Uzazi wa mpango una mambo mengi sana.. sio kuzuia mimba tu
ndio uzazi wa mpango ila hata kupanga idadi na jinsia za watoto ni moja ya njia
za uzazi wa mpango..
Watu wengi wamekua wakitamani jinsia flani za watoto ili wazae
watoto wachache ila kukosa kwa jinsia waliyoipanga hujikuta wakizaa watoto
wengi wakati wakitafuta jinsia husika, mpaka familia hugombana na kutengana kwa
sababu hizi.
Mara nyingi wazazi wa kiume hufikia hatua ya kuvunja ndoa
kabisa hasa wanapokosa watoto wa kiume.
Leo ntamaliza kitendawili hiki kwa kutoa njia ambazo
zinaweza kufanya mtu kupata mtoto wa kiume kwa asilimia nyingi…
Kitaalamu mbegu
zinazotoa mtoto wa kiume XY huenda kwa mwendo mkali sana kwenda kwenye
mfuko wa uzazi lakini hufa haraka. lakini mbegu zinazotoa mtoto wa kike XX
husafiri taratibu na huchelewa kufika na kufa ndani ya mfuko wa uzazi kwani mbegu hizi
huweza kuvumilia hali mbaya ya kimazingira ndani ya mfuko wa uzazi wa mwanamke,
hivyo njia pekee ya kupata mtoto wa kiume ni kuhakikisha mbegu hizo za kiumeXY
zinakutana na mayai ya kike kwenye mfuko wa uzazi haraka kabla ya kufa..
Zifuatazo ni njia hizo tano kali…
1. Hakikisha unashiriki tendo la ndoa siku
mayai ya mwanamke yanapokua yameshuka{ovulation}
Ukishiriki tendo la ndoa siku hii ambayo
yai linakua limeshuka mbegu za kiume huweza kufika mapema na kujiunga na mayai
ya kike na kutengeneza
mtoto{fertilization}hii ni siku ya 14 KABLA YA KUONA DAMU YA MWEZI UNAOFUATA SIO BAADA YA KUONA SIKU ZAKO..
Kama
wewe mwanamke hujui siku yako ya ovulation fanya hivi.
Pima joto lako la mwili: nunua kipima
joto[thermometer} na kisha pima joto lako kila asubuhi , siku ukiona joto lako
limeongezeka kidogo ujue umeanza ovulation na hiyo ndio siku muhimu ya kutafuta
mtoto..
Angalia maji maji ya uke: kawaida maji ya uke
hua mazito na kuvutika kama maji ya mayai mabichi wakati mwanamke anapoanza ovulation..
2. Wewe mwanaume ongeza idadi ya mbegu
zako..{sperm count}
Mwanaume anatakiwa aongeze wingi wa mbegu zake hasa kwa kukaa siku mbili
mpaka tano bila kushiriki tendo la ndoa wakati akisubiri mwanamke wake aanze
ovulation.
Njia zingine za kuongeza mbegu ni
weka korodani kwenye hali ya ubaridi:kawaida korodani hutengeneza mbegu nyingi wakati wa hali ya ubaridi kuliko joto hivyo mwanaume anatakiwa kuepuka kuvaa nguo zilizobana sana, na kuwekalaptop kwenye mapaja
acha kuvuta sigara na kunywa pombe:wanaume wanaokunywa pombe na kuvuta sigara hua na mbegu kidogo sawasawa na wavutaji wa bangi..
matumizi ya dawa za cancer pia husababisha uzalishaji wa mbegu kidogo sana.
3. Tumia style za ngono ambazo zinahamasisha
muingilio mkubwa{deep penetration}
Hii huzipa faida mbegu za mtoto wa kiume{XY} kufika haraka na kufanya fertilization na upande
mwingine, muingiliano mdogo{shallow penetration}husababisha mbegu kumwagwa mbali na
mlango wa mfuko wa uzazi hivyo mbegu huweza kukutana na hali ya tindikali kwenye uke hivyo
mbegu za mtoto wa kiume kufa haraka na
kuziacha mbegu zinazotoa mtoto wa kike.{XX}.
4. Hakikisha mwanamke anafika kileleni:
Mwanamke anapofika kileleni hutoa maji mengi ukeni ambayo hupunguza wingi
wa tindikali ambayo ni adui wa mbegu
zote hasa mbegu za mtoto wa kiume XY ambazo hua haziwezi kuvumilia hali
ngumu ya kimazingira.
5. Usifanye tendo la ndoa kabla na baada ya
ovulation;
Kabla ya ovulation mbegu za mtoto wa kiume XY hufika haraka kwenye mfuko
wa uzazi kama kawaida na kukuta mayai ya
mwanamke hayajafika na kufa vivo hivyo baada ya ovulation..
No comments:
Post a Comment