"Wanasayansi wamethibitisha mawasiliano ya watu wanaokutana kwa mara ya kwanza hutegemea zaidi ishara za kimwili, ambapo asilimia 55% huwa ni kwa kutumia ishara, asilimia 38% yakiwa maongezi ya kutumia sauti pamoja na asilimia 7% ikiwa vitu ambavyo haviendani kabisa na unachokiongea."
Utafiti uliofanywa na chuo kimoja kikuu nchini Marekani, imebainisha
kama ukitaka kujua iwapo mwanamke amevutiwa na wewe, inabidi uangalie
zaidi ishara kuliko maongezi, na hii kuhitimisha wanawake huongea
tofauti na wanachomaanisha. kiumeni.com imekuandalia ishara kumi
zilizothibitishwa na watafiti pamoja na wanasayansi ambazo mwanamke
hufanya pindi anapovutiwa na wewe akiwa anajijua au hakiwa hajijui ili
kukuonyesha kama amevutika nawe.
Jifunze ishara hizi na maisha yako ya kimahusiano yatabadilika kwa hali ambayo hautaitarajia.
#10; Anashika au kupikicha nywele.
Kwa zaidi ya miaka 40, watafiti wamenyumbuisha tabia wanazozifanya
wanawake kukujulisha wamevutiwa na wewe, iwapo mwanamke akizishika shika
nywele zake kwa muda mfupi inaweza kuwa ishara ya kukupa taarifa ya
kuwa anafurahia uwepo wako, ila akiendelea kuzichezea kwa muda mrefu
inawezekana akawa katika hali ya kutokujiamini au hakuamini wewe.
#9; Anauma midomo yake.
Tabia hii mwanamke huifanya ili kuhamisha fikra zako kuelekea kwenye
midomo yake, inaweza maanisha ukienda na ukiwa mchombezaji mzuri mabusu
yanaweza kuwa ya kufikia, inabidi uwe mwangalifu sana wakati wa
kuitambua hii tabia na akiwa anauma midomo yake kwa muda inamaanisha
amevutiwa nawe ila kuuma midomo mara kwa mara inaweza onyesha ndio
mazoea yake, kwa hiyo kuwa makini kutofautisha kati ya hizo tabia mbili.
#8; Anacheka cheka, kukusumbua na kukuangalia kwa macho mazuri.
Hii tabia zipo pande zote mbili, hata wanaume pia huifanya ila kwa
wanawake wanaweza pia kuitumia ili kukujua nia yako kwao, kwa hio
usiichukulie kwa haraka sana inawezekana anakujaribu tu.
#7; Anakukaribia sana kimwili.
Ukaribu tunao karibia watu inategemeana na mahusiano yetu kwao,
ukimkaribia mtu sana huwa mara zote ni katika hali ya upendo, kwahio mwanamke
akikukaribia sana inawezekana akawa anafanya hivyo ili upendezwe naye
zaidi, inabidi kabla hujafanya maamuzi yeyote hakikisha umehakikisha
mkaribio wake kwako sio wa hali ya kikawaida, na unaweza hakikisha kwa
kusogea kidogo ili kumtegeshea kama atasogea tena huku ukiwa na tabasamu
usoni.
#6; Anachangia unachozungumza na kuongelea kuhusu mambo yake binafsi.
Baada ya kufanya mazungumzo kwa muda na kunoga, jaribu kupeleka mambo
mbele kwa kuanzisha mada ambayo inahusu maisha yako binafsi ila
hakikisha mada isiwe ya ndani sana na isiwe inaelekea kana kwamba
unataka kumjua kwa undani na maelezo yake yasiwe yanamlenga, hii
itamfanya ajisikie huru na kutokuogopa, iwapo mambo yakienda vizuri na
amevutika nawe utaona na yeye anachangia kwa kutoa mada inayohusu mambo
yake binafsi, watu huwa wanaongea kuhusu mambo ya ndani kwa watu
wanaowapenda na kujisikia huru mbele yao.
Iwapo maongezi haya mkiyafanya huku mnakula chipsi kwa pamoja itafanya
mambo yaende vizuri zaidi, kutumia vitu pamoja huongeza ukaribu na
maelewano zaidi.
#5; Anakua na urafiki wa kimaongezi wakati mnaongea.
Sahau kuhusu mistari ya kutongozea
ulioifanyia mazoezi, ikija kwenye kuangalia hamasa ya mwanamke kwako,
huangalii jinsi unavyomsifia, unaangalia mapokeo ya maneno unayomwambia,
mwanamke akikujibu hata kama kwenye hali ya kukataa jambo, akikujibu
kwa sauti ya upole na laini ujue amependezwa nawe, kwahiyo usiwahi
kuondoka kutoka katika mazingira hayo au sehemu hio, ila akikujibu kwa
sauti ya ukali, tafuta pakutokea.
Ili kuondokana na kupoteza muda kutongoza
mwanamke ambaye havutiwi na wewe, jaribu kwa kuanza na maswali rahisi
ambayo majibu yake ni rahisi, kwa njia hii utajua kama kapendezwa na
wewe au vipi, kama hajapendezwa na wewe utaona anakuondoa kwenye
maongezi ila aliyependezwa na wewe ataendelea na maongezi.
#4; Anakua katika mkao wa mwaliko kimaongezi.
Mwanamke akiwa amependezwa na wewe huwa anakua amekaa mkao wa mwaliko wa
kimaongezi, akikuangalia anakua na macho ya kiurafiki na si ya ukali na
hata ukiwa mbali utajua kwamba pozi na macho yake vinakuita.
#3; Anakua na ishara unazozifanya wewe.
Mwanamke akipendezwa nawe, atakua anajibu mapokeo ya ishara zako
unazotoa, kwa mfano ukitabasamu na yeye utamuona anatabasamu vile vile,
ukicheka na yeye atakufatiliza hivyo hivyo.
#2; Anapindisha kichwa kidogo na kutabasamu.
Watafiti wamebainisha mwanamke akipindisha kichwa kidogo na kuachia
sehemu ya shingo yake kuonekana kidogo ikifuatiwa na tabasamu mara
nyingi anakua amevutiwa na anachokiangalia.
#1; Anachezesha macho.
Kukutanisha macho ni kitendo cha ukaribu kwa binadamu, kurudia rudia au
kuendeleza kukutanisha macho huwa kuna maana kuu mbili, kwanza kuonyesha
hali ya mguso kihisia, na pili kuonyesha hali ya jazba.
Ili kujua kama analo hitaji la kuongea nawe, angalia jinsi
anavyochezesha na kukutanisha macho na wewe, utakuta mnakutanisha macho
zaidi ya mara kadhaa na kukiwa na tabasamu nyingi, kama ukiona
mmekutanisha macho halafu akaacha kukuangalia tena jua huyo hajavutika
na wewe, na isiwe na shaka sana maana mara nyingi kitu hichi huweza
kutokea bila ya wewe kukitambua.
No comments:
Post a Comment