"Kuondokana na mawazo ya mpenzi wako mlie achana ni moja kati ya vitu
vigumu sana, kuachana ni kitendo cha dakika ila hisia huwa haziondoki
papo hapo"
Hisia huchanganywa zaidi na vitu mlivyokua navyo na kutumia wote kwa
pamoja kama mapenzi, sehemu mlizokua mmezoea kwenda wote na hata sehemu
mliokua mkilala pamoja, labda kitu kinachoumiza kichwa zaidi hata kama
ilikua lazima uhusiano kuvunjika iwe kwa kumfumania au la, ni ugumu wa
kuondoka kwa hisia ulizonazo pamoja na kumbukumbu za maisha yenu
mlivyokua wapenzi na kuendelea na maisha ya kawaida.
kiumeni.com tumekutafutia na kuweka pamoja njia ya kukurudisha na
kuondokana na mvunjiko wa moyo na hisia katika kipindi hiki kigumu cha kuachwa na kukurudisha katika hali ya kawaida ya maisha...
- Mtoe kwenye hio nafasi uliokua umemweka...
Kitu cha kwanza acha kuhisi kuwa mpenzi wako huyo alikua ni zawadi toka
kwa Mungu, maana najua unajua kabisa alikua hajakamilika, na kama tukiwa
wa kweli hakuwa anafikia hata karibu ya kitu kizuri na mapungufu yake
ni mengi ndo maana mpaka sasa hivi uko kwenye hii hali, tengeneza orodha
ya vitu na tabia zote ambazo ni vibaya kuhusu yeye na karibisha rafiki
zako wakusaidie.
- Hakikisha wakati mnaachana makubaliano ya pande zote mbili yamefikiwa...
Kuwa na uhakika kwamba mmesha achana na hamuwezi kurudiana tena na ndo
mwisho wa mahusiano yenu na wala sio likizo inasaidia sana kukutuliza
hisia na kuondokana na matumaini hewa, na kama kuna kitu chochote cha
kuweka sawa ungeweka sawa sasa hivi maana ndo mwisho wa ukurasa wa
uhusiano.
- Usijaribu kumpigia simu...
Hata kama ukimpigia simu haito saidia, sana sana utakua unajiumiza moyo
kwa hisia unazozisababisha, na hii ndo nguzo kubwa ya kutumia ili
undokane na mpasuko wa moyo, baada ya kuwa nae kwa kipindi kirefu namba
yake ndo namba ulioipiga mara nyingi zaidi, kwa hio kwa vyovyote vile
hisia zitakua zinakutuma kwa hali ya juu ili ufanye hivi, cha kufanya
hakikisha umeifuta namba yake, na kama ukimpigia simu utajikuta
unajiongezea miezi ya kutomsahau na kuumia kwa msongo wa mawazo, na mtoe
kwenye orodha ya marafiki zako wa facebook, fikiri ukiwa facebook
ukaona picha yake akiwa amekumbatiwa na mwanaume mwingine, nadhani
unakiona kwanini mwanzo mpya ni muhimu.
Bila mpenzi wako kukushika mkia, sasa hivi una muda wa kutosha kufanya
mazoezi na kujiweka mweili katika hali nzuri, mazoezi ni mazuri kwa afya
yako na ni njia nzuri ya kuondokana na hisia, ukiwa na mwili mzuri ni
kitu kizuri cha kuvutia wasichana wapya.
- Kaa mbali na marafiki zake pamoja na sehemu anazopendelea...
Kama unataka kuondokana na hisia zitokanazo na kukutana na mpenzi wako
wa zamani kwa mda huu, inabidi ujitoe kwa baadhi ya mambo, inabidi ukate
mawasiliano na baadhi ya marafiki ambao wapo upande wake na kuachana
kabisa na baadhi ya sehemu mlizokua mnapendelea kwenda. Ni vitu vidogo
kuvitoa kama utakuwa unahitaji pumziko la hisia, mawazo na akili yako
kwa ujumla.
- Tupa mbali kumbukumbu zozote zinazokukumbusha wewe na yeye...
Hilo doli, kadi na hayo maua aliyokupa kwa ajili ya siku yako ya
kuzaliwa, hilo shati alilokununulia, hizo picha zilizotoka vizuri za
yeye na wewe, ondoa zote na eiza uzitupe au uweke mbali, utavyoharakisha
kutoa hivyo vitu ndo utakavyo sahau kwa haraka zaidi na kabla hujauliza
"ndio", unaweza acha vitu ambavyo havikuletei hisia yeyote, ila nguo
zake, vito vya kuvaa na vingine vyovyote vinavyo kukumbusha mbali
viondoe.
- Usijaribu kufata vitu vyako...
Usijaribu kufata vitu vyako, nguo, cd na kila kitu kingine, jaribu
kuviwazia kama umevipoteza, iwapo ukiviendea utajisababishia mjazo wa
hisia usioutaka, jaribu kukaa mbali nae kwanza kwa sasa, ni bei rahisi
kulipia kuliko kwenda na kumkuta anamawazo au hasira na kusababisha vitu
vingine ambavyo ungeviepuka kama usinge kwenda.
- Tumia muda na marafiki zako...
Mapenzi hutusahaulisha marafiki, tunakosa mda kabisa wa kutumia pamoja
na marafiki maana wapenzi wetu hututaka tutumie muda zaidi na wao,
lakini sasa hivi upo singo ni vizuri ukatumia muda wako na washikaji, na
kufanya mambo yanayo kuburudisha, ukitumia muda upo bize na mambo ya
kukufurahisha huwezi pata muda wa kumuwaza tena.
- Kumbuka mambo mabaya kuhusu yeye...
Hisia hazikimbiwi, hata zikipita siku baada ya kuachana, unaweza
kujikuta unaanza kumuwaza, cha kufanya ukijikuta hivyo anza kufikiria
mabaya yote kuhusu yeye, nyakati alizokua anakuboa, jinsi mlivyokua
mnagombana, tabia zake ulizokua huzipendi, hii itakusaidia kuondokana na
hisia za kumkumbuka.
- Tumia vyema uhuru wako ulionao sasa na jiachie...
Mahusiano huwa ni kijitoa na kujifunga ili kumfurahisha mpenzio, kuwa
singo kunatakiwa kuwe juu ya kujirusha na kujiachia na kufanya kitu
chochote ambacho unajisikia kufanya, kama ni kwenda klabu, nenda. Fanya
yote na rudisha furaha yako na msahau kwa yote mabaya alionayo.
- Fanya mapenzi na msichana mwingine...
Moja kati ya njia zilizo na uhakika zaidi kufanya kazi ni kufanya mapenzi
na msichana mwingine, maana sababu kubwa inayotufanya kutoachana na
hisia za mpenzi wa zamani ni hofu jinsi ya kumpata msichana mpya, ndo
kitu kikubwa kinachoturudisha nyuma kwenye mazingira tuliyoyazoea.
Kumtafuta msichana mpya au upendo mpya hata kama ni wa siku moja ni njia
nzuri ya kuondokana na mvunjiko wa hisia.
No comments:
Post a Comment