VIJANA wenzangu, natumaini mnaendelea vyema na shughuli zenu za kila siku katika ujenzi wa taifa na jamii, au siyo?
Hapa nazungumzia mada inayosema ‘Kupoteza Bikra’. Mada hii imetokana na
maswali mengi ambayo nimewahi kuyapata kutoka kwa wasomaji wangu,
hususan wasichana, ambao wanasema; “Brother Danny, sijawahi kukutana na
mwanamume, lakini siku niliyokutana naye, damu haikutoka.
Hii imenipa wakati mgumu kwa mume wangu ambaye nilimwambia kwamba mimi
ni bikra na sikuwa tayari kukutana naye mpaka tulipofunga ndoa, sasa
anasema kwamba nilimdanganya. Tatizo ni nini?” Hili ni moja kati ya
maswali mengi ninayoyapata.
Kwanza kabla sijaendelea, ningependa kufafanua bikira au mwanamwali ni nani, na ubikra ni nini. Bikira ni
mtu yeyote, msichana au mvulana, ambaye hajawahi kufanya tendo la ndoa
hata mara moja. Kwa hiyo basi, ubikira ni hali ya mtu kutokutana kimwili
na mtu wa jinsia nyingine. Nadhani hapo wasomaji wangu mnaweza
kunielewa japo kwa ufupi.
Nini maana ya kupoteza bikira?
Hili ni swali zuri sana. Kama nilivyosema hapo juu; wewe unakuwa bikira
mpaka pale utakapokuwa umefanya tendo la ndoa na mtu wa jinsia tofauti.
Hata hivyo, tafsiri hii huwaacha watu wengi wakiwa njia panda.
Wakati watunga sera kwingineko duniani wanatafsiri ndoa kwa kueleza
kwamba hata kufanya ngono na mtu wa jinsia yako (kama mashoga na
wasagaji) kunatoa bikira yako, labda ungekuwa wakati muafaka wa
kuangalia kwa undani nini maana ya bikira.
Wakati tunapozungumzia bikira, tunafikiria kuhusu “ndoa haramu za
Wazungu wanaopendelea ushoga na usagaji” ambao wanatafsiri ngono kama
kigezo cha jinsia. Lakini ukweli ni kwamba, tafsiri muafaka ya ubikira
inakufanya uone kwamba kufanya vitendo mbalimbali vya ngono kungeweza
kukufanya ukajiita bikira wakati siyo kweli.
Kwa nadharia, chini ya tafsiri ya jadi ya ubikira, mtu ambaye
anajihusisha na vitendo vya ushoga (kwa mwanamume) na usagaji (kwa
mwanamke) anaweza kufanya ngono kila siku na bado akawa bikira. Mtu
anayefanya mapenzi ya bila kujamiiana (oral sex) kila mara pia ni
bikira. Kuna ukweli wowote katika hili? Nadhani hapa kuna upungufu.
Tafsiri nzima ya ubikira kwa hakika inahitaji kuandikwa upya. Labda
kabla sijaendelea zaidi, wacha niwatoe shaka wale ambao hawajawahi
kufanya mapenzi lakini siku ya siku wakajiona kwamba hawana bikira.
Bikira inaweza kutoka kwa njia nyingi zaidi ya kufanya mapenzi. Msichana
anayeshiriki michezo mbalimbali anaweza kuitoa bikira yake. Au kama
anabeba mizigo mizito, au ana matatizo kwenye tumbo la uzazi na wakati
wa ‘period’ anatokwa na damu sana, na mambo mengine kadha wa kadha
yanayoweza kufafanuliwa kwa kina na wataalamu wa afya.
Ubikira ni hali ya kutokuingiliwa kimaumbile, yaani kwa viungo vya uzazi
vya kiume na vya kike, lakini inaweza ikawa na tofauti kwa namna fulani
pia. Kama mvulana au hajawahi kufanya mapenzi na mwanamke, lakini akawa
anajichua, ama anafanya mapenzi kinyume cha maumbile; awe basha au
msenge, hakika hawezi kujiita bikira. Atajiita bikira kinadharia tu,
lakini kivitendo siyo bikira kwa sababu raha ama karaha ya tendo la ndoa
anaijua!
