Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya
kimapenzi, kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba
zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata
udhaniavyo.
Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji
zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi
katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike
ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume.
Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani
suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa
zawadi.
Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo
itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili
yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo,
Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpenzi wako ni mtu wa
karibu jaribu kuchunguza ni kitu gani ambacho huwa anakipendelea sana,
Baada ya kupata majibu anza kufanya uchunguzi mwingine ni kitu ambacho
huwa anapenda kulizungumzia sana, baada ya kupata majibu, majibu hayo
yaweke katika halmashauri yako ya kumbukumbu. Na mwisho wa siku mnunue
kitu hicho kwani ndiyo zawadi itakayompendeza.
"Pia wakati mwingine maneno yangu sio sheria unaweza inanunua zawadi ambayo kiukweli unahisi fika itampendeza mwezi wako"
Hayo ni baadhi ya mambo machache ya kuzingatia katika kufanya uchaguzi
wa zawadi ya kumpa mpenzi wako. Kwani zawadi ni ishara upendo imara. Pia
imeshauriwa ya kwamba zawadi ni heri iwe ile ya kudumu kwani hii
hukumbukwa daima.
Pasipo kupoteza muda tuendelee kidogo kwa kuangalia japo kwa uchache umuhimu wa zawadi katika mahusiano ya ndoa.
1.Huimarisha uhusiano na kuongezeka mapenzi ya kweli
Pindi utoapo zawadi kwa mwenzi wako, mwenzi huyo hujihisi yeye ni wa
thamani sana mbele yako. kwani zawadi kutafsiriwa na mpokeaji kama ni
mtu wa thamani sana, mtu ambaye anapendwa kweli . hivyo pindi
ufanyapo kitendo cha utoaji wa zawadi yeyote ile kwa mwenzi wako,
hufanya mahusiano yenu yaimarike na si kuteteleka.
2. Humfanya mtu ajihisi yupo mahali salama.
Usishangae huo ndio ukweli, kama ulikuwa hauna kawaida ya kumpa zawadi
mpenzi wako basi anza kufanya hivyo mara moja. Kwani zawadi hutafsiwa
na mpokeaji ya kwamba yupo mahali sahihi. Hivyo ili kuweza kuudumisha
upendo wako na mwenzi wako jenga utaratibu wa kumpa zawadi mpenzi wako.
3. Zawadi huacha kumbukumbu.
Hakuna kitu ambacho huacha alama kubwa katika mahusiano kama zawadi.
Hivi hajawahi kukutana na mtu anamwambia ya kwamba kitu hiki alinipa
fulani? Bila shaka umewahi kukutana na mtu wa aina hiyo. Kama ndivyo
hivyo amini ya kwamba zawadi huacha alama katika mahusiano.
Na ili kuacha alama hiyo, kama nilivyosema hapo awali ua kwamba zawadi
ni lazima iwe ni ya kudumu. Pia kabla sijaweka nukta nikumbushe pande
zote mbili mvulana na msichana ana haki ya kutoa zawadi kwa mwezi wake.
Hivyo nikusihi ya kwamba ujijengee utaratibu wa kutoa zawadi kwa mwezi
wako.
No comments:
Post a Comment