BUNGE limepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, na sasa
sheria imetamka kuwa ofi sa wa umma aliyesababishia serikali au taasisi
ya umma kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa makusudi au kwa uzembe,
atachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kukatwa mshahara wa miezi sita.
Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amesema mabadiliko ya
Sheria ya Bajeti na yale ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
yaliyopitishwa jana bungeni, hayakusudii kupoka kwa namna yoyote ile
mamlaka ya kisheria ya Bunge.
Kifungu cha 65(2) cha Sheria ya Bajeti kinaweka masharti kuwa iwapo
itathibitika kuwa ofisa wa umma kwa makusudi au kutokana na uzembe,
alisababisha serikali au taasisi ya umma kushindwa kutekeleza majukumu
yake chini ya sheria hiyo, atatenda kosa la kinidhamu.
Masaju alisema atawajibishwa binafsi kwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu
au kushtakiwa kwa kosa la jinai kulingana na aina ya madhara yatokanayo
na kushindwa majukumu hayo.
Kuhusu uhamisho wa fedha, alisema baada ya mabadiliko hayo hivi sasa
uwasilishaji wa taarifa za uhamisho wa fedha na uwasilishaji wa taarifa
za serikali na taarifa za mapato na matumizi, zitawasilishwa kila baada
ya miezi sita kwa maana ya nusu mwaka, badala ya miezi mitatu kwa maana
ya robo mwaka kama ilivyokuwa awali.
Akihitimisha hoja yake aliyoiwasilisha bungeni kuhusu Muswada wa Sheria
ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2017, ambayo ndani yake
ililenga kufanya mabadiliko katika Sheria ya Bajeti na mabadiliko ya
sheria ya ofisi yake, Masaju alisema kimsingi muswada huo sio wa
kubadilisha kanuni za haki na madaraka ya Bunge wala madaraka ya Kamati
ya Bajeti kama baadhi ya wabunge wanavyodhani
Wednesday, June 20, 2018
WATUMISHA Wavivu wa Serikali Kukiona Cha Moto...Mishahara Kufyekwa
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment