Mimi nimeolewa miaka 15 sasa na tumejaaliwa watoto 4. Ndoa yetu
ilipofikisha miaka 4-5 mume wangu alicheat, nikamkamata through sms
akapinga sn lakini baadae alikubali akakiri kosa na kuomba msamaha.
nikamsamehe
Tumeendelea kuishi na nilipopata mtoto wa tatu akanicheat tena, safari
hii alikuwa nje ya nchi kimasomo, napo alikiri na kuomba msamaha,
nikamsamehe
wakati niko mjamzito mimba ya mtoto wa nne alinicheat tena, kibaya zaidi
alinicheat na house girl wng akampa ujauzito. kwa ivo wkt mimi nina
mimba na House girl naye mjamzito(japo sikujua km house girl alikuwa
mjamzito kwani aliondoka nyumbani) niligundua baadae kuwa mtt wa
aliyekuwa house Girl wangu ni wa mume wangu
kama kawaida yake akaomba msamaha safari hii hadi kupiga goti na kulia
ili nimsamehe...na mimi kwa kuwa bado nampenda na nimemvumilia kwa mengi
nikaamua kumsamehe tena..ila tulikubailana masharti mengi na akakubali
masharti yote niliyompa..mwanzoni alibehave vizuri sn akawa muwazi kwng
hanifichi chochote kuhusu huyo mtt.. na tuliishi maisha ya furaha kwn
alinijali mno na alionekana kweli amerigrate.
sasa cha kushangaza siku za karibuni amebadilika san, amekuwa msiri na
hasemi chochote kuhusu huyo mtt wa nje..siku hizi anatuma hela kwa siri
na pia anawasiliana na huyo mama wa mtoto kwa siri haniambii chochote..
nilipoona mabadiliko niliamua kumuuliza imekuwaje tena mbona siri tena
wkt tulikubaliana kila kitu kiwe open? hakunijibu isipokuwa alikuwa
mkali na kufoka na kusema hilo swala tumeshamalizana nalo sitaki
kulisikiasikia tena..
nikajaribu tena siku nyingine kumuuliza na majibu ndio hayo hayo, kwa
kifupi hataki na anakwepa kuzungumzia hilo suala kabisa...sasa najiuliza
kwa nini anafanya siri? km hakuna jambo lolote baya basi anaficha nini?
ina maana kuna kitu zaidi ya mtoto.
Sasa jamani mimi nimeamua km ifuatavyo
1. Na mimi nimeamua kuwa na mahusiano nje ya ndoa, jamani msinilaumu
nami pia nahitaji kuliwazwa na kufarijiwa kwa kifupi nimechoka na
mastress yasiykuwa na mwisho, sikuwahi kumcheat mume wng ktk maisha yote
ya ndoa. ila sasa atanisamehe tu ht akijua wl sijali, nipo tayari kwa
lolote..
2. Sina mpango wa kuondoka kwenye nyumba tuliyojenga pamoja nitaishi
hapa hapa kwani sipendi wtt wng walelwe na mzazi mmoja..wtt hawajui
kinachoendelea in fact hata ndugu na jamaa hawajui chochote kwani mimi
sijawaambia na wala sijawahi kuwaeleza matatizo ya ndoa yng..kwa nje
tunaonekana familia iliyobarikiwa na ina furaha lkn wenyewe ndio
tunaojua ndani kukoje
3. Kwa sababu sisemagi matatizo yangu kwa ndugu na marafiki nimeamua
kuweka hapa labda nitapunguza kitu fulani kichwani kwani sometime naona
km nazidiwa mawazo vile
Wednesday, June 20, 2018
JAMANI Naombeni Msinilaumu Kwa Uamuzi Huu Niliouchukua Kwa Mume Wangu
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment