"Tambua matatizo yako kwanza na elekeza nguvu na uwezo wako kwenye kutafuta jawabu".
Mara nyingi maisha hutupeleka sehemu ambazo hatuzielewi, tunahangaika na
tunashindwa kusonga mbele sababu ya kusahau vitu vidogo vidogo ambavyo
ndivyo vinabeba muhimili unaoshikilia uwezo wetu wa kukua katika
mafanikio, kiumeni.com imekuandalia ukumbusho wa kanuni zinazotufanya
tufanikiwe na kutujenga katika mafanikio.
#1; Wewe ni mtu pekee unaowajibika katika kutafuta na kujiletea mafanikio yako mwenyewe.
Sehemu bora na nzuri ya maisha yako itakuja pale utakapoamua na kujua
hayo maisha ni maisha yako na hakuna mtu mwingine anayeweza
kuyabadilisha tofauti na wewe mwenyewe, hakuna wa kumlilia, hakuna wa
kumtegemea tofauti na kujitegemea mwenyewe, kutakua na hali ngumu
zitakazo kusumbua ila ukiamini kwa moyo wako wote na kuongoza maisha
yako utafanya kile ambacho hutaamini unaweza na utashangazwa na uwezo
ulionao.
Usifate nani kafanya nini, unatakiwa ufanye maamuzi yako mwenyewe na kwa
sheria ulizojitengenezea mwenyewe na mafanikio yatafuata, mwanzo hua ni
mgumu na furaha sio kitu unachopaswa kuangalia kwa sasa, usikubali
kuishi kwa kiwango cha maisha ulichonacho sasa, badili hali yako kwa
kukataa na kuchukia mazingira uliyonayo sasa maana unaweza kuishi kwenye
hali nzuri zaidi kuliko hii ukifanya maamuzi ya uhakika, na siku zote
kumbuka mbuyu ulianza kama mchicha.
#2; Sio mpaka uvumbue dhahabu au kompyuta ndo ufanikiwe.
Kuwa na mafanikio hakuhitaji uvumbue kitu chochote, ukiwa na wazo jipya
na fikra chanya zenye maono ya kugeuza sababu na athari kuwa wazo la
kimaendeleo kwa kutumia mazingira yaliyopo inaweza kukusaidia sana, hata
hivyo unaweza kuvumbua kitu na bado ikawa njia ngumu kupata mafanikio,
ukiangalia watu wengi hasa waliopata mafanikio makubwa wengi wao
waliendeleza vitu vilivyopo kwa kuvipatia muonekano mpya ambao ulikuwa
haukufikiriwa hapo kabla au walitumia kitu hicho hicho kilichokuwepo na
kukipa mguso wa kipekee wa kimasoko na kikawaletea mafanikio makubwa
zaidi kwa kukiuza zaidi, ubunifu ni kuunganisha mambo, kuunganisha mambo
ina maana ya kutafuta msukumo kutokana na mawazo makubwa ambayo tayari
yapo na kuyafanya yawe na utofauti ambao mwanzo haukuonekana.
#3; Hakuna maendeleo bila matendo.
Jambo ambalo hujalianzishwa leo haliwezi kamwe kufanikiwa kesho, mawazo
mengi mazuri yameshindwa kufanikiwa kwa sababu wenye hayo mawazo
wameshindwa kuyafanyia matendo, jambo moja kuu la kuweka maanani,
mafanikio sio kitu cha kuonekana wakati bado hujafanya kitu, usitegemee
kitu kikubwa wakati bado haujakifanyia tendo lolote, anza kwa kulitenda
kwanza na kuwa na subira, ukishalianza hatua zinazofuata baada ya hapo
zikiwa na nia na kutendwa katika hali sahihi mafanikio lazima yaonekane,
kila kilichoanza kwa kutoonekana baada ya muda wa matendo lazima kianze
kuonekana na chenyewe.
#4; Uvumilivu hushinda.
Kama msemo wa kale unavyosema, "mvumilivu hula mbivu", maji ya mto
hupasua jiwe si kutokana na nguvu na kasi ya maji, ila inatokana na
ubishi na uvumilivu wa maji kupita sehemu ile ile, ukiwa mvumilivu hata
kama umeanza kwa kukosea mwisho wa siku utafanikiwa kwa chochote
unachofanya.
#5; Kufeli sio tija ya kuacha kujaribu.
Usije amka miaka sabini na tano na ukaanza kuhesabu kile ambacho
ungeweza kufanya ukiwa angali na nguvu za kukifanya, kama umeamua
kufanya kitu bora ufanye na si kutoa visingizio na kutumia uoga wako
kugeuza maamuzi yako mwenyewe, watu wachache sana hufanya kitu sahihi
kwa mara ya kwanza ila huendelea kufanya wanachofanya mpaka hapo
wanapokipatia, binadamu hawapai ila hutembea hatua moja baada ya
nyingine na hufika waendapo na hata kimawazo pia hufanya hivyo hivyo na
kutimiza malengo yao.
#6; Kuwa makini na kila kitu.
Ukiwa umetingwa na mawazo ya kuangalia nyuma na pembeni kwa kile ambacho
nafsi yako inahuzunika kwa kutokifanya na ukiangalia kwa umakini
unajikuta hukufanya kwa sababu ya woga, huu ndio muda wa kukifanya hicho
kitu, ila kuwa makini na ukifanyacho achana na hofu, hofu uliyonayo ndo
itakufanya usikifanye vizuri, kama wasemavyo "kunguru muoga hukimbiza
bawa lake".
#7; Mawazo chanya huleta uzalishaji.
Mawazo ndo usukani uendeshao maisha yetu kuelekea uelekeo flani, iwapo
mawazo yako yakiwa chanya basi na maisha yako pia yatakuwa endelevu na
iwapo mawazo yakiwa tofauti, mawazo hasi basi ujue hapo maisha lazima
yakushinde na kukuendea kombo, ndo maana kiumeni.com tunaamini mafanikio
huanza kichwani kwa mawazo endelevu na hushuka moyoni kwa nia iliyo
madhubuti.
#8; Unatakiwa uwamini unaweza.
Jambo la kwanza na siri kubwa ya mafanikio ni kiasi gani unajiamini,
mafanikio huanza na ndoto na ili matendo yazae matunda lazima ujiamini
asilimia mia ya kuwa unaweza na kujua unachokifanya.
#9; Kusaidia wengine ndo moja ya sehemu ya kuwa na mafanikio.
Watu waliofanikiwa daima huja na mawazo mapya na njia bora za kuwasaidia
wengine, hii ikiwa na maana iwapo ukiweza kusaidia wengine, hayo hayo
mawazo endelevu ndio yatakusaidia na wewe pia kukua katika mafanikio,
mafanikio yako ya muda mrefu yanatokana na jinsi unavyonufaisha jamii
ikuzungukayo.
#10; Mafanikio ni safari ya hatua zisizohesabika.
No comments:
Post a Comment