Karibuni tena Wapendwa
2zungumzie mambo tofauti ktk maisha ya mwanaadam. Ni mara nyingine tena
2nakutana 2kizungumzia kuhusu Adhabu kubwa ya mpenzi anayekusaliti ktk
mapenzi. endelea ...
Wanaume wengi wanapobaini kuwa
wapenzi wao wanawasaliti, hutunisha misuli kwa kuonesha umwamba kwa kuwatwanga
makonde wapenzi wao au kuwafanyia mbaya wale waliowanasa. Lakini uchunguzi wa
wana mapenzi unaonesha kuwa ubabe haukomeshi tabia ya usaliti.
Kuna wengi ambao waliwafumania
wake zao, wakawapiga na kuwajeruhi, lakini wakajikuta hawakukomesha tatizo,
zaidi ya kuwapa usugu wapenzi wao wa kuendeleza wizi tena kwa dharau na kejeli
huku wakibembelezana kwa maneno haya: “mzushi kaenda kazini njoo sasa hivi
Mikosi Gesti” au “vipi yule bwege alikuuliza jana ulipochelewa kurudi”. Jamaa anaweza kumuuliza hivyo mke au mpenzi wa
mtu.
Katika hali ya kawaida usaliti
ni jambo linalouma kwa kiwango kikubwa. Katika mapenzi hakuna suala la
kuazimana mume au mke. Watu huazimana magari au pesa, lakini laazizi hakuna jasiri
wa namna hiyo! Hivyo ndivyo lakini, kupiga au kuachana baada ya kufumaniana
kunasaidia? Jibu hakusaidii, kwani ukimpiga adhabu inaishia hapo hapo,
kesho yake watakaokutana watakusaliti tena kupozana machungu.
Maamuzi ya kuacha naye
hayasaidii kwani ukimwacha mpenzi wako hujamtibu, utakuwa umetoa mwanya wa yeye
kuendelea kukusaliti na kukuumiza zaidi pale macho yako yatakapowaona
wameshikana mikono mitaani kwa uhuru na raha zao.
Ukiamua kuua na wewe utauawa,
huku wanadamu wenzako wakikucheka kwa uzembe wa kufikiri. Jamani usaliti upo
kila siku, si tunawaona wake na wapenzi wa watu wanaingizana gesti kila siku?
Hivyo, kama hujamfuma mpenzi wako leo kuna
siku utakutana na meseji kali akibembelezana na ‘kidume’ mwingine kwa
maeneo fulani. Utafanyaje baada ya kubaini hivyo, maana kama ni tukio
basi utakuwa umeona lile la stejini laivuuuuuu bila chenga. Twende pamoja ili
tuelimishane kama wadau wa mapenzi njia sahihi ya kufanya ili kumwadhibu mpenzi
msaliti.
Mwanzo wa yote, baada ya kuwaona uso
kwa macho wakisaliti penzi, unatakiwa kutoa ishara zitakazoonesha kuwa
umewaona, halafu ondoka eneo hilo. Ukifika home mtu mzima endelea kunywa maji
ili kupoza presha. Akirudi mpenzi wako jitahidi kumkaribisha kwa bashasha,
lakini usimuulize ulichoona mwache aendelee kujiuliza mwenyewe.
Au kama umenasa meseji za
kimahaba kutoka kwa mwizi wako, zitume kwenye simu yako kwanza, kisha baada ya
kumaliza uchunguzi wako mtumie tena sms hizo mkeo/mumeo. Ukifanya hivyo
usimuulize, endelea kumpenda na ikiwezekana ongeza matunzo. Nunua ‘mikuku’
akaange kila siku na umpe penzi moto moto.
Nakwambia ukifanya hivyo
mpenzi wako ataumia sana na hataendelea kukusaliti kwa kuwa atakuwa anawaza
unafikiria kumfanya nini? Na kwa yule uliyemshika naye, vivyo hivyo usizozane
naye, mwache! Utashangaa anahama eneo maana atakuwa anafikiri unamwandalia
kombora kumbe wewe wala, umeamua kujituliza tu!
Wadau wa mapenzi hii ndiyo
dawa ya mtu msaliti. Mwadhibu kwa upole, wanasaikolojia wameithibitisha adhabu
hii kuwa ina uchungu mara 1,000 zaidi ya kupiga au kukemea. Ukisema umwache
siyo dawa kwani unaweza kutafuta mwanamke/mwanaume mwingine naye akawa na tabia
zile zile, ikiwa ndivyo utaacha wangapi basi katika maisha haya?
Adhabu ya mpenzi anayekusaliti
ni kumnasa kwenye usaliti wake kisha kumpuuza huku wewe ukiendelea na mambo
yako kama kawaida, ukifanya hivyo utakuwa unamtibu ugonjwa wake wa kupenda
penda hovyo na hii ndiyo dawa hasa ya kumponya msaliti, lakini pia inasaidia
kupunguza maumivu ya penzi. Kumchunga na kumlilia machozi hakusaidii.
No comments:
Post a Comment