Kwa hiyo basi, kabla ya kueleza tafsiri mpya, fikiria katika mambo haya
yafuatayo na uyatafakari jinsi yanavyoweza kusimama katika suala zima la
ubikira.
* Mtu aliyebakwa au kutomaswa huwa siyo bikira tena?
* Hivi ngono ndiyo njia pekee ya kuangalia ubikira wa mtu?
* Kama utajihusisha na vitendo vingine vya mahaba, lakini si vya kuingiliwa kimwili, ni busara kujiita wewe bikira?
* Utatafsiri vipi kupoteza bikra yako kama wewe ulikuwa/au bado ni msagaji au shoga ama wa kawaida?
* Kuwa bikira kunaegemea kwenye hisia zako, shughuli zako, au vyote kwa pamoja?
* Kuna jambo lolote la kihisia katika kupoteza bikira yako, kwa maana
kwamba kama utafanya mapenzi na mtu na ukashindwa kuona dalili za bikira
kutoka au tofauti yoyote?
Tafsiri mpya...
Napendekeza kwamba ubikira una pande mbili. Nadhani kuna ubikira wa
kihisia na ubikira wa kimwili. Nadhani kama kweli mtu anataka asiwe
bikira anatakiwa kuachana na mambo yote ya kihisia kuhusu ubikira na
kujihusisha na vitendo vya ngono kimwili.
Katika tafsiri yangu hii, kitendo chochote cha ngono kinachohusisha watu
kuchojoa nguo na kusisimkwa mpaka kufikia mshindo hata bila kuingiliana
kimwili basi ni ngono. Nadhani kuwa uchi na kusisimuana ni ‘hatua
ambayo haina kurudi nyuma’, siyo kuingiliana kimwili.
Haijalishi kama kitendo hicho ni cha mwanamke na mwanamume kwa asili au
ni cha wanaume kwa wanaume (mabasha na mashoga) au wanawake kwa wanawake
(wasagaji), kama utashirikiana mwili wako na mtu mwingine, au kama
utampa raha ya kimahaba mtu mwingine mpaka akafikia mshindo na kutoa
manii au ukiwa na madhumuni atoe manii, basi umefanya ngono.
Pia nadhani kwamba ubikira siyo kitu fulani ambacho ‘unapoteza’ au
‘kinachukuliwa’, bali kitu fulani ambacho unashirikiana na mtu mwingine,
mara moja tu katika maisha. Kama hukumpatia mtu mwingine, basi
utaendelea kujihesabu kama ni bikira.
Nadhani watu ambao wamebakwa au kutomaswa bado wataendelea kuwa bikira
katika hisia hata kama miili yao imefanya mapenzi. Hawajakoma kuwa
bikira, na wala hawajawahi kufurahia na kuijua raha ya hisia za
kimapenzi ambayo huenda sambamba na kuutoa mwili wako kwa mahaba kwa mtu
mwingine.
Kama bikira yako imetolewa na mtu mwingine kwa mabavu, japokuwa ni kwa
kufanya mapenzi kimwili, sidhani kama ni busara kusema kwamba wewe si
bikira tena. Bado utaendelea kujichukulia kana kwamba hujawahi kufanya
mapenzi, bado utaona ngono kama kitu kigeni kwako.
Kuwa mwathirika wa kubakwa hakuwezi kukakulazimu uishi na alama ambayo
hukuiomba au kuitaka. Ubikira siyo kitu ambacho mtu anakipoteza kwa
bahati mbaya, kutokuwa bikira ni jambo ambalo mtu analichagua mwenyewe.
Mtu aliyebakwa na kwa bahati mbaya akapata mimba, bado kwa fikra zake
ataendelea kujiita bikira, na hilo linaweza lisiwe kosa kwake! Haijui
raha ya mapenzi, hajui maana ya mapenzi, mpaka pale atakapoamua mwenyewe
kwa nafsi yake kwamba anahitaji kufanya mapenzi, ndipo anapoweza
kuamini akilini mwake kwamba si bikira tena!
Nini kinachokufanya uwe bikira?
