"Siku zote angalia ulichonacho na siyo kile ambacho hauna, kwa sababu siyo kile dunia inachokichukua ndiyo kinachohesabika ila ni kile ulichonacho na jinsi unavyokitumia".
Tukienda na ukweli kuwepo kwa furaha kwenye maisha ya mtu haimaanishi ndo ya kuwa mtu huyo huwa hana matatizo, ukiwa katika hali ngumu na ukaona wenzako wanafuraha haimaanishi maisha yao ni mazuri sana kuzidi ya kwako, sema wanakuwa na uwezo mkubwa wa uvumilivu na wanaangalia zaidi kile walichonacho na si vile walivyovipoteza, maisha ni mawimbi hupanda na kushuka, kinachokupasa ni kutokata tamaa na kusonga mbele.
Siku zote angalia ulichonacho na siyo kile ambacho hauna, kwa sababu siyo kile dunia inachokichukua ndo kinachohesabika ila ni kile ulichonacho na jinsi unavyokitumia.
Kiumeni.com imekuandalia mambo 8 ya kuangalia wakati maisha yakienda kombo na kukufanya kukosa nguvu na hali ya kupigana nayo.
- #1, Maumivu ni sehemu ya ukuaji.
Kama kiumeni.com tunavyosema mambo mazuri hayahitaji haraka, kuwa mvumilivu na ijenge akili yako kwa mawazo chanya na kila kitu kitakuwa sawa, japo haviwezi kubadilika na kuwa sawa muda huo huo, kuwa na subira lazima yatakuwa sawa.
Kumbuka kuna aina mbili za maumivu, maumivu yanayokuuma na maumivu yanayokujenga na kukubadilisha, ukiwa unaendelea na maisha yako usiyapinge, maumivu yote mawili yatakusaidia ukuwe kimaisha.
- #2, Kila kitu kwenye maisha ni cha muda mfupi.
Kwa hiyo kama kuna vitu havikuendei sawa sasa hivi, jua matatizo yatapita na mwangaza utakuja. Sio kwa sababu maisha ni magumu ndo yasikufanye usitabasamu, na sio kwa sababu kuna kitu kinakusumbua ndo kisikufanye usicheke, kila kipindi kinakupa fursa mpya na mwisho mwingine, unapata nafasi ya pili ya kujirekebisha mambo yako na makosa yako kwa kila sekunde, unachotakiwa ni kuichukua na kuitumia vizuri.
- #3, Wasiwasi na lawama haziwezi kubadilisha kitu.
Ukiitumia leo unalaumu kuhusu jana, haitofanya kesho kuwa rahisi na yenye mafanikio, chukua hatua na chukua ulichojifunza na endeleza maisha yako, fanya mabadiliko na usiangalie nyuma.
Kwa chochote kinachotokea, kumbuka furaha ya kweli huanza kuingia pindi
unapoacha lawama kuhusu matatizo yako na badala yake kutumia huo muda
kuyaelewa na kuelekeza nguvu kuyatatua matatizo yako.
- #4, Makovu yako ni alama ya ujasiri wako.
Usiyaonee aibu makovu maisha yaliyokuachia, makovu humaanisha maumivu
yamekwisha na kidonda kimepona, pia humaanisha umeyashinda maumivu
yaliyosababishwa na miangaiko ya maisha yako, hakikisha umejifunza vyema
somo ulilopatiwa kutokana na hayo makovu, kuwa mjasiri zaidi na endelea
kusonga mbele.
- #5, Kila mahangaiko unayopitia ni hatua ya kusonga mbele.
Kama unakitaka hicho kitu lazima utakitimiza ili mradi uwe na husuda
pamoja na maamuzi ya kukitaka bila kuangalia na kujali kharaha
unazozipata pamoja na mahangaiko unayoyapitia maana ndo hatua zenyewe za
kusonga mbele.
- #6, Kelele za watu wengine zisikufanye wewe kutokuendelea.
