"Unatakiwa uwe na subira japo unahamu kubwa, angalia usije ukaharibu na
usimtongoze msichana hapo hapo, kinachotakiwa ni kufuata masharti madogo
na uwezo mkubwa wa kuangalia na kutafakari..".
Facebook ndio habari ya mjini..., kila mtu yupo na kila msichana mzuri
au mbaya, hata yule wa kwenye ndoto zako anaitumia, na ni sehemu iliyo
na wasichana wengi zaidi waliounganisha na mtandao mmoja kuliko mtaani,
mashuleni na maofisini. Na kizuri zaidi kupita yote hayo, hata kama uwe
na aibu ya kutongoza kiasi gani, face buku huwezi kutetemeka hata
ukucha, unachotakiwa kujua ni mpangilio kwanza ili uweze kuwavutia
wasichana wa kila aina.
Facebook ni msitu wa wasichana, kwa hio inakupasa kuwa na subira japo
kuwa unaham kubwa, angalia usije haribu na usimtongoze msichana papo
hapo, kinachotakiwa ni kufuata masharti kidogo ambayo
kiumeni.com inakupa na uwezo mkubwa wa kuangalia na kutafakari...
Futa picha zako zote zile mbaya na ambazo haziitajiki, kwa mfano zile
ulizopiga baa na vimada tofauti tofauti, na sidhani kama ulitakiwa
uziweke intaneti kila mtu hazione!, hakikisha umetoa picha zote za
wanawake wakiwa watupu hata kama ulikua umezishea tu, maana zinaleta
muuonekano mbaya kihisia na zinamwonyesha msichana kwamba wewe sio mtu
mzuri
wa kuanzisha mahusiano naye, zifute na zile ambazo
umejipiga mwenyewe, kwa vyovyote vile hazikuonyeshi ukiwa mtanashati,
hakikisha zimebaki za kwako peke yako na hata kama za marafiki zisiwe na
hisia zozote ambazo zinaweza kumfanya msichana hahisi hujatulia.
- Tengeneza marafiki zaidi...
Ukiweza kupata marafiki wengi zaidi, ndivyo utakavyo kuwa unaongeza wigo
mpana zaidi wa kumpata na kumchambua yule mwenye mvuto zaidi uliokua
ukimwota kwenye ndoto zako, kwa hio kama kiumeni.com tunavyokushauri
hakikisha unajiunga na marafiki wengi zaidi uwezavyo, tafuta hata wale
uliosoma nao zamani na jiunge kwenye magrupu ya facebook ili upate
marafiki zaidi.
Kama ukiwa umeweza kujiunga na marafiki wengi, utakua na nafasi kubwa ya
kumchambua yupi unaemtaka, angalia komenti zote zinazopita pamoja na
picha mbali mbali zinazopita, ukimwona yule aliyekushika macho na hisia
kakomenti, hata kama kakomenti kwenye komenti ya rafiki yako, na wewe
komenti hapo hapo na hakikisha umeweka na komenti tata juu yake ili
apate sababu ya kukujibu wewe, na kama hajatoa maoni, tafuta rafiki
unayemjua aweze kukutambulisha kwake, muulize rafiki yako kiungwana kwa
mfano... "Mambo, nimemwona msichana mrembo rafiki yako Angel, unaweza
kunitambulisha kwake?", hili swali lipo moja kwa moja na sidhani kama
anaweza kataa kukutambulisha.
- Mtumie mwaliko wa kuwa marafiki...
Kwa hio kama mmeweza kukomenti hapa na pale pamoja, sasa hivi atakua
ameshakujua, mtumie mwaliko wa kuwa marafiki, kuna asilimia kubwa sana
lazima akubali, na mkisha kuwa marafiki sasa unaweza kuanza kukomenti
kwenye maandiko yake na picha zake, pia mnaweza piga stori za hapa na
pale kwa kuchati, baada ya maendeleo kwenda vizuri na mazoea yamekua ya
kutosha, unaweza mwomba siku moja muweze kutoka wote mtoko!.
- Vuta subira na kuwa jasiri...
Iwapo ikitokea asipokujibu, japo ni mara chache sana iwapo umefuata
maelezo vizuri ya kiumeni.com, usije chukulia haraka na kukurupuka,
usimuulize chochote kuhusu hilo, endelea na stori, mpe muda na subiri
tena wakati mwingine mwafaka wa kumba mtoko tena.
Ili kuongeza mafanikio unaweza fanya kwa msichana zaidi ya mmoja, maana samaki ni wengi sana baharini.
No comments:
Post a Comment