Nimekwishaeleza tafsiri halisi za ubikira. Lakini unapozungumza na watu
kuhusu suala hili, unagundua kwamba kuna mambo mengi yanayojitokeza
katika ‘mapenzi kwa mara ya kwanza’ ambayo yana umuhimu kimwili,
kihisia, kiakili, na hata kisiasa.
Inaweza kuwa si rahisi kusema kwamba ubikira siyo tafsiri rahisi kama
tunavyosema sasa, hivyo ngoja tuangalie mambo machache ambayo yanaweza
kusaidia katika uelewa wetu:
Tafsiri ya kale
Tafsiri inayojulikana zaidi ni kwamba bikira ni mtu yeyote ambaye
hajawahi kufanya mapenzi na mtu wa jinsia nyingine. Hata tafsiri hii
inaonekana kupwaya, kwani ukiangalia kwa undani utagundua kwamba hili
lilikuwa ni suala la kimwili zaidi, au la kitiba.
Mwanamke mwenye uke uliobana (intact hymen) alikuwa anachukuliwa kwamba
bado bikira, na huo ndio ulikuwa mwisho wa mjadala. Wanawake katika zama
za kati, kwa mfano, walikuwa wanachukuliwa kwamba ni bikira kama
walikuwa na uke unaobana. Kama mwanamke alikata ‘utepe’ (hymen) wakati
amepanda punda au kukimbia, alichukuliwa kwamba si bikira tena. Kama
mwanamke alizaliwa huku sehemu zake za siri zikiwa ndogo sana, alikuwa
anachukuliwa kama si bikira.
Ni muhimu pia kutambua kwamba bado kuna tamaduni mpaka leo, kama watu wa
Mashariki ya Kati, ambao bado wanashikilia msimamo kama huu. Na kwa
hakika, hakukuwepo na kipimo kwa wanaume.
Ubikira ni kitu ambacho kilikuwa na nguvu zaidi kwa wanawake tu.
Kulikuwa na tafsiri ndogo sana ya ubikira kwa mwanamume, lakini umuhimu
wa ubikira kwa mwanamke ulikuwa mkubwa zaidi. (Hulka hii bado inaendelea
mpaka leo, wakati ambapo ukweli ni kwamba neno hili linawahusu wanaume
na wanawake pia, lakini bado watu wanadhani kwamba ni ‘suala’ la
wanawake na ndio wanaopaswa kutunza bikira zao.)
Hili linaweza kuwa jambo geni kwetu, lakini ni muhimu kuzingatia kwa
nini ‘utepe’ (hymen) kwa mwanamke ulikuwa unachukuliwa kwa umuhimu
mkubwa – hii ilikuwa ni dalili tosha kwamba kama hakuwa na hali hiyo
basi ni wazi kwamba aliwahi kufanya mapenzi na mwanamume mwingine.
Mwanamke ambaye alikuwa ‘amekata utepe’ alikuwa hana thamani kwa sababu
ilionekana kama ni uzembe wake ndiyo maana ‘utepe’ ukakatika, kama
alivyokuwa mwanamke ambaye kiungo chake cha uzazi kilikuwa kidogo sana.
Kwa maana hiyo, bikira alikuwa mwanamke ambaye angeweza kuthibitishwa
ubikira wake kimwili, hakuwahi kupitishwa uume kwenye uke wake.
Na tena hakukuwa na kipimo kwa mwanamume kuhusu suala hili. Kwahiyo
kutafsiri ubikira siyo rahisi kama tunavyoweza kufikiria sasa, na
tafsiri imebadilika kutoka ile ya kale na sasa.
Jinsia nyingine?
Tafsiri ya sasa, inayowahusu wanaume na wanawake, iko kama hivi: Kama
umefanya ngono (kuingiliana kimwili), basi wewe siyo bikira.
Fikiria kama kiungo cha kiume hakijahusika hapo? Ina maana kwamba
wasagaji wawili ambao hawajawahi kukutana na mwanamume hata mara moja,
lakini wamekuwa wakisagana pengine kwa miaka mingi wanaweza kuwa bado
bikira? Hata kama wana uzoefu wa masuala ya mahaba? Inaweza kuwa hivyo,
kutegemeana na tafsiri yako mwenyewe!
