"Kama Waswahili wasemavyo, Hasira... Hasara!, Cheka uongeze siku."
Msongo wa mawazo ndo kitu kinachomtokea mara nyingi
zaidi na mara kwa mara kwa binadamu mtu mzima, ndo maana kuna misemo
kama, "Mtu mzima ni jalala la matatizo", na kwenye matatizo yanakuja
mawazo... na mawazo ya kisongamana ndo msongo wenyewe wa mawazo, sababu
za msongo wa mawazo hutofautiana kutoka mtu na mtu, kama msongo wa
mawazo unavyoharibu maisha yetu na kufanya tusifikirie vizuri ndivyo
hivyo hivyo kinachotokea hata kwenye miili yetu, na kufanya mifumo ya
mwili kudhurika kwa hali ya juu kama ifuatavyo...
Ukiwa na msongo kimwili au kiakili, mwili hubadilisha nguvu zake na
kuzielekeza kwenye mfumo wa kupigana, huhisi kuna tatizo kimwili ambalo
linatakiwa kupambana nalo na kusababisha ushilikiano wa mfumo wa neva
kutuma taarifa kwenye tezi ya adreno kutoa homoni ya adrenaline na
cortisol, homoni hizi husababisha moyo kwenda mbio, presha ya damu
kuongezeka, kasi ya mfumo wa umeng'enyo wa chakula nayo kuongezeka
pamoja
na kuongeza kiasi cha glukosi(sukari) kwenye milija ya damu, hali hii
inayosababishwa na msongo huisha mara baada ya hali ya msongo(stress)
kwisha.
Kukiwa na msongo(stress), misuli hupanuka, mvuto wa misuli kwa muda
mrefu husababisha uchovu, maumivu, kuumwa kichwa au kipanda uso na
athari nyingi nyinginezo.
Msongo(stress) hufanya mtu kutopumua vizuri
kwa kusababisha upumuaji wa kasi ambao husababisha mshituko wa maumivu ya kifua kubana kwa baadhi ya watu.
Msongo wa hali ya juu husababisha mapigo ya moyo kwenda mbio, misuli ya
moyo kuvutika na mishipa inayopeleka damu kwenye misuli mikubwa na moyo
kusinyaa na kusababisha kujaa kwa damu inayotakiwa kusambazwa sehemu
hizi za mwili, kuruddia rudia kwa msongo wa hali ya juu husababisha
kuvimba kwa mishipa hivyo kutokea kwa ugonjwa wa moyo.
- Mfumo wa homoni endocrini
Endocrini ni homoni nzinazomwagwa moja kwa moja kwenye damu
, mwili
ukiwa kwenye msongo sehemu ya ubongo inayoitwa hypothalamus hutuma
taalifa na kusababisha tezi ya adeno kutengeneza homoni ya cortisol
pamoja na epinephrine ambayo wakati mwingine huitwa "homoni ya msongo'.
INI
Baada ya homoni ya cortisol na epinephrine kutolewa, ini hutengeneza
glukosi(sukari) kwa wingi, sukari hii huenda moja kwa moja damuni na
kutumika kuupa nguvu mwili kwa ajili ya dharura.
Kwa baadhi ya watu msongo hufanya mtu kula zaidi au kutokupata hamu ya
chakula tofauti na ilivyo kawaida, msongo unaweza kukusababisha ule
chakula tofauti tofauti au uvute sigara kwa wigi, au
uzidishe utumiaji wa pombe na vileo na kukufanya uzulike kwa kiungulia,
au tumbo kujaa gesi, tumbo linaweza kupata maumivu au kutapika pindi
msongo ukiwa katika hali ya juu sana.
Kwa wanaume, homoni nyingi ya cortisol inayotolewa kwa shindikizo la
msongo huathiri ufanyaji kazi wa kawaida wa mfumo wa uzalishaji, msongo
wa hali ya juu husababisha homoni ya testosterone kutokufanya kazi
vizuri na kusababisha utengenezaji wa shahawa kuwa mdogo ambao
huleteleza ugumba wa muda.
Kwa wanawake msongo husababisha kuingia mara kwa mara kwenye hedhi na
tarehe kutokua za uhakika za kuingia kwenye siku zao au kusababisha
tumbo la hedhi kuuma sana na kupunguza hamu ya kufanya mapenzi.
No comments:
Post a Comment