Maisha
ya kimapenzi kila ikiitwa leo yanazidi kubadilika ujuzi uliokuwa nao
jana yawezekana wazi kabisa leo sio ujuzi kabisa ila ni kitu cha kawaida
kwa baadhi ya watu sasa chukua mda mfupi kusoma makala hii utajifunza
kitu
MMMH
mshaanza eti nimeisha ingia mama Chaunabe kitanga na njia nisiye na
bleki kwenye domo langu, wahenga wanasema kinywa cha mkubwa kinanuka
lakini maneno hayanuki. Najua maneno yangu ya shombo huenda
hayakufurahishi wewe ambaye kila kukicha unabadili wanaume na kuonekana
una hila.
Shutuuu
dada mwanamke tabia babu wee, mwanamke kujua mumeo anataka nini,
mwanamke kujituma kwenye kiwanja kifupi cha sita kwa sita.
Unasahau cha kumvutia mwanaume unakimbilia kuukoboa mwili nani kakuambia weupe mali? Basi mkaa usinge nununuliwa!
Tena leo nakazi na wewe, nani kakuambia weusi ni laana. Basi leo nataka nikuambie wewe usiye na haya uliyemaliza vipodozi mwisho wa siku uso unakuparama kama mchawi mzee, unalo hilo?

Siri ya weusi maana yake ni utamu hata zambarau tamu ni nyeusi, zabibu tamu ni nyeusi na hata usingizi mtamu unapatikana usiku mweusi. Huoni Mzungu akimuonja mswahili anachanganyikiwa.
Wewe
unajikoboa Mzungu ajipake masizi? Acha ubwege. Nimejikuta hata
nikisahau kuelezea nilichokikusudia kwa ajili ya malimbukeni wachache,
jivunie weusi wako babu wewe. Tuachane
na hayo ambayo kwa kiasi nimejikuta nikipandwa na mzuka na kuingia
kwenye mada nyingine. Kama unabisha mwangalie jirani yako anayetumia
mkorogo ngozi kama kuku wa mayai aliyezeeka
No comments:
Post a Comment