Ni asili ya watu kuongea, kwa lolote na chochote ufanyacho lazima yupo
atakaekuwa na mawazo tofauti na wewe, usiangushwe moyo, kuwa na msimamo
na jambo lako.
- #7, Kama ipo, ipo Tu.
Huwezi lazimisha vitu vitokee ila unaweza kuvisababisha vitokee kwa
kufanya mambo kwa nia na juhudi kubwa, hata kama mambo yakienda vibaya
ndo uelewa wako unavyozidi kukuwa zaidi juu ya hilo jambo linalokusumbua
na kumaanisha utafanya vizuri zaidi mara nyingine maana mafundisho
mazuri na muhimu katika maisha huwa tunajifunza wakati maisha yanapokuwa
magumu au pindi tunapokua tumefanya makosa katika maisha.
Penda maisha yako, jiamini hasa kwenye mambo yanayokuwa yamegusa maisha yako na amini maamuzi unayokua umeyafanya, amini fikra zako na tumia nafasi vizuri pale zinapojitokeza, usin'gang'anie mambo ila tumia njia mbadala kwa kuyachunguza matatizo yako na kuyaelewa hapo unaweza kuelekeza nguvu zako zote kuyatatua, usitumie papara na kutaka kutumia nguvu kulazimisha kitu kitokee bali kuwa na subira na sababisha jambo kutokea kwa kutumia akili yako ipasavyo badala ya kulazimisha, sawa sawa na ulazimishe hii tivotu iliyokutayarishia haya makala kuitwa waulizewanawake.com wakati kiuhalisia inaitwa kiumeni.com, maana kama ipo ipo tu.
Penda maisha yako, jiamini hasa kwenye mambo yanayokuwa yamegusa maisha yako na amini maamuzi unayokua umeyafanya, amini fikra zako na tumia nafasi vizuri pale zinapojitokeza, usin'gang'anie mambo ila tumia njia mbadala kwa kuyachunguza matatizo yako na kuyaelewa hapo unaweza kuelekeza nguvu zako zote kuyatatua, usitumie papara na kutaka kutumia nguvu kulazimisha kitu kitokee bali kuwa na subira na sababisha jambo kutokea kwa kutumia akili yako ipasavyo badala ya kulazimisha, sawa sawa na ulazimishe hii tivotu iliyokutayarishia haya makala kuitwa waulizewanawake.com wakati kiuhalisia inaitwa kiumeni.com, maana kama ipo ipo tu.
- #8, Kitu kizuri unachoweza kukifanya ni kuendelea kufanya unachofanya kwa juhudi.
Maisha ni magumu ila wewe ni mgumu zaidi, tafuta nguvu za kucheka kila
siku, tafuta ujasiri wa kufanya na kujisikia utofauti wenye kupendeza,
tafuta njia kwenye moyo wako kufanya na wengine watabasamu, pia usijipe
msongo wa mawazo kwa vitu ambavyo huwezi kuvibadilisha, ishi maisha
huru, penda kwa upendo, ongea kwa wema na ukweli, fanya kazi kwa bidii
na hata kama mafanikio huyaoni ongeza bidii zaidi na endelea kufanya unachofanya. Endelea kukua.
Kiumeni.com inakupa ushauri wa vitu vya kufanya kila siku asubuhi mara umkapo,
- Amka ukiwa na fikra chanya.
- Kula kwa afya.
- Fanya mazoezi kuulinda mwili wako, kuupa nguvu na kuupendezesha.
- Usiwe na wasiwasi sana.
- Kuwa na juhudi kwenye kazi na bidii.
- Tabasamu na cheka mara kwa mara.
- Lala vizuri.
Uwanja ni wako.
Ni kitu gani kinachokusaidia wakati mambo yako yakienda vibaya?.
Ni fikra gani chanya unayoifikiria kichwani mwako wakati kila kitu kikienda vibaya?.
Toa maoni yako ndani ya kiumeni.com hapo chini na shirikisha mawazo yako kwa watu wengine.
No comments:
Post a Comment