Lakini katika hili, huwezi kusema kwamba wanawake hawa wawili bado
bikira kwa sababu hawajawahi kukutana na mwanamume ingawa wana uzoefu wa
ngono. Kukutana kwao kwa mara ya kwanza na kufanya mapenzi ya kusagana,
wakajitosheleza wenyewe namna walivyojua, tayari kuliwatoa bikira kwa
sababu tangu dakika ile waliweza kutambua raha ya mapenzi. Hisia zao
zote zilikuwa kwenye ngono na kwa hakika waliweza hata kufikia mshindo
na wanaendelea kufanya hivyo. Tofauti yao pekee ni kule kutoingiliwa na
mwanamume tu.
Na vipi kuhusu kumwingilia mtu kinyume na maumbile, yaani kwa mashoga?
Mwanamume ambaye ni shoga na mwingine ambaye ni ‘basha’ ambao hawajawahi
kufanya mapenzi na mwanamke wanaweza kuendelea kujiita ni bikira kwa
sababu tu wanafanya mapenzi kinyume cha maumbile? Kitendo hicho hakiwezi
kuwa kimeipoteza bikira yao? Kuna baadhi ya tamaduni, ingawa si nyingi,
ambazo zinaruhusu mapenzi ya kinyume cha maumbile kwa mwanamke na
mwanamume ili tu kuilinda bikira ya mwanamke. Binti anaweza kuwa
anampenda mwanamume, lakini kwa kuwa mila zinamtaka akiolewa akutwe na
bikira, anaridhia kufanya mapenzi kinyume cha maumbile na mwanamume
ampendaye ili ailinde bikira! Unashangaa? Wenyewe wanajijua. Sasa kama
kujamiiana kinyume na maumbile siyo muafaka, vipi kwa wanaume kwa
wanaume?
Tafsiri hii huwa ngumu zaidi kwa watu ambao ni bisexual, yaani wanaoweza
kufanya mapenzi na watu wa jinsia mbili tofauti. Je, huyu anaweza kuwa
bado bikira kama atafanya mapenzi na mtu wa jinsia yake na kisha kufanya
mapenzi na mtu wa jinsia tofauti?
Hapa tena hakuna neno rahisi kwa suala hili la kihisia, kama ubikira
unatafsiriwa kwa mtu kuingiliana kimwili na mtu wa jinsia tofauti. Na
pamoja na ukweli kwamba mtu anaweza akafikiri kitu fulani na kukielezea
vizuri, kile ambacho kinathaminiwa na mila huonekana ndicho muhimu
zaidi.
Mtu aliyebakwa
Dhana halisi ya bikira ni mtu ambaye hana uzoefu kuhusu kujamiiana kwa
mwanamke na mwanamume, lakini haiishii hapo. Pamoja na hayo pia kuna
wazo la mtu fulani ambaye anaweza akawa na msongo wa mawazo, asiye na
uhakika, au hana uzoefu wa kile kinachoweza kuwafurahisha au namna ya
kumridhisha mwenzake – jambo ambalo linaweza kufanana na mtu ambaye
amedhalilishwa ama kubakwa. Na kusema kwamba kuingiliwa huko kunaweza
kukawa mwanzo wa kuelewa utamu wa ngono katu hakuna nafasi hapa kwa
sababu hakulingani na hisia za mtu aliyeridhia kufanya ngono na yule
aliyelazimishwa ingawa wote wameshiriki tendo la ngono kimwili.
Uzoefu wakati mwingine unaonekana kama kitu ambacho mtu mwingine
anajifunza. Ni dhahiri kwamba mtu ambaye amebakwa hajajifunza kitu
chochote kinachoweza kufurahisha, na anakuwa hawezi kuwa na hamu ya
kujifunza. Na kusema kwamba kuingiliana kimwili kwa mwanamke na
mwanamume kwa mara ya kwanza kama ndiko kutolewa bikira kutaitweza
furaha ya mtu huyu na hatakuwa na uzoefu wowote.
No comments:
Post a Comment