Unampenda mwanaume flani lakini hajaonyesha dalili zozote za kukupenda?
Umejaribu kutumia maujanja yako uliobarikiwa nayo kama mwanamke lakini
bado unashindwa kuinasua akili yake? Kumfanya mwanaume akupende si jambo
gumu la kufanya, kile unachohitaji ni kutumia mbinu hakika ambayo
imefanyiwa utafiti na kuonyesha kuwa inafanya kazi mia kwa mia.
Tukirudia kutumia mbinu hakika ni kuwa kama team ya Nesi Mapenzi,
tumekuja na miongozo ambayo ikitumiwa vizuri basi bila shaka unaweza
kumfanya mwanaume yeyote akupende.
1. Kuwa machoni mwake
Kumfanya mtu akupende ni rahisi. Iwapo mara kwa mara utakuwa machoni
mwake itafikia wakati flani kuwa amekuzoea kiasi cha kuwa akienda mahali
asipokuona basi hasikii raha. Hii unafaa kuitumia kwa mwanaume
unayemzimia kwa kuwa karibu na yeye mara kwa mara. Mfano akienda library
kusoma, wewe unafaa uwe uko karibu naye, akiwa ameenda kula lunch
katika hoteli flani unaweza kupata kisababu cha kuenda naye nk ilimradi
muda wake mwingi awe anakutia machoni.
2. Jeuza mtindo
Baada ya kuona ya kuwa amekuzoea ama mmezoeana, kile unachotakiwa
kufanya ni kubadilisha mtindo mzima. Usipokee simu zake kwa muda wa siku
tatu, akikutext mjibu baada ya masaa matatu huku ukimwambia uko buzy.
Zile sehemu ambazo amekuzoea mnakutana pamoja usiwe ukienda mara kwa
mara. Kufanya hivi kutamfanya mwanaume kuvutiwa zaidi na wewe kwani
tayari ulikuwa ushamzoesha yeye kukuona mara kwa mara. Iwapo kama
mwanauume ataonyesha interest na wewe hapa basi fahamu kuwa umepiga
hatua kubwa kumfanya mwanaume huyu akupende. [Soma: Hatua za kufanya iwapo unataka mpenzi wako wa zamani arudiane nawe]
3. Mfanye specially kwako
Mfanye ajiskie maalum wako. Njia moja wapo ya kumfanya mwanaume azuzuike
kwako ni kumchukulia kwa njia ambayo kunamfanya yeye kujiskia ama
kujiona mtu maalum sana kwa maisha yako. Kama uko na marafiki ama katika
gumzo la watu, makinika kwake peke yake na kujihusisha na yale ambayo
ataongea. Mwangalie machoni bila kupesa huku ukimuuliza maswali ya
kepekee ambayo yanamlenga yeye.
Pia unaweza kujaribu maji mapya kwa kuonyesha azma ya kutaka kuyajua
maisha yake, vitu anavyovipenda na kutaka kujua urafiki wenu nk.
4. Kutana naye 'kibahati mbaya'
Kutana naye kibahati mbaya. Hii kutamfanya kufikia kana kwamba kuna
uunganisho kati yenu. Mfano kama umegudua ya kuwa anapenda kusoma gazeti
katika mkahawa flani mjini, unaweza kujipeleka hapo kimakusudi ilimradi
aone kuwa makutano yenu yalikuwa ni sadfa. Mfanyie saprize kwa
kushangaa kukutana naye hapo. Mwangalie vile atakavyofanyika wakati
ambapo amekuona. [Soma: Mambo wanawake hufanya ambayo huwachukiza wanaume]
5. Jirembeshe uonekane
Kujirembesha haimaanishi kujibadilisha vile ulivyo. La! Vile
unavyotakiwa ni kuhakikisha ya kuwa unakuwa nadhifu na msafi. Hakikisha
kuwa unavalia nguo zako za kawaida lakini zitie nakshi kiasi flani.
Mfano unaweza kuvaa bangili,shanga, vipuli nk. Pia jipulize marashi
mazuri (wanaume huwa wanyonge ikija maswala ya marashi ya wanawake).
Hakikisha haubadilishi tabia zako ili uweze kumfanya mwanaume akupende.
6. Onyesha uhuru wako
Jambo ambalo wanawake hukosea kwa wanaume ni ile tabia ya kutojitegemea
wao wenyewe. Tabia ambayo inachukiza mwanaume ni kuona mwanamke anapenda
kumtegemea mwanaume kama kupe.
Vile unavyotakiwa kufanya ni kuhakikisha kuwa unajitegemea wewe
mwenyewe. Muonyeshe kuwa wewe una maisha yako, vitu unavyopenda kufanya,
una marafiki zako na kuwa hutegemei yeyote katika maisha yako. Usiogope
kutoa maoni yako kuhusu maswala fulani. Amini usiamini, mwanaume
akikuona unatabia kama hizi atavutiwa nawe bila yeye kujielewa. [Soma: Tabia chafu za wanawake ambazo zinapendwa na wanaume]
NB: Hakikisha kuwa hauigi tabia za mtu yeyote. Kama unaona baadhi
ya kufanya mambo haya ni magumu, chukua muda wako wote wa kufanya
mazoezi ili mwishowe uweze kushika. Ukiiga tabia ambazo si zako ni
rahisi kugunduliwa na mwishowe utajiharibia mwenyewe kwa kuitwa feki.
Monday, August 20, 2018
Jinsi Ya Kumfanya Mwanaume Akupende -Wanaume Watashindwa Kujizuia
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

Ushuhuda Wangu wa Kutoka Moyoni 💖
ReplyDeleteBaada ya baba yangu mdogo kuniacha kwa miezi saba mirefu, nilikuwa nimevunjika moyo kabisa. Alinizuia kwenye mitandao yote ya kijamii, akaondoka, na hakukuwa na njia ya kumfikia. Karibu nikate tamaa, lakini ndani kabisa nilijua singeweza kupata mtu yeyote ambaye angenipenda na kunitendea jinsi alivyonitendea.
Siku moja, bosi wangu kazini aligundua jinsi nilivyokuwa na huzuni na akanitambulisha kwa Dkt. Dawn. Dkt. Dawn alisikiliza hadithi yangu na akaahidi kwamba mpenzi wangu angerudi kwangu ndani ya siku tatu. Kwa kweli, sikuamini mwanzoni—lakini kwa mshangao wangu mkubwa, siku ya tatu simu yangu iliita. Ilikuwa yeye! Alikuwa akilia na kuomba msamaha, akisema hataniacha tena.
Tangu siku hiyo, uhusiano wetu umekuwa na nguvu na uzuri zaidi kuliko hapo awali. Amekuwa akipenda na kunijali mimi na mtoto wetu, na sasa tunafunga ndoa katika miezi miwili tu! ❤️
Shukrani zote kwa Dkt. Dawn, ambaye kwa kweli alifanya jambo lisilowezekana liwezekane. Ninampendekeza kwa moyo wote kwa yeyote anayekabiliwa na changamoto katika:
Masuala ya uhusiano au ndoa
Ugonjwa au magonjwa
Matatizo ya utasa au bahati nasibu
Kesi za mahakamani au urejeshaji wa mali
Dkt. Dawn kweli hutatua matatizo kwa ufanisi na hurudisha furaha katika maisha ya watu.
Wasiliana na Dr. Dawn kwenye WhatsApp: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com