Mwanaume usijidanganye kuwa “Mimi
mke wangu hapendi vitu vizuri” hakuna kitu kama hicho, kila mwanamke
hupenda vitu vizuri na wanawake wengi hujali zaidi muonekano wao kuliko
kitu kingine chochote. Hii ndiyo maana hata kule kijijini ambapo binti
mdogo hana uwezo wa kununua viatu lakini ndala zake au yeboyebo
ataziosha vizuri ili kupendeza kuliko mtoto wa kiume ambaye hata kuoga
inakuwa shida.
Mwanamke anajifanya hapendi vitu
vizuri kwakuwa anajua uwezo wako na anakupenda. Mwanamke anayekupenda
akiona huwezi kumnunulia kitu flani atajifanya kutokukipenda ili tu
asikukwaze, lakini hamiaanishi kuwa hakipendi kitu husika. Kwasababu
hiyo basi kama mwanaume unapaswa kufahamu kuwa, kulingana na uwezo wako
hakikisha unamdekeza mwenza wako, kwani atakuvumilia tu pale anapojua
kuwa huna uwezo.
Niwanawake wachache sana ambao
watajua kuwa una uwezo mkubwa wa kuwanunulia vitu vizuri halafu
ukajifanya mbahili au ukasema hawapendi vitu vizuri halafu
wakakuvumilia. Atavumilia tu pale anapojua kuwa huna, kama unacho na
humdekezi atatafuta mtu wa kumdekeza na hapa naomba nifafanue kidogo,
“Atatafuta mtu wa kumdekeza..” kwa maana kwamba kwa mwanamke inakuwa na
maana zaidi kama akifanyiwa kitu cha kimapenzi na mwanaume.
Mwanamke mwenye uweo zakununua nguo
ya laki mbili hataipenda ile nguo kama atakavyopenda nguo ya elfu
hamsini aliyonunuliwa na mpenzi wake. Hivyo usione tu kwakuwa
anafanyakazi basi ukajisahau ukasema atanunua mwenyewe pesa anazo. Hapo
nisawa na kumuambia ajidekeze kitu ambacho hakina maana kwake, mdekeze
wewe hata kama ni kwa kidogo kiasi gani ulichonacho. Mpe vitu vya
kusimulia kwa mashoga zake na yeye aweze kusema “Hii kaninunulia baba
flani…” ajihisi naye ana mwanaume.
No comments:
Post a Comment