Baada ya taarifa kuenea mitandaoni kuwa mkuu wa kanisa letu anatuhumiwa
kubeba mrembo wa watu, nimeona kuna emergency ya kuandika juu ya hii
mada. Lengo langu sio ku promote uchepukaji, but no, my position is, mtu
anapochepuka humkosea Mwenyezi Mungu, lakini pia humkosea mwenzi wake.
Unapomkosea Mwenyezi Mungu ni rahisi kusamehewa ukiomba msamaha, na
Mungu anaweza akakupa ka adhabu mambo yakaisha.
Kimbembe mpenzi wako akikudaka, sio rahisi sana kurejesha mahusiano mema
na mpenzi wako, that is why am here to 'prevent a major catastrophes'
btn you and your partner from happening:
Rule No 1 ya kuchepuka bila kudakwa
Usinogewe na penzi la mchepuko! Mwizi huwa hadakwi siku ya kwanza. Wengi
wanaochepuka huwa wananogewa na kujisahau mpaka wanaanza kupiga piga
simu na kutuma text hovyo. Mara hujiachia na kujisahau kuwa wanachofanya
kinatakiwa kiwe siri. Ukiona umeshaanza kunogewa na penzi la mchepuko,
au yeye keshaanza konogewa na wewe, piga chini, ni bora utafute mchepuko
mwingine na uanze nao mwanzo...
Rule No 2 ya kuchepuka bila kudakwa
Msifanyie mambo yenu 'machoni pa watu'
Kama mnavyojua kuwa penzi ni kikohozi, basi usikohoe mahali ambapo watu
wanajua sauti yako. Kama unachepuka ni bora ukachepukie mbali kabisa na
maeneo ambayo umezoeleka. Hii itapunguza kuenea kwa info juu ya
uchepukaji wenu.
Rule No 3 ya kuchepuka bila kudakwa
Kumbuka, hakuna siri ya watu watatu. Usimhadithie mtu YEYOTE juu ya
uhusiano wako na mchepuko. Mkiweza kuifanya hii ikawa siri yenu wawili,
itawasaidia kuliongezea uhai penzi lenu la siri. Pale unapo mwambia
rafiki yako, naye atamwambia mwingine na mwingine na mwishowe siri
itavuja sehemu isiyotakiwa kufika, so from there mtawekewa mitego na
kuanza kufuatiliwa kwa siri.
Rule No 4, ya kuchepuka bila kudakwa
Simu ni adui wa penzi mchepuko
Watu wengi wanaochepuka hudakwa sana kwa njia ya simu. Kuwa muwazi kwa
mchepuko wako kuwa upo kwenye serious relationship/ ndoa na so
ajicontrol hasa kupiga piga simu na kutuma vi text. Kama vip ni bora
utafute kisimu special kwa ajili ya mchepuko wako. Kisajili kwa jina la
mtu asiye na uhusiano wowote kabisa na wewe. Then uwe unakitumia
kuwasiliana na mchepuko wako. Ili mambo yakibuma, inakuwa ni rahisi
kwako kukikana hicho kisimu. Unaweza ukasingizia kuwa labda kuna mtu
alikisahau kwenye gari wakati umewapa mafundi lifti kwenda site n.k
Rule No 5 ya kuchepuka bila kudakwa
Dont leave any phyisical evidence.
Jaribu kupoteza ushahidi wowote wa yale yatakayotokea kwenye crime
scene! Juzi hapa kuna mdau alileta kisa chake kuwa alichepuka na shem
wake alafu shem akasahau bikini master bed room, so wife alivyokuja
akaikuta na ikawa msala.
So kama ukiwa na mchepuko, hakikisha hakuna ushahidi utakao watia
hatiani pasi na kuacha shaka. Huu ni uzembe mkubwa sana ambao unawafanya
watu wadakwe kirahisi.
Hitimisho:
Nadhani ukifuata kanuni hizo hapo juu itakuwa ni msingi mzuri wa kutunza
penzi/ ndoa yako kwa mda mrefu zaidi. Mwisho naomba nikuache na agalizo
kutoka Mithali 14:12 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu,
Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
Wednesday, July 25, 2018
Jinsi ya Kuchepuka Bila Kukamatwa!
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment