Wapo
wanawake ambao wamekuwa kwenye uhusiano kwa nyakati tofauti na na
wanaume tofauti na kuishia kuachwa. Marafiki ukweli ni kwamba hakuna
kanuni za moja kwa moja kwenye uhusiano, lakini angalau nivyema kuwa na
uelewa wa mambo ya msingi zaidi kuyafahamu ili kujipa uhakika wa ndoa na
boyfrend wako.
Wasichana
wanaoachwa wengi wao hujitathmini sana lakini hawaoni kasoro
iliyowaahanisha na wapenszi wao ambao awali walikuwa wakitangaza nia ya
kuwaoa mara kwa mara.
Inawezekana
yapo mambo mengi zaidi, lakini mambo haya hapa chini, ukiwa nayo
makini, unajisogeza kwenye uhakika wa kuingia kwenye ndoa na boyfriend
wako.
Kumkosoa sana
Baadhi
ya wananwake wana kasumba hii. Boyfriend wake huenda anazungumza jambo
au anachangia hoja fulani, yeye anamkosoa. Mbaya zaidi ukosoaji wke ni
ule wa ujuaji, wenye kauli za kutojali na kuonyesha ujuaji zaidi. Bahati
mbaya wananume kwa namna walivyoumbwa, kihulka hawapo tayari kuwa chini
ya wanawake na hawajisikii vizuri kuonekana hawajui. Acha tabia ya
kumkosoa mpenzi wako hata kama una uhakika kuwa anachosema si sahihi.
Lakini
kwa uhusiano mzuri, wenye urafiki, zipo njia nzuri za heshima za
kumkosoa mpenzi wako kwa hoja na siyo kumuonyesha kuwa ‘yeye si lolote’
bali hana elimu au uelewa wa jambo hilo. Mfano unaweza kumwambia, ‘Baby
lakini ujue unavyosema si sawa, lakini kwa ninavyojua mimi…’, kwa lugha
nzuri kama hii, mwanaume wako atakuwa tayari kukusikiliza na hutakuwa
umemjeruhi hisia zake kwa kukuonyesha kuwa hana uelewa wa mambo.
Kuwa mkali
inawezekana
mna mjadala fulani, zuia hisia zako na kuwa mkali, hasa kukaripiana.
Mwanamke anapaswa kuwa mnyenyekevu kwa mwanaume wake. Kitndo cha
kuonyesha ukali kwa boyfriend wako, kitampa taswira kuwa hata kwenye
ndoa mnayoiendea, kelele na kumshushia heshima ndipo kutakapotawala
uhusiano wenu, jambo ambalo litamfanya aondoe kichwani wazo la kufunga
ndoa nawe.
Kumlinganisha na wanaume wengine.
Epuka
kabisa kumlinganisha mwanaume wako na wanaume wengine. wapo baadhi ya
wanawake wana hulka hiyo. Wanapokuwa kwenye mijadala fulani au
kuelekezana kitu kinachohusu majukumu yao, hulinganisha. Hilo ni kosa
kubwa sana.
Utamsikia
mwanamke anasema ‘Jifunze kwa wanaume wenzako, ona Jumanne anavyofanya
kwa mpenzi wake Mayasa’. Kufanya hivyo ni kumuumiza mpenzi wako, lakini
pia kutapunguza mapenzi na mawazo ya kukuoa. Mwanaume anapenda kuwa
halisi, wa kipekee na asiyelinganishwa na yeyote. Mwanaume huamini
alivyo, yupo tofauti na mwanaume mwingine yeyote kwa kila kitu,
kumlinganisha ni kumfukuza mikononi mwako.
Usikubali faragha
Wanawake
wengi hawajaelewa hii, lakini ukweli ni kwamba ili kumpa mwanaume
mshawasha wa kukuoa jiweke mbali na mazingira yatakayorahisiha kukutana
kimwili. Ni vizuri zaidi ikiwa kwenye uhusiano wenu kati ya ahadi muhimu
iwe na ya kukutana kimwili mtakapokuwa kwenye ndoa.
Mwanaume
anaweza kusukumwa na kiu ya ngono tu, lakini akishakupata huenda
akakutana na vitu asivyotarajia na hapo ukawa mwisho wenu. Jiulize,
utajaribiwa na wangapi? Kama mwanaume atafanya sababu ya kukataa kwako
faragha kabla ya ndoa, kuhairisha ndoa na wewe, mruhusu aende salama
kuliko kugeuzwa wa ‘mpira wa majaribio’. Msimamo wako utamfanya aone
anakwenda kumuoa mwanamke mwenye heshima, anayejitunza na kuhifadhi
maadili.
Kama
bado unao usichana wako ni vizuri zaidi, lakini hata kama ulishafanya
kosa, siyo mbaya kuanza kujilinda kwa upya ili meisho wa siku uingie
kwenye ndoa ukiwa mpya kabisa kwa mumeo.
Acha kuomba sana pesa
Hili
limekuwa tatizo kwa wanaume wengi. ni kweli mwanaume ana wajibu wa
kumtunza mke wake, lakini asimgeuze mradi. Kwani kabla ya kuwa naye,
ulikuwa unaishije? Ulikiwa huli? Hununui manukato nk? jibu ni hapana.
Jenga
utaratibu wa kuvumilia ili akitaka kukusaidia fedha afanye yeye
mwenyewe na siyo kwa shuruti zako. ukiendekeza pesa sana, atakupiga
chini na kusubiri mwingine.
Mitindo isiyo na staha
Kwenda
na wakati kumetaka kuharibu wasichana wa siku hizi. Kuna mavazi ya
kubana au kuacha nusu ya sehemu ya mwili nje kwa kuamini ndiyo kuvutia –
siyo kweli. Ukiona mwanaume anakusifia kwa mavazi yako ya hovyo, ujue
hana nia ya kukuoa, anakutumia kama chombo chake cha starehe na siku ya
kuoa ikifika, atamtafuta mwanamke mwenye maadili.
Usiwe
hivyo, linda utamaduni wetu, heshimu uanawake wako kwa kuvaa mavazi ya
heshima na kutengeneza nywele zako katika mtindo unaokubalika.
SHARE NA MARAFIKI.
Tuesday, August 7, 2018
Usimfanyie Mpenzi Wako Mambo Haya Kama Unataka Akuoe
About Anonymous
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment