"Anajua kukutumia, anajua kukushika vilivyo kihisia za mapenzi na anajua
kukukamatilia vilivyo!, ila gharama alizonazo zinazidi bajeti ya
serikali!."
Tuseme kwenye muda maisha yako yana kila kitu kinaenda sawa, unasehemu
nzuri ya kuishi, unava vizuri, maisha yako yanaenda sawa na una uwezo wa
kujipatia chochote kile unachohitaji.
Sasa hivi umejipatia mchumba ila kila saa swali hili linakuingia akilini "Je ananipenda mie kama mie au anapenda pesa zangu?".
Hizi hapa ni dalili ambazo kiumeni.com imekukusanyia ili kujua iwapo
msichana uliyenae anakupenda kweli au anachokifuata ni ujazo wa pochi
yako na hela zako, misho wa siku akuache solemba na kukuumiza roho yako.
- Anataka zawadi za thamani...
Ukiwa unampa zawadi za kihisia ambazo hazina gharama zozote, ila zina
kumbukumbu flani ambayo ni spesho kwenu, kumbukumbu nzuri ya wakati
flani katika mapenzi yenu atakuangalia kwa jicho baya huku akielekeza
pua yake kwenye zawadi anayoitaka.
Wanawake waliopo kwa ajiri ya pesa huwa hawana hisia na zawadi zenye
umaalumu wa kipekee kwenye mahusiano ila wanapendelea zawadi
zilizopikiwa gharama na fedha.
- Marafiki zake wanaishi maisha ya gharama ya juu...
Kuna usemi usemao, "Utamjua mtu kutokana na iana ya marafiki
waliomzunguka", kama msichana wako anatumia muda mwingi na marafiki
wenye matumizi ya hali ya juu, ujue yupo nawe ili apate hio hela ya
kukidhi garama ya hayo matumizi anayoyataka.
- Ana hamasa kubwa ya kujua hali ya maisha yako kiuchumi...
Msichana
wako anakua anakuuliza sana maswali ya hapa na pale yenye marengo ya
kujua hali yako kiuchumi tokea siku ya kwanza upo nae, unaweza
kuchanganya maswali yake na kudhani anataka tu kujua mambo kuhusu wewe
kimaisha, hapa anataka kujua kama una uwezo wa kutosha wa kutimiza
mahitaji yake katika kipindi chote cha mahusiano yenu.
- Halipii bili hata siku moja...
Bili ikija mezani utamuona anakua bize na simu au kitu chochote kingine,
anakua hata haioni kama ipo pale, hawezi kujitolea hata siku moja
kulipia hata soda, ukiona hivyo ujue kakupenda kwa uwezo wako ulionao na
sio kitu kingine.
- Hajiamini mbele ya wanawake wengine wenye hadhi aliyojiwekea...
Siku zote anavaa vizuri kwa nguo za gharama, vito vya thamani na
aliyependeza, na anafanya vyote hivyo kwa kutumia pochi yako, na kwa
sababu kawekeza sana kwenye muonekano wake hapendi wanawake wengine
wanaomfanana au wenye hadhi ya juu kumshinda yeye, saa zote anakua
hajiamini wakiwepo karibu.
- Anatumia maumbile yake na muonekano wake kupata mahitaji yake...
Atafanya chochote na kutafuta udhaifu wako kwake na ana uwezo mkubwa na
ukufunzi mzuri juu ya mapenzi na anajua kuutumia vilivyo kukutoa hela na
anaweza fanya hivyo katikati ya kufanya mapenzi au baada kukwambia
baadhi ya mahitaji yake na shida zake.
Anatunza hadhi yake saa zote na anahakikisha inabaki pale pale kwa nguo
na vito vya thamani anavyovaa, huwa hapendi kuwa karibu na watu anaohisi
wana hadhi ya chini na hutumia kiburi chake na maneno ya kejeri
kuhakikisha wanakaa mbali nae.
Anaonyesha kupendezwa zaidi mwanaume anapoongelea maswala ya kifedha kuliko kitu chochote kingine.
- Anawapanda wapenzi wake...
Badala ya kupanda cheo, anawapanda wapenzi wake, ukiangalia historia
yake ya mahusiano kati ya mpenzi wake aliyopita na wa sasa, wa sasa
anakua na pesa nyingi kuliko yule wa zamani, anafanya hivi ili kukidhi
mahitaji yake ambayo yanakua yanapanda zaidi.
Ukimwona unajua kabisa kutokana na jinsi alivyo kwa muonekano wake ya
kuwa yupo nje ya ligi yako, ukimwangalia anakila kitu kizuri, na unaweza
kujiuliza anatafuta nini na mwanaume wa aina yako.
Ukiwa na pesa nzuri ujue yupo kuongezea zaidi hadi aliyoifikia kutoka kwako.
- Anahadhi ya kuwa na cheo...
Ukimwona unaweza sema anafanya kazi sehemu flani ila sio kiivyo!, yeye
yupo bize na starehe na kula bata kwa wingi, zaidi ya hapo hana kitu
anachofanya ila gharama zake ni za juu kushinda uwezo wa kipato chake na
anaujuzi mkubwa wa kutumia hisia zako kulipia kila kitu anachohitaji.
No comments:
Post a Comment