Shoga baada ya wiki iliyopita kuongelea raha ya mchezo kushangilia,
nilipata meseji za kutosha na wengine wakiniambia wamefanyia kazi na
kufurahia chakula cha usiku. Shoga mwenzako huwa nafarijika sana kama
ninachokufunza hapa unakifanyia kazi na unafurahia, upo somo?
Basi baada ya hayo shoga, nikuwekee hapa kile ambacho umekisoma kwa
ufupi hapo juu na kutamani ukione kwa urefu. Kama nakuona vile
ulivyovuta pumzi shoga wangu mie maana si kwa kutoa macho huko, utasema
si wa nchi hii! Ehhheee heeee heeiya shoga, upo? Shoga, asikudanganye
mtu siku hizi kila kitu kinataka maandalizi, mfano unapokuwa mjamzito ni
vyema ukafanya maandalizi ya kumlea mtoto utakayemzaa.
Mnapotaka kuanza ujenzi wa nyumba au kufungua biashara na mumeo, lazima
maandalizi yawepo kwani bila kufanya hivyo mtakwama tu. Si kwa hayo tu,
hata ukimpata mchumba ili muingie kwenye hatua ya ndoa lazima maandalizi
yawepo ndiyo maana kuna kitchen part , send off
kisha ndoa na harusi inamalizia.
kisha ndoa na harusi inamalizia.
Baada ya kufuatwa na shoga yetu mmoja ambaye sitamtaja kwa jina na
kunilalamikia kuhusu mumewe kutokuwa na mushawasha wa yale mambo yetu,
nimegundua kinachofanya mzee asiwe na hamu naye ni kukosa maandalizi.
Shoga, hakuna jambo baya kama mwanamke kutokuwa mbunifu wa kumuandaa
mzee ili akiwa kazini mawazo yote yawe kwake huku akijisemea moyoni;
“Leo usiku nitampa mambo mazuri mke wangu hadi afurahi na roho yake.”
Kauli hiyo haiwezi kuja hivihivi bila wewe mwanamke kumwandaa mzee
akaandalika kweli kuanzia asubuhi anapojiandaa kwenda kazini na akiwa
kazini. Kama usiku wa siku hiyo alikufurahisha na bado kiu yako
haijaisha, kabla hajaondoka msifie kwa vimbwanga vyake vya usiku na
mwambie kama isingekuwa kwenda kazini bado ulikuwa unamhitaji. Kauli
hiyo itamfanya mzee anapoondoka kuelekea kibaruani, mawazo yote kuwa
kwako na kupanga atakapomaliza kazi kutopitia kokote zaidi ya kurudi
nyumbani kukufurahisha.
Akiwa kazini, mtumie meseji ya malovee kwamba umemmis sana na unatamani
akufanyie mambo mazuri kama aliyokufanyia usiku.Hapo utakuwa umemroga
bila kwenda kwa sangoma, na ukijua anakaribia kumaliza kazi mpigie simu
zungumza naye kwa sauti ya mahabati, hapo utamfanya mzee kusisimka na
atatoka huko akiwa na hasira za kukupa penzi shatashata.
Kwa leo niishie hapa shoga wangu wa ukwee maana mimi tena kwa kuachiwa
nafasi kidogo natiririka kama mvua za msituni! Tukutane tena wiki ijayo
kwa mada nyingine tamu zaidi, upo?
No comments:
Post a Comment