Unajua nini?
Haipaswi kuwa hivi ndo maana bongoswaggz ipo kwa ajili yako ili kumaliza maswala madogo madogo kama haya, kukuondoa katika mazingira ya kutokua na maamuzi dhabiti na kutokujua nini cha kufanya ndani ya sekta ya utongozaji na kukufanya uwe mwanaume kiongozi na mtanashati kwa kujua ni nini cha kufanya na mda gani unapaswa kukifanya ili kuwa mtaalamu katika sekta ya mahusiano.
Haipaswi kuwa hivi ndo maana bongoswaggz ipo kwa ajili yako ili kumaliza maswala madogo madogo kama haya, kukuondoa katika mazingira ya kutokua na maamuzi dhabiti na kutokujua nini cha kufanya ndani ya sekta ya utongozaji na kukufanya uwe mwanaume kiongozi na mtanashati kwa kujua ni nini cha kufanya na mda gani unapaswa kukifanya ili kuwa mtaalamu katika sekta ya mahusiano.
Kujiamini
ni kitu kinachochukua nafasi kubwa na ndo msingi mkubwa katika
mahusiano na hasa wakati wa utongozaji, na ndicho kitu mwanamke hutumia
kumpima mwanaume na kumpa nafasi ya uwezekano wa kuwa na yeye au la, ila
mara nyingi mtu hushindwa kujiamini kutokana na hofu ya kutokujua ni
nini cha kufanya au kuongea wakati wa utongozaji.
Mwanamme
ambaye huwa hafanikiwi kwenye utongozaji hufanya makosa madogo madogo
kama kumpandisha hadhi mwanamke anayemtongoza mpaka kiasi ambacho
anaifanya hadhi yake binafsi kuonekana ndogo na siyo tu anamtongoza
mwanamke kwa wasiwasi na kutojiamini, bali anamtongoza hovyo hovyo bila
mpangilio na zaidi ya hapo anamuweka wazi mwanamke kwamba anataka kumjua
zaidi ya kawaida na anajitangaza bila kujijua kwamba, anahitaji na huyo
mwanamke apendezwe naye hapo hapo.
Nayajua
haya kwa sababu kwa muda mrefu na mimi msichana nilikua hivi hivi
nawaona wanaume jinsi wanavyojikanyaga, mtaalamu wa utongozaji huwa
anasubira na huwa hapaparuki hovyo hovyo tu, kutongoza ni sanaa na
inahitaji uelewa mkubwa na hata mimi iwapo ningelikua ndo huyo mwanamke
sidhani kama ningelikubali hivi hivi, lazima atake kukujua kwanza ndo
mambo mengine yafuate.
Ukitaka
kuishia kusonywa na matusi juu ingia na mstari wa "Dada samahani
nimetokea kukupenda nataka tuwe wote, kila nikikaa nakuwaza wewe,
nikinywa maji nakuona kwenye glasi", bila kuangalia mazingira na papara
za kusema yaliyo moyoni mwako, huu mstari lazima utakutokea puani,
mwanadada ndo amekuona siku hiyo hiyo, hata alikua hajui mtu kama wewe
upo katika hii dunia, hakujui na unategemea akuambie anakupenda pia, we
vipi?, hapo unapoteza nafasi na utaishia kuambiwa usiyoyataka na kuumia
moyo tu.
Naamini
kabisa mwanaume yeyote mwenye mtazamo sahihi na mwenye hamu ya
kujifunza anaweza kuelewa jinsi ya kutongoza mwanamke sehemu yeyote na
mahali popote pale, kutongoza hakuitaji kukalili mistari ya kutongozea
wala kumpulizia dawa kutoka kwa mganga, kama unania ya kujifunza endelea
kusoma nakala za waulizewanaume.
Mwanaume
mtongozaji hajishushi na anatumia mbinu ya kuonyesha ujasiri wa
kimaongezi na akiongea na mwanamke, mwanamke hutambua ya kuwa huyu jamaa
ana nia naye kutokana na lugha anayoitumia wakati wa maongezi.
Makosa
makubwa mawili ambayo hufanya wanaume wakati wa kutaka kumtongoza
msichana, ni kusubiri na kusita kwa muda mrefu na kutojua nini cha
kuzungumza.
Kama ni kwenye sherehe ndipo ulipomuona, piga moyo konde na mwendee na mwambie,
>>"Nimekuona kutoka mbali ila moyo wangu ukang'ang'ania mpaka nije nikusalimie, mambo?"
>>"Siku yako inaendaje?"
>>"Upo upande wa bibi harusi au bwana harusi?"
>>"Oooh, upande wa bibi harusi, ndo maana dada yako amewahi kuolewa!, ukoo wenu mzima inavyoonyesha umelaaniwa kwa uzuri!"
Mchokoze
kwa maneno matamu, muulize maswali ya kumfanya afurahie maongezi na
kama ukiwa unatoa sifa ifiche ndani ya sentensi inayovutia, ukitaka
kumjua uliza maswali ambayo majibu yake ni mepesi na rahisi, kama
ukitaka kujua anachofanya muulize,
>>"Kwa hiyo familia nzima mwanafunzi amebaki ni wewe tu, maana dada yako tayari ameshaolewa?"
Kwa
maswali ya namna hio atajikuta anajiongelea kuhusu yeye na kukufanya
akuzoee mapema, na ukiona maongezi yanaelekea ukingoni unatakiwa unakuwa
shapu na mbunifu kwa kuanzisha mada nyingine inayovutia zaidi,
itakayoleta maongezi matamu zaidi.
Kujua
kitu cha kusema wakati wa kutongoza ni ngumu, ila inabidi ujiamini na
ufanye kujisahau na kuweka akili kama upo unaongea na dada yako ila
maongezi yaweke yawe ya kuvutia zaidi na uyapambe kwa sifa bila
kuonyesha nia yako moja kwa moja, mwisho wa maongezi muombe namba ya
simu au omba umtoe mtoko akuonyeshe maeneo hayo maana wewe ni mgeni na
maongezi yamekupendezea na ungependa kuyaendeleza siku nyingine.
Acha
kuwa na wasiwasi na kufikiria nini cha kuongea, we mfate kwanza na
maongezi yatajitengeneza yenyewe kwa jinsi ya mazingira mliyopo na weka
akilini kitu kimoja, huyo msichana unayeenda kumtongoza inawezekana
anatongozwa mara tano au zaidi kwa siku tokea alipokuwa na miaka kumi na
nane, kwa hiyo inawezekana ameshatongozwa zaidi ya mara 1000, kwa hiyo
usifanye vitu ambavyo ameshavizoea kila siku na kuishia kutoa maamuzi ya
kutokubali maombi yako kama wengine waliokataliwa waliotoa maombi yao
hapo mwanzo kabla yako, kuwa mbunifu na tumia mazingira yako kwa usahihi
na uzuri zaidi.
Hakikisha katika maongezi yako usiongelee wala kugusia vitu vifuatavyo,
- Usimsifie sana, atakuona kama unambeza.
- Usijaribu wala kumuuliza kama ana mtu, ana mshikaji wake au anamahusiano na mtu yeyote yule.
- Usimuulize maswali magumu ambayo yanahitaji uelewa wa kitu fulani.
Vitu vifuatavyo ni ambavyo hutakiwi kuvifanya wakati wa utongozaji,
- Usiongee kwa sauti ya juu sana,
- Usijibu kitu au jambo kwa haraka sana,
- Usiwe unaondoka ondoka au kuhamisha mapozi, usiwe na papara na kuwa mtulivu.
Kitu cha kuweka akilini zaidi usifikilie sana unachokiongelea, ukifikiria sana utakaribisha wasi wasi na kutokujiamini.
Wakati wa maongezi yako ya utongozaji, hakikisha unahusisha mambo yafuatayo,
- Vitu ambavyo anashauku navyo na anavipendelea,
- Vitu ambavyo unashauku navyo,
- Hadithi zenye vichekesho na mguso wa mahaba,
- Jifunze jinsi ya kuhadithia hadithi za kuvutia,
- Mfanye acheke na kutabasamu kwa kile unachokiona,
- Michezo ya furaha na ya kuvutia,
- Unaweza kujikweza kidogo ila usipitilize.
No comments:
Post a Comment