo mengine kama hayo.
Tuesday, June 19, 2018
Hizi Hapa Sifa za Wife Material, Kwa Vijana Wanaotafuta Kuoa
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment